Kwa mechi ya jana Madini Fc Vs Simba Sc bado tunasafari ndefu.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Jana Nikiwa Sheik Amri Abeid Stadium Arusha Kufuatilia Mtanange kati Ya vijana Wa Madini Fc ambaye alikua Mwenyeji na Simba Sc Mgeni kuna vitu ambavyo nimeviona Havipendezi katika Soka.

Simba Baada ya kutumia Geti Kubwa kuingia uwanjani Wao Walitumia Uwanja unaotumiwa na Mashabiki kuingia Uwanjani tena Kwa Miguu na baadaye ndo basi lao likaingia likiwa tupu Sijajua walimaanisha nini.

Tumeshuhudia Timu kadhaa zikipigwa faini kwa kosa la wachezaji wake kutotumia Milango ya Kawaida kuingia uwanjani Nahisi faini hazitoshi ndio maana Kila siku hizi timu zinarudia makosa yale yale.

Ushauri kwa TFF watengeneze Sheria kali kuhusu hili ikiwa ni Pamoja na Timu husika kupokwa pointi 3 kama Adhabu kwa Vitendo hivi.

Jana Uwanja ulivunja Rekodi kwa kuingiza watu ila cha Ajabu Mashabiki karibia wote walikua wa Simba japokuwa Madini fc anatoka Arusha,Niwapongeze sana WanaMbeya kuzipenda timu zao.

Ushauri Chama cha Mkoa wa Arusha Wajipange kuhakikisha Mkoa unapata Timu Shiriki Ligi kuu.
 
Soka la bongo ni upuuzi mtupu, yani hata huko Arusha nao ni wapuuzi kiasi hiki kutosupport timu yao!
Mbeya hawanaga ujinga kama huu.
 
watu wa Arusha ushamba umezidi eti wanashangilia simba wapuuzi sana mbeya ndio kuna watu wenye akili wanasapoti timu yao mbeya city
 
Kumbuka hao Madini wamezoea sana hivyo viwanja vibovu kwa sababu wanacheza ligi daraja la pili ambapo viwanja vingi ni vibovu,,
 
Acheni watu wafurahie munyama anavyotafuna.Madini washangile wanaapolo.Simba ndiyo timu ambayo watu wengi walipoanza kushabikia mpira,waliikuta inang'aa.Sasa washabikie madini wakati wako Arusha hata Tanzanite hawajawahi kuiona!
 
Arusha ni jiji kubwa lenye utajiri mkubwa na watu wengi sana, ila kilichonikera nimefika pale saa 8:45 nakuta tiketi zimeisha, uwanja umejaa na hata walioko nje na tiketi hawaruhusiwi kuingia ndani, yani soka linaendeshwa kihuni huni sana. TFF wanaandaa tiketi nyingi kuliko uwezo wa uwanja. Arusha wameonesha mapenzi ya soka lakini viongozi wa vilabu kama Simba na Yanga hata hawaoni fursa ya kuingiza kipato kupitia Arusha, mashabiki wengi lakini hakuna clubs inachofaidi kiuchumi. Poor viongozi
 
Soka la bongo ni upuuzi mtupu, yani hata huko Arusha nao ni wapuuzi kiasi hiki kutosupport timu yao!
Mbeya hawanaga ujinga kama huu.
Kama soka bongo ni upuuzi hata wewe unayefuatilia na kutoa comment ni mpuuzi zaidi
 
watu wa Arusha ushamba umezidi eti wanashangilia simba wapuuzi sana mbeya ndio kuna watu wenye akili wanasapoti timu yao mbeya city
Kila mtu hushabikia timu anayopenda hatulazimishwi wewe kama unaipenda madini kashabikie sisi wana wa chuga SIMBA DAM DAM
 
simba na yanga ni za dar....arusha watafute timu yao...haiwezekani mji mdogo kama njombe unatimu arusha jiji kubwa hakuna timu
 
Mimi Kuanzia Saa sita mchana nlikua tayari nipo ndani sijapata usumbufu mkubwa nasikia mapato ni milioni 80 kwa vile viingilio ya buku 5 na 7 tu.

Arusha wanahitaji uwanja mkubwa wa Mpira na pia timu ligi kuu
 
simba na yanga ni za dar....arusha watafute timu yao...haiwezekani mji mdogo kama njombe unatimu arusha jiji kubwa hakuna timu
halafu cha ajabu Ukivaa tsheti za Yanga wanakupiga,kuna mtoto amekuja pale amepiga pamba zake za Yanga wanamzuia mtoto hata mwaka mmoja hana kaja na wazaz wake
 

Achana na Simba yetu tafadhali Mkuu. Nenda kamtafutie Kocha wako Mkuu chupi yake iliyobebwa na maji na sasa imegotea pale katika Bwawa lenu Klabuni Jangwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…