Kwa hili lililotokea kariakoo jana kama bado tunahitaji kujifunza na majanga.

Anti-tozo

Member
May 23, 2015
51
52
Basi tutakuwa na vichwa vigumu sana

1.kwa tathmini ya haraka haraka ni majengo mangapi mpaka sasa kariakoo hapo hapo ujenzi unaendelea na biashara bado zinafanyika papo hapo?

2.Tunachukua hatua gani kupitia mfano huu?

3.Bado kwenye swala la kufanya maokozi katika majanga ni changamoto kwetu hii inadhihirisha dhahiri kwamba vitu kama hivi sio priority katika muundo wetu wa taasisi za kukabiliana na majanga

 
litapita na shida watasahau na ndio litakuwa limekwisha mpk litokee tena!.. ujinga mwengine ni watanzania wengi hatushurutishi serikali yetu kufanya mamba kisasa tumekalia kusema Mungu saidia!.. ukweli mchungu ni kwamba hakuna Mungu atakusaidia ukiboronga umeboronga tu!.. hii issue inatakiwa itafune watu wengi sema maneno yatakayokuja ni "kapanga hakuna wa kupangua!"

tunasahau dunia ya sasa ni teknolojia na kuna vitu ukiwanavyo lazima nawe ubadirike kutokana na wewe kuwa na hivyo vitu!, mipango miji wajitafakari pia serikali isajili wajenzi wa majengo kama haya hakuna mtu kujenga ghorofa bila kuwa na injinia aliehakikiwa na serikali, vilevile serikali iwe inafanya ukaguzi kutaepusha madudu mengi mno! watu wamekaa ofisini wanakuza vitambi tu!.

pole kwa waathirika wote.
 
Back
Top Bottom