El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 274
- 508
Jeshi la polisi ni Moja ya taasisi muhimu sana katika ustawi wa nchi yoyote duniani.
Ulinzi wa raia na mali zao ndo kiini cha amani na maendeleo kwa ujumla wake. Wasiwasi nilioupata Juu ya Jeshi letu la polisi ni namna linavyofanya kazi zake. Na kwa Leo nisingependa kuongelea madhaifu yaliyo na baadhi ya polisi wetu kama rushwa, bali kujiuliza kama kweli bado polisi wanaitendea kazi taaluma yao (Professionalism).
Ebu tujiulize, kama kweli tutakuwa salama sisi na mali zetu wakati polisi hawana kabisa upelelezi unaofaa na wa kasi wa matukio ya kijinai.
Hapa karibuni nimejaribu sana kufuatilia kujua iwapo matendo ya kijinai yanapelelezwa vya kutosha na ufuatiliaji makini. Nilishangazwa hakika kuona kinachofanyika hasa ndani ya vituo vya polisi ni kuandika taarifa ya uharifu, ukipenda Report book au RB kama ilivyozoeleka, baada ya hapo hakuna jitihada mahususi za ufuatiliaji.
Hapa nyuma nilishuhudia bwana mmoja jirani ambaye aliibiwa pikipiki yake, baada ya wezi kuruka ukuta na kufanya uharifu huo. Huyu bwana alitoa taarifa na kupewa RB namba. Kwa mawazo yangu nilidhani Sasa polisi wangefika eneo la tukio, kukagua mazingira Yale, na walau kuwahoji watu wengine walioishi eneo lile.
Ajabu, yule bwana alibaki na RB yake mkononi na aliombwa ajitahidi kuchunguzachunguza kujua ni kina nani watakuwa wameiba hiyo pikipiki.
Zamani kidogo, polisi ilipokuwa bado imemakinika, wangekuja eneo la tukio, wangehoji majirani na labda hata ku harrass kiasi Ili kuanza kupata viashiria vya uharifu huo.
Nikajiuliza hiyo polisi ilienda wapi? Hivi unapomwambia raia wa kawaida asiye na taaluma ya upelelezi, na labda hata vyombo vya kitaalamu vya upelelezi, aanze kufanya kazi ya yeye mwenyewe kutafuta mhalifu, hiyo bado ni kazi ya utaalamu? (professionalism).
Kwa Nini tunakuwa na polisi ambao kazi yao ni kuandika RB tu?
Tukio lingine lililonishangaza mpaka kuanza kujiuliza kama kweli bado tuna polisi active na ambao wanaenda na speed ya uharifu kwa maana ya kuuzuia, ni pale ambapo hata mtu angetoa taarifa za uharifu bado tunagundua kwamba mara nyingi hakuna ile Kasi inayotakiwa kwenye kukabili uhalifu huo.
Natumia neno kukabili kwa maana ya counter attack. Ku counter attack ni kulikabili jambo lilijitokeza kwa nguvu ileile.
Ebu nambie, mtu anatoa taarifa ya viashiria vya uharifu mahala. Inachukua muda usiojulikana kwa polisi kuanza kufuatilia . Tena mara nyingi, inamchukua mtoa taarifa, kukumbushia Tena na Tena iwapo kuna ufuatiliaji wowote.
Ebu nambie kwa Dunia hii ambayo, waharifu wako Kasi kutaka kufanya mambo yao, itakuwaje kama bado polisi wetu wanakasi ndogo namna hii ku react juu ya uharifu au hata kushughulikia taarifa zake?
Kuna hatari ya kujikuta tuko katika wakati mbaya kwa kumalizwa na waharifu kwa sababu Kasi yao ya kuteleleza uharifu ni Kali kuliko Kasi ya polisi ya kuzuia huo uharifu.
Nilishuhudia hapa nyuma, mtu mmoja akitoa taarifa kwenye ofisi muhimu ya Jeshi, juu ya kile ambacho, huyu ndugu aliona ni kiashiria halisi cha uharifu wa kijinai. Ajabu mpokea simu ya taarifa alikuwa ni yule tunayemuita huku uraiani " polisi mkubwa".
Kwa mawazo yangu nilidhani, kwa kuwa ni polisi mkubwa amepokea taarifa, basi haraka zingechukuliwa hatua za ufuatiliaji na kujiridhisha kwa polisi juu ya taarifa hiyo.
Wakati narudi kumuuliza yule ndugu kama Kuna mrejesho wowote, alichonieleza ni kwamba, ukiachilia mbali taarifa yenyewe kwa huyo kamanda, hakuwa na hakika kama huyo afande alielewa hata taarifa aliyokuwa akimpa.
Maana anadai, afande alikuwa busy na aliyoyataja kama mambo mengine na angemrudia mtoa taarifa. Ajabu mpaka Leo hakuna mrejesho kwa mtoa taarifa na inaonyesha dhahiri hilo tukio halikufuatiliwa maana bado hali ni ile ile.
Ebu nambie, katika mazingira hayo ambayo polisi hawa act juu ya taarifa kama hiyo, vipi uovu na uharifu ukitawala, kosa litakuwa la nani?
Polisi ndo Wana dhamana kisheria pamoja na mambo mengine kushughulikia uharifu na waharifu.
Hivi kama hawajui kazi zao na kuzifanya kitaalamu ( professionally) hali itakuwaje?
Police, we really trust and have confidence in you. Please,Watch out and execute your mandate professionally.