Msemajiwao
JF-Expert Member
- Sep 12, 2016
- 670
- 1,664
Habari ndugu wazazi wenzangu!
Jana nilifanikiwa kuhudhuria kikao cha wazazi pale ugindoni primary iliyopi kigamboni!
Kikao kiliitishwa na maafisa wafuatao kutoka manispaa;
1. Afisa Maendeleo ya Jamii
2. Afisa Lishe
3. Afisa mmoja kutoka ofisi ya takukuru (w)
Walitueleza vyema umhimu wa watoto kupata chakula muda wa mchana, Hili kila mzazi aliafiki kabisa kwamba ni vyema watoto wapate chakula!
Lakini cha kushangaza wengi ni pale baada ya maafisa hao kutoa maelezo pasipo mjadala wao wenyewe waliamua yafuatayo kwamba tuyapitishe.
1. Eti wazazi tuchangie pesa ya vyombo vya mpishi.
2. Mpishi WALIKUJA nae hapo waliyemuandaa wao kwamba ndiye anayestahili kupikia watoto wetu chakula kwa mchango wa tsh 1000/= kwa siku.
Baada ya kumtambulisha mtu huyo, wazazi tuliomba kuwepo mchakato wa kutangaza tenda ili washindanishwe wengine kuliko kuja na mtu wao mfukoni ambaye hana vigezo.
Baada ya kuomba mchakato wa chakula uzingatie tenda, Maafisa hao walikasirika na kutishia kususia kikao endapo tusipoafiki mawazo yao!
Maswali yalikuwa mengi lakini miongoni mwa maswali?
Mpishi wao huyo alishawahi kupikia watoto wa darasa la mtihani (la nne na la saba) tulichanga elfu 3000 chakula!
Lakini watoto walipewa ugali mbichi na viharage vitatu vya kuhesabu na rundo la mchuzi!
Je, mtu huyo kama alishindwa kupika kwa elfu 3 watoto wachache, angewezaje kupika chakula kwa 1000 shule nzima yenye watoto karibu 1400?
Hili jambo la kupikia watoto shuleni ni zuri lakini wasimamizi wetu wanaligeuza dili kiasi cha kukosa maana halisi ya kupikia watoto shule!
Naomba kufikisha mapendekezo kwa wizara hili jambo maafisa ngazi za wilaya pamoja na walimu wanatukwaza sana wazazi katika kutekeleza maendeleo ya jamii!
Nashauri ni bora tuboreshe yafuatayo!
Ni afadhali kila shule itenge eneo la mamalishe binafsi watakaopika chakula kwa gharama zao wauze!
Ili watoto wachague pa kwenda kununua wenyewe! Ili ikitokea mmoja akiuza chakula kibovu watoto wasinunue chakula kwake apate hasara mwenyewe!
Suala la chakula mashuleni kwa sampuli ya maafisa wetu hawa ni kujidanganya tu!
Pia soma: Mchengerwa: Wanafunzi wote wa kutwa wapate chakula shuleni