Kwa mliowahi au mnaomiliki Gari ni Ushauri gani mnatoa kwa wanaotaka kumiliki Gari

image.jpg
Gari ya mkononi yoyote huna haja ya kumuita fundi juma akagaue mzee peleka ifanywe inspection report kisha ndo ukiridshwa na report lipia. Jamaa zangu wako hapo mikocheni wana mashine nzuri sana na its 40k - kila part mashine inakagua tena gari ikiwa on - engine compression gear box mpaka tires .
 
1. Nini wazingatie wanaotaka kununua gari kwa mara ya kwanza??

1. Nunua gari unayoweza kuimudu, kwa kuanzia anza na Toyota (kuna wdau wanataka kuosha vinywa hapa)...

2. Hakikisha una uwezo wa kuwa na akiba ya pesa kwa ajili ya huduma ndogo ndogo za gari...

3. Gari ni matokeo ya teknolojia, hivyo jipe muda wa kujua baadhi ya vitu vidogo vidogo kuhusu mifumo ya gari, watu wengi wanajua tu kulifanta gari liende lakini hawajui kung'amua matatizo ya gari kabla hayajawa ugonjwa sugu...

4. Jifunze sheria za usalama barabarani, kuwa mvumilivu na mwenye maamuzi ya busara uwapo nyuma ya uskani. Jinsi miaka inavyoenda magari yamekuwa yakiemdeshwa na wehu wasiojali kabisa usalama wa wengine...

2. "Share experience" yako kuhusu kumiliki gari

Haina tofauti na kumiliki mali nyingine yeyote...
 
View attachment 3042086Gari ya mkononi yoyote huna haja ya kumuita fundi juma akagaue mzee peleka ifanywe inspection report kisha ndo ukiridshwa na report lipia. Jamaa zangu wako hapo mikocheni wana mashine nzuri sana na its 40k - kila part mashine inakagua tena gari ikiwa on - engine compression gear box mpaka tires .

Mikocheni sehemu gani?

Maana gereji karibu zote zilizopo Mik9cheni zina mafundi matapeli tu...
 
Unaponunua Gari kwa mara ya kwanza hakikisha haununui mikononi kwa mtu. Jichange uagize nje, au uende Showroom.

NINAEKUPA HUO USHAURI, SINA GARI WALA BAISKELI.

PambanaZaidi/CottonandMore

Mie hushauri kinyume chake kama HALIJUI GARI KABISA!

Nilianza na gari ya mkononi ya bei rahisi kabisa, familia yangu yote ndiyo tulijifunzia hilo! Sikupata gari mbovu ila kuhangaika na mafundi hapa na pale kulinifanya niijue gari ipasavyo!! Nilipoagiza gari ya thamani hakukuwa na lena kwangu hivyo gari mpya ilikuwa safe na pia nilikuwa nishaijua mifumo yote ya magari na vitu muhimu vya kuangalia kila wakati!!

Nilijifunza kwa staff mwenzangu aliagiza cresta enzi hizo akiwa hajui gari kabisa, wiki ile ile akagonga kiemoro cha barabarani! Kidogo awe kichaa maana kilifumua mpaka engine ila alisevu maana angeangukia korongoni!!

Mwingine aliagiza Rav4 enzi hizo, hakujua habari za kucheki maji wala oil!! Kilichotokea gari ilikaa benchi mwaka mzima ikisubiri mshahara upate ahueni akope tena!!

All in all kaona ushauri wako, kaona wangu atapima uzito wa kipato chake na kuamua vyema!
 
Chakwanza hakikisha wewe ni dereva.
Ndugu, hakikisha wewe ni dereva aisee....

Achana na magari ya bei rahisi. Sio gari zenye thamani ndogo, namaanisha gari zilizovunjwa bei, gari ya mil 12 uuziwe mil5 uone umeula, kimbia mbalii.. achana na magari yaliyovunjwa bei.

NB: Mkuu hili lamwisho sio la muhimu sana ila ukiweza achana na passo 😁😁.

Gari yangu yakwanza kununua nilinunua mil 2.5 😁😁. Story yake sitaisimulia, ila tunatoka mbali sana
 
Gari nzuri kwa matumizi ya kawaida hata ya safari binafsi za mbali.

1. Jitahidi upate leseni, sio zile za mchongo, jifunze ulifahamu kabisa namna ya kuendesha.

2. Jitahidi usichange breki na accelerator utakuja kunishukuru

3. Make sure gari unakaa nalo walau miezi 6 hadi mwaka bila kwenda gereji, shida ziwe ndogo ndogo za pancha na services tu

4. Anza na gari ndogo isiyo na cc kubwa kama Carina au Corolla

5. Usishike shike simu au radio while driving, it's very risk

6. Kuwa makini na boda boda hasa kama ni mgeni wa kuendesha gari highway
 
Mwezi iliyopita nilikua mkoa flani hivi nilikutana huko na rafiki yangu mmoja aliajiriwa mwaka 2008 kama mwalimu wa sec. Anasema aliamua kukopa fedha Kwa akili ya kununua ndinga hapo mwezi Nov 2010.
Kipindi hicho hakuna na majukumu mengi. Mshahara unaobaki baada ya Mankato akatumia kununua mafuta na service. Anasema ikafikia kipindi gari ikawa inakula vizuri kuliko yeye.
Mwaka 2018 hiyo ndinga ilipata ajali na kufanya idai pesa nyingi ili irudi kuwa hai.
Anasema Leo hana nyumba, mikopo mingi hajalipa na mwanae wa kwanza Yuko chuo.
Akanishauri kwamba nikipata viela nisihangaike na gari kwani zitaniyumbisha.
Nb.
Ushauri huu ni kama maoni pia ya jamaa. Nimemsikiliza ka redio nna mpango wa kununua ndinga hapo mwaka 2025 baada tu ya election
 
Back
Top Bottom