Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 2,742
- 4,104
Septemba 16 2024 Dunia ilipata taarifa kuwa Sean Combs ametiwa nguvuni na mamlaka na kuzua gumzo kubwa sana katika vyombo vya habari duniani, siku chache baadaye chombo cha habari cha TMZ kilitangazia dunia kuwa katika nyumba ya Combs kumekutwa zaidi ya chumba elfu moja za mafuta ya watoto (Baby Oil), kila kona tarifa zikafika kuwa mafuta hayo yalitumika kama kilainishi wakati wa faragha kitu ambacho watu wengi wameungana kukubaliana kwa kauli moja.
Binafsi sitaki kusema kama Combs hana hatia na hilo liwe wazi kabsa, ila ajabu ni kuona namna ambavyo content creators wengi duniani wamekuwa wakisubiria vitu vya kina fulani viumane kwanza ndipo waingie kwenye capcut watengeneze video pamoja na audio ambazo zina maudhui ya kuonesha aidha maisha ya Sean Combs.
Sio kila mtu ni content creator wengine tubakie watazamaji tu, haina maana umenunua Samsung A15 na upo na bando la Halotel la mwezi mzma basi unaweza kuwa content creator, uongo huo.
Kila content creator anataka kuchukua njia rahisi na hii imeonekana wazi katika wiki mbili zilizopita ambapo ukiingia kwenye mtandao wa kijamii wa Tiktok basi kwenye video kumi ungekutana na video zenye uhusiano wa kesi ya Sean Combs.
Unakutana na content creator ana followers wasiozidi elfu moja basi anaona njia bora ya kupata engagement ni kuweka maudhui ya Sean Combs na mada kuhusu baby oils. Hawataki kuweka maudhui ambayo yatawafanya watanzania wajifunze kupitia video hizo. Hawataki kutumia akili zao kutafuta fikra mpya za kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Angalia karibu na jamii yako, kuna mabilioni ya vyanzo vya maudhui- vitabu, sinema, muziki, vyakula, watu, na hata uzoefu wa maisha ya watu. Lakini content creator hawa hukaa hapo na kufikiria masuala yasiyo na tija.
Sio ajabu kuona kuna kurasa za tiktok ambazo ni mahususi kwa ajili ya kufundisha watu kuhusu DIY (Do It Yourself) wakionesha namna ya kupika vyakula, au kutumia pasi ya mkaa, ni rahisi kuona wakionesha utamaduni wao huku wakijipatia followers wengi, video fupi ya dakika 1 na sekunde ishirini unakuta ina views zaidi ya Milioni 2 na like zaidi ya milioni moja. Inasikitisha.
Unajua kwa nini? Kwa sababu content creators wetu hawana ujasiri wa kujifunza wafanye vitu gani zaidi ya maeneo yao ya kawaida, kazi ni pranks za kijinga na kipuuzi tu.
Unajua kwa nini? Kwa sababu content creators wetu hawana ujasiri wa kujifunza wafanye vitu gani zaidi ya maeneo yao ya kawaida, kazi ni pranks za kijinga na kipuuzi tu.
Hakuna cha msingi kama content creator utaenda kuanzia fujo katika kijiwe cha kahawa huku mwenzio akikurekodi kisha jioni uichapishe tiktok upate views! Kisa eti Prank? Je ukipigwa na kujeruhiwa, hasara inakuwa kwa nani?
Unawapatia challenge watu mitaa kuwa watafune pilipili za Carolina Reaper pamoja na Ghost Pepper ili uwapatie elfu 20, je unadhani uchungu na ukali hizi pilipili utapungua kwa kumpa mtu elfu 20? Unahitaji kufanya kazi zaidi, kufikiria, na kuja na wazo lenye mantiki.
Unaweka wimbo wa Vivian kisha utuoneshe matackle na maziwer, vijana wa ovyo wataitazama na kukuachia likes nyingi tu ila misingi ya umewapatia nini jamii yako? ungetaka hivyo ungekwenda kuweka video zako Onlyfans.
Content creators kwa sasa wanatumia mitandao kwa minadhiri ya ajabu sana, mara huyu nauza shanga na vikuku, mara huyu amekuwa mwalimu wa mahusiano kwa wanawake wakati hapo alipo ana ndoa tatu zimevunjika.
Tafuta pembe na mwanga ambao hakuna mtu mwingine amekwisha kuona, tengeneza kitu upige pesa huku watu wanachukua vitu chanya kwenye bidhaa na huduma yako.
Kuna mdau mmoja aliwahi kusema kama Meli ya Titanic ingelipata ajali mwaka 2024 basi database ya Tiktok, Snapchat pamoja Instagram zimeelemewa kwani wahanga wa ajali wangekuwa busy kuonesha namna ambavyo meli imegonga mwamba, namna ambavyo kuna baridi kali, hapo ungekuta mtu anaipa kipaumbele simu yake kisa tu alifungua akaunti ya tiktok na nywila hazifahamu hivyo kwake yeye wafuasi milioni 1 na laki 9 waliopo tiktok pamoja na wafuasi laki 8 kwenye mtandao wa Instagram ni wa muhimu kuliko hata maisha yake.
Kesi ya Sean Combs ikifika tamati na kufungwa jela, je hawa content creators waliojikita zaidi kuonesha maisha ya Sean Combs, Baby Oils pamoja na kuandika upya mashairi ya nyimbo zake, hawa content creators watafanya nini?
Watasubiri tena mtu mwingine kiumane ndo waanze tena kufanya contents? Ni wazi kuwa Sean Combs amekosea sana tena sana ila namna watu wa mtandao wanavyomuongea na kumkandia kwenye contents zao ni kama vile tokea kuumbwa kwa dunia, huyu ndo mdhambi mkuu.
Hakuna contents kumhusu Charles Albright, hakuna video kuhusu upuuzi ambao Rodney James Alcala, sio mitandao ya kijamii wala online television hakuna masimulizi kuhusu unyama wa Johhny Joe Avalos, hatujasikia contents creator wakielezea kwa upana suala ya Shlomo Erez Helbrans wala kuhusu Josh Duggar.
Kinachomtokea sasa hivi Khabane Lame huko mitandaoni ndo ufinyu wa kuja na maudhui mapya ili kuvutia zaidi hadhira yako, kila siku unakula maudhui yale yale mwisho utahama utachoka? Sio kitu cha ajabu kukuta akaunti yako yenye wafuasi milioni 1 asubuhi ikiwa na wafuasi 2000.