Kuelekea 2025 Kwa kuangalia historia na matendo ya Mbunge wako unadhani 2025 anaweza kutoboa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,018
3,074
Wakuu mko vyede?

Uchaguzi Mkuu unakuja 2025, tumeshaanza kuona vimbwanga, ukifika mwaka wenyewe wa uchaguzi itakuwa balaa. Sasa hivi wabunge ndio wanakumbuka kurudi majimboni kwao, sasa hivi ndio wanapiga picha na watu wa hali ya chini, sasa hivi ndio wanajifanya wanajua sana kutetea haki za wananchi, yaani ilimradi kunenepesha ng'ombe siku ya mnada.

Kwa kuangalia matendo ya nyuma ya Mbunge wako na vile vyote alivyoahidi kuhakikisha vinatokea jimboni kwake, ukipima na kuchuja makapi unadhani mbunge wako atawaweza kutoboa 2025 au akakeshe kwenye mizimu?

Gwajima (Gwajiboy) mpaka sasa akakeshe tu na mizimu, mbali na ile Rede Cup sioni kingine alichofanya:KEKLaugh::KEKLaugh::KEKLaugh:

Narudisha mpira kwenu wadau.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Jina lake imebidi niingie google nimtafute, maana huko bungeni sijawahi muona hata akigonga meza ni kg tu mwili zinaongezeka.
 
Hakika baba Askofu Gwajima hatoboi, kwetu sisi hapati ata kura ya muumini wake
 
Wakuu mko vyede?

Uchaguzi Mkuu unakuja 2025, tumeshaanza kuona vimbwanga, ukifika mwaka wenyewe wa uchaguzi itakuwa balaa. Sasa hivi wabunge ndio wanakumbuka kurudi majimboni kwao...
sema wabunge wa magufuli wa kuiba kura. hakuna mbunge aliyechaguliwa.
 
sijawahi kuwa na mbunge mimi......utashangaa akina Luhaga na yule Msukuma, kelele na mikwara yoteeee mwisho wa siku watapitisha ile bajeti ya copy and paste ya Mwigulu
 
Sisi watanzania ni wajinga sana hasa vijana wa aina ya mwashambwa.pamoja na mateso yaliyoletwa na ccm bado wataichagua tu ijapokuwa majimbo machache ya watu wanaojielewa.kule kwetu Ruvuma hawajielewi utaona akina mhagama,ngonyani nk wataacha kuchagua maccm.haya kule mby,moro kwa akina tale mambo ni yale yale tu.tuombe Mungu na tuhamasishane kama kule kwa madiba tuone.
 
Uchaguzi wa serikali ya mtaa mwaka huu 2024 utatoa taswira halisi tunakwenda vipi 2025 dhidi ya wabunge lakini hata hivyo naona wenyeviti wengi wa mitaa ni wazembe sana hivyo naona vyama vingine mbalimbali kwa kiasi kikubwa kuchukua nafasi. Ccm ndani ya chama kuanzia tawi kuna mvutano mkubwa na fukuto kubwa sana
 
Huyu wa kwangu hapa Ubungo bwana Kitila Mkumbo sidhani kama atatoboa mimi binafsi hapati kura yangu
 
Back
Top Bottom