Kwa muda huu inawezekana kweli

My Mud

Senior Member
Oct 5, 2012
108
17
muhali gani wanajukwaa wezangu!nimemaliza kidato cha nne mwaka 2008 takribani miaka tisa imepita.Kwasasa nimeajiriwa nahitaji kujiendeleza ila lazima nipitie A level .Je ninaweza nikamudu masomo ya a level kwa komb ya pcm maana nimemaliza shule miaka mingi hata yale mafomula ya hesabu nimesahau.
 
Tafuta pesa achana na hiyo miPcm...
 

Kwa ulipofikia kamwe usipoteze muda na A-level. Kama unataka usomevPCM basi unajua ukimaliza A-level pia unataka usome nn chuo. Muda ndo huu tafuta chuo kizuri ukasome diploma. Angalia DIT, Arusha tech au MUST, moja kati ya sehemu hizo itakufaa kwa PCM unayoitaka. Ukitaka kupoteza miaka miwili then ujilaumu nenda A-level. Huko utasoma miaka miwili bila kujua upo kundi la kukosa au lah. Ila chui kila semester unakua unajua ukaze au ulegeze.
 
Sema unataka kuja kusomea nini chuo naamini wanajukwaa watakupa ushauri mzuri kama kuna ulazima wa kupitia F6 au kuna njia mbadala.
 
nataka kusoma mechanical engineering lakini kusoma kwangu kutategemea mkopo wa body kwani nitaomba likizo bila malipo kutokana kwamba fani hiyo ni tofauti na fani ninayo tumikia sasa. ningechukua hata diploma ila kwa sasa sina uwezo wa kumudu ada na gharama zingine kwa miaka mitatu ya masomo nikiwa sipokei mshahara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…