Kwa Milioni 30, UTT amis na nyumba ya kupangisha kipi bora?

Fene

JF-Expert Member
May 4, 2021
2,808
4,415
Salaaam Wachumi

Rejea mada hapo juu
Je upi ni uwekezaji ulio bora endapo katika harakat zako za utafutaji ukajaaliwa umeishika 30Mil cash
Na option ukawa umeweka ni hizo mbili kati ya kuwekeza utt amis ambapo kwa utafiti niliofanya humu return yake yaweza kuwa 250k-300k per month
Na kujenga nyumba ya kupangisha ambapo return yake kwa uwekezaji wa 30Mil naamin pia wazoefu watatoa muangaza
Nb/ katika ujenzi wa nyumba tuna assume kiwanja bado

JE NI UPI UWEKEZAJI ULIO BORA KATI YA HIVYO KWA MTAZAMO WAKO?
 
Kama Bado upo una fight(umri below 40), nakushauri wekeza utt. Lakini kama una familia na unasomesha, tafuta mradi wa maana. Nyumba ya kupanga siyo mradi wa maana zaidi ya mmiliki kukopesheka kwenye taasisi za kifedha.

Nje ya mada...
Anawezaje mtu amiliki 30m kupitia akili isiyoweza kufannya maamuzi magumu? Au ulishinda bahati nasibu?
 
Jenga nyumba utakula mafao mpaka unazeeka
Hyo mirad ya maana ndo ipi mkuu?? Taja tufaidike wengi
Nyumba ya kupanga siyo mradi wa kutegemea. Payback period yake ni kubwa, kuwadai Wapangaji Kodi ni stress. Kuna kipindi wapangaji wanaadimika, Gharama za uchakavu nk.

Miradi mizuri ni kama kilimo Cha kisasa, ufugaji wa kisasa, biashara ya vipuli vya magari na pikipiki NK
 
Huu msemo huwa siuelewi. Real estate ndo biashara inayoweza kukupa kipato kizuri na inakufanya ukopesheke kiwepesi sana na taasisi za fedha as long as una mzunguko.

Nyumba za kukodisha na kupanga ni biashara salama kuliko hizo zote ulizotaja.

Ila, Kama biashara nyingine inatakiwa kufanya utafiti unanunua kiwanja wapi na nyumba utazijienga za aina gani na kwanini. Ukikosea hili unaingia hasara ila hasara si ya moja kwa moja kama ukiingia hasara katka kilimo sijui uchuuzi. Angalau nyumba inakuwepo pale unaweza kuuza au kukopea bank na kujaribu jambo lingine.
 
Nyumba za kukodisha na kupanga ni biashara salama kuliko hizo zote ulizotaja.
Boss, milioni 30 unajenga nyumba ya namna gani, na kwa mji kama wa Dar, ikakamilika kuwa chanzo cha mapato? Eneo lipi?

Fanya uwanja unao tayari, boma unalisimamisha kwa 10m - 12m, ikianza kuongeo kiinglishi tu, 30 imekata na bado hujafikia kupangisha!

Atafute shughuli, awekeze angalau 12m, aone muelekeo, ikitiki, aongeze mtaji
 
Upo sawa kuwa 30M ni ndogo kwenye ujenzi kutegemeana na aina ya ujenzi. Ila hiyo ya biashara ni yale yale tu. Hujawahi fanya biashara huna wa kukushika mkono kukuambia pita hapa, kanunue pale, uza hapa kitakachokukuta ni mwishoni huna biashara, huna pesa afadhali hata aliyejenga ikabaki finishi anaweza ingia bank akachukua morgage akamaliza iwapo tu eneo ni zuri kibiashara.
 
Sio ndgo. Mjini 30 ml unsshusha vyumba vya kupanga. Tuna mifano hai.
 
Ok boss, ndo maana nikasema ni ndogo kutegemeana na aina ya ujenzi. Yaani unajenga nini.
Sio ndogo 30m watu vimeshuka vyumba viwili na sebule, 2
Chumba master hata 7
Chumba sebule 4
Wewe unaujua ujenzi kweli wa nyumba za kupanga. Sio nyumba yako. Nyumba za kupanga.
Inatosha sana. No option yako unataka nn.
UTT kwa 30m uwongo. Jenga nyumba. Pambana. Alafu hela peleka sasa utt.
 
Upo sawa sikupingi. Nimesema ni ndogo kutegemeana na aina ya ujenzi.
 
Back
Top Bottom