Kwa nilichokiona kwenye sherehe za uapisho wa Rais Kagame Rwanda, tuna la kujifunza kutoka kwao!

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
6,705
16,739
Hakika zile sherehe zilifaana sana kuanzia maandalizi, muonekano, mpangilio na protoko isee hawa wenzetu wameweza na wanajua kweli. wenzetu si wakispot spot wanania kweli ya jambo na inaonekana wakiamua kitu lazima wafanye.


Kwetu tanzania tunaweza kufanya zaidi ya wao kama tu tutapangilia vizuri mambo yetu huku kinachotuanguza kamati za maandalizi unakuta wazee kibao wamejipachika ili tu wapige pesa alafu anavutwa kijana mmoja huyo basi anabebeshwa kila aina ya kazi humo.

Pia soma: Rais Samia kwenda Rwanda Agosti 11, 2024 kuhudhuria uapisho wa Rais Kagame

Hizi sherehe za kitaifa ni muhimu sana ziwe na maandalizi mazuri maana huwa zinabeba utambulisho wetu kimataifa isee. Nina uhakika foreigner wengi walioangalia zile sherehe teyari wameanza kuweka booking kwenda rwanda. mimi pia nimetamani nitembelee rwanda mwaka huu mwishoni.
 
Back
Top Bottom