Kwa maslahi mapana ya chadema, Nawashauri wenye busara wamuombe mbowe kwa hekima akinusuru chama asigombee

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,640
22,285
Naamini mzee mbowe ni mzee mwenye maono makubwa sana.

Kwa busara zake nashauri apate ushauri mwingine kutoka kwa wazee asigombee amuunge mkono Tundu lissu kama baba mlezi wa chama!

Chadema ni mtoto aliyezaliwa na mgumba na kutelekezwa matunzo;
Mbowe ni mama mzazi wa mtoto na Tundu lissu ni mama mlezi hivyo wasigombanie nani wa kumlea mtoto huyu wa dawa!
Wazingatie zaidi afya bora ya mtoto chadema!

Tundu lissu yupo tayali kumlea mtoto huyu aliyekosa matunzo,

Lakini Mbowe anaona bora mtoto auwawe wagawane mwili wakazike kama yeye hatomlea mwenyewe!
Chadema ni chama cha siasa siyo kampuni binafsi.

Wapo wapi wazee wenye hekima wakamwambie Mbowe kwamba haitampunguzia kitu kwake kumpa Tundu lissu nafasi.

Hata Mussa alimwachia kijiti Joshua pamoja na ulemavu wake!

Wako wapi vijana wasio na uchawa chadema ili wamuombe mbowe apumzike!?

Ccm katika hili wanahakikisha kuni hazikati moto, ACT inafungua mageti kuwa chama kikuu cha uponzani!

Mwenye masikio na asikie saa 48 zinakaribia.
 
Chama kimejaa watu wajinga hicho kuliko kile ambacho tunakidhania. Huu mchakato wa uchaguzi umenifunulia mengi sana.

Mtu waliyemuuza kwetu ili tumchague awe Rais wa nchi leo wanamtukana wanasema hana uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama chao.
 
Huo uamuzi wa mbowe ndio utamuonesha haswa yeye ni mtu wa namna gani, na anasimamia nini..
Frankly suala la lissu kuwa chairman ni muhimu kuliko chochote kwa sasa.
what I do believe is: Mbowe atamuunga mkono Lisu, japo system inamshawishi sana Mbowe asifanye hivyo. Utashi wa Mbowe autumie ipasavyo
 
Chama kimejaa watu wajinga hicho kuliko kile ambacho tunakidhania. Huu mchakato wa uchaguzi umenifunulia mengi sana.

Mtu waliyemuuza kwetu ili tumchague awe Rais wa nchi leo wanamtukana wanasema hana uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama chao.
Umenena mkuu
 
Namshukuru Tundu amefanya mengi yamekuwa wazi, na wakae nae makini sana wasimchezee rafu za kijinga atawaumbua vibaya sana.

Tusisahau kwa sasa hapa Tanzania hakuna mwanasiasa wa upunzani msafi na anayeaminika kama Tundu.
Wampe nafasi tu
 
Freeman alkaeli mbowe ni Bonge la mwanasiasa hata sisi CCM Tunamtaka Mbowe ili tupate wa kushindana nae ...kuliko mkimleta huyo ANTI paslisu wenu ...tutampasua mapema sana!

Bora abakie mbowe tupambane
 
Mtu waliyemuuza kwetu ili tumchague awe Rais wa nchi leo wanamtukana wanasema hana uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama chao.
HOJA NZITO sana hii hakuna wa kuijibu, Yericko alijaribu akaishia kujiaibisha tu.
 
Uchaguzi haina tatizo per se.
In fact, nadhani yeyote atakayeshinda wanaweza kukiunganisha Chama baada ya Uchaguzi.
 
Back
Top Bottom