Kuelekea 2025 Kwa mtazamo wangu Mbowe na Lissu ni vita zaidi ya nje kuliko ya ndani. Ni mwendelezo wa Zitto na Maria Sarungi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
596
450
Miaka ya 2010 wakati Zitto Zuberi Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wanaanza kujenga “picha ya kundi ndani ya Chadema” kwa lengo la kuchukua kiti cha Freeman Mbowe (FAM) CHADEMA, mambo kadhaa yalikuwa dhahiri na yanaweza kulinganishwa kwa kiwango kikubwa kwa mizania na mlinganisho na hali ya sasa.

Mosi; Jina la Maria Sarungi liko katikati. Alikuwa karibu sana na kundi hili na ukaribu wake ulikuwa wenye mrengo wa kuunga mkono hoja zao hususan zile zenye mashambulizi na kukibagaza CHADEMA. Leo ukaribu huo haupo kama tu ilivyokuwa kwa watu wengine kama Maxience Melo, Eric Kabendera nk. Kazi iliisha, maslahi yameisha.

Sasa Maria ni mkaribu wa Lissu (TAL) ingawa anajitahidi kuonesha na kushawishi ukaribu na FAM, lakini historia inaonyesha tofauti kubwa. Aidha, kupitia space yake alijenga “informal contact” na viongozi wengi wa CHADEMA. Alitumia “lack of political space” na “fear of lack of political visibility”. It was sort of informal institution ambayo nashangaa CDM seniors went in full with exception ya FAM na JJM

Pili; Zitto Kabwe (ZZK) alikuwa amejenga umaarufu mkubwa ndani na nje ya chama chake. Akiamini kwamba haukutokana na chama chake. Umaarufu wake kwa kuwa ulienda sambamba na kukibagaza CHADEMA ulipata hata uungaji mkono wa wabaya wa CHADEMA na wana CCM kupitia kumwona kama instrument. Ilikuwa fursa kukigawa. Pambio zilichochewa kwelikweli kumwonesha ni wa pekee.

TAL naye hali ni hiyohiyo kwa sasa. Pambio ni kama zilezile za ZZK. Kumjenga kipekee. Tofauti ni moja tu, CCM hawamwoni kama instrument, ila wabaya wa CHADEMA wanamuunga mkono. Hawa hawataki kuona CHADEMA ikiwa thabiti. Wanataka kuona hali ya nchi ikiwa unstable, wadumishe status quo maana inawapa benefits. Ni ambao kwa muda wote ni wakosoaji na wabagazaji wa CHADEMA. Si wanachama wa CHADEMA.

TAL anapitishwa katikati yao na kwa wanachama wa CHADEMA ambao kwa kuwaangalia ni majeruhi wa michakato ya kisiasa ndani ya CHADEMA au kwa muda tayari kupitia instruments za Maria Sarungi tayari wako mkobani mwake na wakati huohuo wakiwa ndani ya CHADEMA.

Sina hakika na ukubwa, nafasi na ushawishi wa kundi hili la wana CHADEMA kumpa ushindi TAL lakini pia hatma yake kama akishindwa, ambayo ni very likely given the circumstances na kama Mbowe atagombea. Ni dhahiri, haiwezi kuwa CHADEMA.

Tatu; ZZK aliamini ushawishi wake itakuwa mwisho wa CHADEMA kama akitoka. Kwa pambio zilivyokuwa alijaa upepo akiamini ana wafuasi na timu kubwa within the party ranks na wanachama. But this didn’t materialize. Ingawa similar situation kama nilivyoeleza iko likely kutokea kwa TAL, but kuna tofauti kidogo.

ZZK alikuwa tayari politically alienated na downgraded. But mkutano wa TAL wa kutangaza nia umeshaonesha dalili wazi compare to FAM’s gathering. Saying that; tayari TAL alishaanza kuwa downgraded and mistrusted, though not for long enough compare to ZZK. Approach yake ya kushambulia viongozi wenzake inaongeza zaidi tatizo. Haoneshi kuwa na nia ya kubaki jumuishi na integrated regardless the results, which is surprising. Anatafuta nafasi kwa kutoboa mtumbwi aliomo.

Nne, kuna kitu kinaitwa ACT Wazalendo. Ilianza kazi mapema tu similar to current situation of kitu kinaitwa Sauti ya Wananchi. ZZK exit was to ACT Wazalendo. TAL japo hataji exit mwenendo wake “ni wa kujaribu” kugombea.

Amesukumwa na msukumo wa ghafla, ambao upepo wake unaweza kuhojika sana. Hawezi eleza current political trends pekee kama sababu. Kuna jambo zaidi. Hapa ni possible Sauti ya Wananchi platform. Championed by Boniface Mwabukusi, Dr. Slaa and co. Of course Maria Sarungi also within. Walijaribu kuichota CHADEMA from within ikashindikana. But through TAL exit this may work out. Remember a registered pending political party? Nitarudi…

Jambo la tano na mwisho kwa sasa. TAL like ZZK ameshaanza lugha za mapema za CHADEMA ina jasho, mali na uwekezaji wake. ZZK said exactly the same prior to exit. Peter Msigwa too, similar sentiments.

Kauli za namna hii tayari zinajenga flashpoint for possible warfare. Basically ana set platforms for future confrontations. As I said anajaribu within ili kujenga kwingine. Anajiandaa kukibagaza CHADEMA akiwa ndani ili mbeleni iwe rahisi.
 
Uzi mzur sana .

Tofaut ya TAL na ZZK ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri

ZZK alikuwa na back up ya deepstate, lakini zaid alikuwa ameshaandaa chama..

TL hana uwezo, narudia hana uwezo wa ku run any significant political party so far
SyW imejaa wanaharakati na watu wanaodhani siasa ni harakati na kufokea watawala muda wote...

Hoja zao zimejengwa kwenye msingi wa chuki, majungu na fitina dhidi ya Mbowe.

Hao kina Mwabukusi, Slaa, Lissu, Libe, Mwakitwange, ni loosers.,

Hawana back up tofaut na Mbowe..

Mbowe asipopenda TL awe Chairman hawi.. hata afanyeje..

Back up ya hilo kundi pia yupo Heche na Lema Godbless.... Hawa nadhan ni zaid ya tunachokiona...

Mbowe ana memba wengi sana KK lakini Strategically aligned to Deep state..

Hoja zao za Jasho na Damu lengo lake ni hate politics... Kufanarakanisha na kudai siasa za confrontation.....

Kwa hakika baada ya Uchaguzi CDM haitabaki moja.. lakini agenda za TAL ni evil... Hata akishinda ataendeleza majungu na kukiua hiki chama, aidha amsingizie mwenyekiti mambo mengi maovu kwamba he did this and that for the past 20years alaf akimbie.

Kumbuka TL yupo Tanzania nusu nusu, familia yake yote ipo nje na watoto ni iraia wa US.. hili pekee linatosha kuonyesha namna analipa fadhila kwa 'baadhi' ya diaspora na hao loyal partnes wake.

Hao hao 'baadhi' ya Diaspora kuna kipindi walianzisha bla bla dhidi ya JF, Max akawapiga chini ..., wakaamua kukomaa na Clubhouse na Magrouo ya Whatsap.

Its a virus within the body, Mbowe awe smart, eitha akiondoe au aish nacho kwa mkakati huku akikitengenezea dawa...dawa zipo nyingi sana sana.....
 
Chagua kuandika kwa lugha moja ili ueleweke.
Si kweli TAL anaungwa mkono na wasio itakia mema CHADEMA.

Ushahidi ni hapa JF wale chawa wote wa CCM wanampigia kampeni Mbowe na kumbagaza Lissu.
Hii U turn gani imekujaje ghafla hivi?
Jibu n hili Mbowe anaungwa mkono na CCM Kwa sababu ya mapendano na mafungamano ya wazi wazi bila kificho aliyonayo Kwa CCM.
Kwangu Mbowe ndiye anayetumika kuwakwamisha CHADEMA kusonga mbele maana yupo hapo kutetea maslahi binafsi ya SACCOS yake.
Something smells fishy.
 
Hapa jf sio ushahidi, tupo tunatumia I'd zaidi ya 10 kwa one member. 3 za CCM, 3 za Lissu na 3 za Mbowe. Inategemea unataka comment ipi tu
 
Kuna Siasa za Upinzani za aina mbili.
Aina ya kwanza ndiyo hii tunayoiona Zanzibar na Bara siku zote.
Zanzibar Maalim Seif "anasemekana" kashinda, lakini mwisho wa siku anaridhia kushindwa na kuwa sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Aina hii ndiyo iliyopo Tanzania Bara.
Tunaishia kusikia kwamba "inasemekana" Lowassa alishinda, lakini akatangazwa JPM.
Hizi ni Siasa za kuchoshana.
Kupotezeana muda.
Hazina manufaa kwa Taifa.
Siasa za aina ya pili, ni Siasa za Jino kwa Jino.
Akishinda CCM, ashinde kihalali.
Akishinda ACT Wazalendo, ashinde kihalali.
Akishinda CHADEMA, ashinde kihalali.
Na dawa yake ni moja tu.
Refarii asiegemee upande wowote.
Kama Refarii hawi Huru, pesa za Walipa Kodi zisipotee kuendesha Chaguzi za kipuuzi.
Hizi ndiyo Siasa zitakazoiletea Nchi yetu heshima.
Kama hakuna TUME HURU YA UCHAGUZI, tuitangaze Tanzania kuwa Nchi ya Kifalme.
Mfalme akiwa CCM.
Lakini kama tunasema Nchi yetu ni ya Kidemokrasia, Tume ya Uchaguzi iwe Huru.
La sivyo tusipoteze pesa kufanya Chaguzi zisizo Huru wala za haki.
CHADEMA wanapasa kuachana na Siasa zilizo zoeleka.
CHADEMA, Chama Kikuu cha Upinzani, kianze Siasa za kuiheshimisha Tanzania.
Siasa ambazo wakongwe hawaziwezi.
 
Mkuu heshima kwako,

Kwanza hizo ndio zimekuwa siasa za Tanzania kwa miaka yote tangu siasa za vyama vingi mwaka 95..

Kwenye mimbari ya Vyama vya siasa ni zaid ya tunayoyaona kwa macho...

Game zake sio rahisi... Hata CCM wanaotaka mabadiliko wapo.... Ila ni kugumu sana...

Kuna siasa za kitanzania na siasa za nchi nyingine...

Inaumiza lakini tusisahau duniani matabaka ni mawili tu.

Tabaka tawala na tabaka tawaliwa...

Hakuna katikati...
Na hakuna mshindi wa jumla maana kuna watakaopenda, kuchukia, kususa, kupuuza nk...

Siasa zote duniani ni "ubabaishaji"
Media zinajioanga zina create watu....

Its a rude world.
 
Hizi "conspiracy theory" sijui huwa mnazitoa wapi!!!
Kwa nini tunapenda sana kuwa mbele ya wakati kama wapiga ramli!!?
Mimi ni muumini wa ukweli usio na shaka, yaani ukweli unaosindikizwa na ushahidi.

Kuna mtu anatengeneza "supremacy" kwa manufaa yake ya baadaye.
 
Uzi mzur sana .

Tofaut ya TAL na ZZK ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri

ZZK alikuwa na back up ya deepstate, lakini zaid alikuwa ameshaandaa chama..

TL hana uwezo, narudia hana uwezo wa ku run any significant political party so far
SyW imejaa wanaharakati na watu wanaodhani siasa ni harakati na kufokea watawala muda wote...

Hoja zao zimejengwa kwenye msingi wa chuki, majungu na fitina dhidi ya Mbowe.

Hao kina Mwabukusi, Slaa, Lissu, Libe, Mwakitwange, ni loosers.,

Hawana back up tofaut na Mbowe..

Mbowe asipopenda TL awe Chairman hawi.. hata afanyeje..

Back up ya hilo kundi pia yupo Heche na Lema Godbless.... Hawa nadhan ni zaid ya tunachokiona...

Mbowe ana memba wengi sana KK lakini Strategically aligned to Deep state..

Hoja zao za Jasho na Damu lengo lake ni hate politics... Kufanarakanisha na kudai siasa za confrontation.....

Kwa hakika baada ya Uchaguzi CDM haitabaki moja.. lakini agenda za TAL ni evil... Hata akishinda ataendeleza majungu na kukiua hiki chama, aidha amsingizie mwenyekiti mambo mengi maovu kwamba he did this and that for the past 20years alaf akimbie.

Kumbuka TL yupo Tanzania nusu nusu, familia yake yote ipo nje na watoto ni iraia wa US.. hili pekee linatosha kuonyesha namna analipa fadhila kwa 'baadhi' ya diaspora na hao loyal partnes wake.

Hao hao 'baadhi' ya Diaspora kuna kipindi walianzisha bla bla dhidi ya JF, Max akawapiga chini ..., wakaamua kukomaa na Clubhouse na Magrouo ya Whatsap.

Its a virus within the body, Mbowe awe smart, eitha akiondoe au aish nacho kwa mkakati huku akikitengenezea dawa...dawa zipo nyingi sana sana.....
Hoja zako zimejaa M.afiii
 
Wanataka kuona hali ya nchi ikiwa unstable, wadumishe status quo maana inawapa benefits.
Hii Nchi iko Stable?! Wakati Watu wanatekwa na kuuwawa na wengine kuikimbia Nchi stability gani hiyo?.

Na kama Uchaguzi wa ndani CHADEMA hautakuwa HURU na HAKI ukigubikwa na RUSHWA au UKABILA basi namshauri Lissu afungue Chama tutamfuata.
 
Binafsi sio mwanasiasa na sina chama! Mimi huwa natafakari kwanini LISU ali survive zile risasi, madhira yote aliyopitia, kubali au kataa LISU akiwa mwenyekiti, akaenda kupambana na SSH, Lisu anapita! Wapiga kura wengi kwa sasa hawana habari na zidumu fikira za mwenyekiti. Kizazi cha sasa kinataka watu wa aina ya Lisu, calibre za akina JPM, akikohoa, amekohoa! Yakobo wa biblia, alikuwa mtu mjanjamnja, lakini bado Mungu akamtumia kujitengenezea Taifa Lake! Vivyohivyo, pamoja na mapungufu ya Lisu, ujanjaujanja na hila zinazosemwa, bado anaweza akatumiwa na Mungu!
 
Chagua kuandika kwa lugha moja ili ueleweke.
Si kweli TAL anaungwa mkono na wasio itakia mema CHADEMA.

Ushahidi ni hapa JF wale chawa wote wa CCM wanampigia kampeni Mbowe na kumbagaza Lissu.
Hii U turn gani imekujaje ghafla hivi?
Jibu n hili Mbowe anaungwa mkono na CCM Kwa sababu ya mapendano na mafungamano ya wazi wazi bila kificho aliyonayo Kwa CCM.
Kwangu Mbowe ndiye anayetumika kuwakwamisha CHADEMA kusonga mbele maana yupo hapo kutetea maslahi binafsi ya SACCOS yake.
Something smells fishy.
Mbowe hakwamishi chadema ila ni mtu asiyependa siasa zenye kuleta fujo zisizo na sababu. Mbowe anapenda diplomasia katika kuleta maelewano mf maridhiano na serikali ya CCM ingawa CCM hawataki maridhiano.Pia je, wewe unayetaka Chadema kusonga mbele Kwa kusababisha maandamano yenye kusababisha nguvu za Dola kutumia silaha unapata faida Gani? Watanzania wenye mapenzi mema hasa vyama vya siasa vya upinzani wenye mapenzi mema mnapaswa kuunganisha nguvu ya pamoja kudai KATIBA MPYA, na TUME HURU YA UCHAGUZI maana ndiyo msingi wa mambo yote. Chaguzi za ndani katika vyama Kwa nini ziwe mtego wa kuleta utengano wa viongozi wenye nguvu kama Mbowe na Lisu? Wanasiasa wa Tanzania, angalieni yasijirudie Yale mambo ya Dr Slaa na Hayati Lowasa ya 2015. Malumbano yasiyo natija.Angalieni sana.Unganeni Kwa sasa kudai mambo ya msingi kabla ya UCHAGUZI ujao.
 
Uzi mzur sana .

Tofaut ya TAL na ZZK ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri

ZZK alikuwa na back up ya deepstate, lakini zaid alikuwa ameshaandaa chama..

TL hana uwezo, narudia hana uwezo wa ku run any significant political party so far
SyW imejaa wanaharakati na watu wanaodhani siasa ni harakati na kufokea watawala muda wote...

Hoja zao zimejengwa kwenye msingi wa chuki, majungu na fitina dhidi ya Mbowe.

Hao kina Mwabukusi, Slaa, Lissu, Libe, Mwakitwange, ni loosers.,

Hawana back up tofaut na Mbowe..

Mbowe asipopenda TL awe Chairman hawi.. hata afanyeje..

Back up ya hilo kundi pia yupo Heche na Lema Godbless.... Hawa nadhan ni zaid ya tunachokiona...

Mbowe ana memba wengi sana KK lakini Strategically aligned to Deep state..

Hoja zao za Jasho na Damu lengo lake ni hate politics... Kufanarakanisha na kudai siasa za confrontation.....

Kwa hakika baada ya Uchaguzi CDM haitabaki moja.. lakini agenda za TAL ni evil... Hata akishinda ataendeleza majungu na kukiua hiki chama, aidha amsingizie mwenyekiti mambo mengi maovu kwamba he did this and that for the past 20years alaf akimbie.

Kumbuka TL yupo Tanzania nusu nusu, familia yake yote ipo nje na watoto ni iraia wa US.. hili pekee linatosha kuonyesha namna analipa fadhila kwa 'baadhi' ya diaspora na hao loyal partnes wake.

Hao hao 'baadhi' ya Diaspora kuna kipindi walianzisha bla bla dhidi ya JF, Max akawapiga chini ..., wakaamua kukomaa na Clubhouse na Magrouo ya Whatsap.

It’s a virus within the body, Mbowe awe smart, eitha akiondoe au aish nacho kwa mkakati huku akikitengenezea dawa...dawa zipo nyingi sana sana.....
Kimsingi tunafikiri sawa. Hiyo ya deep state nimeonesha kwamba probably TAL hana lakini ana mfumo ulio nje ya chama zaidi kuliko within ndiyo maana anashambulia na kukibagaza chama chake hata kwa gharama ya reputation. Lengo ni ku set future benchmarks. Tayari KK Lema is out. Maria Sarungi ameanza kuchokonoa akina Heche waoneshe msimamo. Basically ni political game ambayo players ni wa nje zaidi. Mitandaoni. Ambao wengi wamekuwa si na mishale na chuki kwa Mbowe bali na CHADEMA yenyewe. Hawataki kuona uthabiti wa CHADEMA ili kuipa nafuu dola. Maria Sarungi basically ni state set trap…
 
TAL anakwenda kuiua CHADAME, huwezi kuwa na washauri wa ovyo kama Maria ukabaki salama. kitakachowaumiza zaidi nje ya CHADEMA they are nothing, hawawezi kuanzisha chama kipya na ACT hawawezi kulea upuuzi wao. Ingekua ni lissu tu angeweza kungana vizuri na ACT ila kundi llilokuepo nyuma yake ni toxic.
 
Hoja zako zimejaa M.afiii
Brainwashed...
Kimsingi tunafikiri sawa. Hiyo ya deep state nimeonesha kwamba probably TAL hana lakini ana mfumo ulio nje ya chama zaidi kuliko within ndiyo maana anashambulia na kukibagaza chama chake hata kwa gharama ya reputation. Lengo ni ku set future benchmarks. Tayari KK Lema is out. Maria Sarungi ameanza kuchokonoa akina Heche waoneshe msimamo. Basically ni political game ambayo players ni wa nje zaidi. Mitandaoni. Ambao wengi wamekuwa si na mishale na chuki kwa Mbowe bali na CHADEMA yenyewe. Hawataki kuona uthabiti wa CHADEMA ili kuipa nafuu dola. Maria Sarungi basically ni state set trap…
Safi sana mkuu,

Exactly! This is entirely an outsider political game... (Loosers game)

Ilinichukua muda sana kujua hilo kuhusu Maria

Bahati mbaya sana anatumia vijana wadogo, wakumia anaanza bla bla... Nadhani na Soka ni mmoja wao...

Sasaivi anamtumia Fred na wengine, anajificha kwenye kichaka cha activism radicalism and confrontation kitu ambacho Tanzania hakifanyi kazi.
Ipo mifano mingi sana ambayo haikuwahi kufanikiwa kwenye siasa radical Tanzania ukianza na Kambona, Mrema, Hamad Sheriff Hamad, Segondo Mvungi, nk

Hata Tundu asipokuwa makini nae akishakabidhiwa CDM mambo yatakuwa haya haya kama tunayoyaona leo kwa FAM

Kwa bahati mbaya sana TL sio mvumilivu, wataratuana hadharani in 2 to 3 years time from now.

Kuna kila dalili FAM will play smart katika hili na atamuachia TL kiti japo kwa Muda ku mprove Wrong.

Wafuasi wa FAM watakuwa na busara na kukubali maamuzi ya FAM na Outside Pressure wakijua kabisa TL wont run the show as promised, na ataachia chama mapema pengine kuliko Makani kwa excuse ya Democracy and blabla.

Muda ni msema kweli.
 
Nothing new here than SPECULATION 🤔🤔
 
Speculation, an activity of finding possible answers by guessing without having enough evidence 😅🤣😅🤣
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Hii Nchi iko Stable?! Wakati Watu wanatekwa na kuuwawa na wengine kuikimbia Nchi stability gani hiyo?.

Na kama Uchaguzi wa ndani CHADEMA hautakuwa HURU na HAKI ukigubikwa na RUSHWA au UKABILA basi namshauri Lissu afungue Chama tutamfuata.
Vipi akishindwa kihalali?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom