Nyerere alikiasa chama chake kwamba yale mazuri yafuateni,mabaya yaacheni aende nayo,Chama Chake Pendwa kimechukua Maovu yake kimezika mazuri yake.
Watanzania tulikuwa tunashirikiana kwa kila nyanja bila kujali Ukanda ua dini zetu.Hata alipoanzisha vyama vingi bado hatukuchukiana kwa kiasi tunachokiona leo.Wengi tulikuwa hatuelewi lakini hakuna mahali Mpinzani aliitwa Lofa,Mpumbavu,hovyo au Nyumbu.
Leo tumegawanywa kama kuku waendao sokoni,huko kuna atakyepikwa supu,pilau,au kukaangwa.Jamani sisi watanzania sote ni sawa.
Watawala msitujengee chuki na uhasama.Vyama vya siasa viko kulingana na Katiba na sheria ya nchi