Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 21,956
- 23,466
Dalili si nzuri kabisa kwa upande wa huyu muungwana tena zimejidhihirisha wazi mapema kweli, ana kibaru kigumu na mtihani mzito sana kurlekea uchaguzi huo muhimu wa kanda ya Pwani. Kiufupi kimbe jamaa hakubaliki wala hatakiwi bana pwani.
Ili walau kukwepa fedheha atakayokumbana nayo ni afadhalli akajiengua mapema ili kulinda hadhi na heshima alioyojijengea kwa muda mrefu ndani ya chadema na jamii nzima kwa ujumla.
Licha ya kuwa tayari ameshawekeza vya kutosha kwa wajumbe, lakini wengi wao wameshakunja mlungula wa kutosha lakini hawamkubali wala kumuamini kutokana na aina ya siasa zake za harakati, majivuno, ubishi, ujuaji, kiburi na ubabe vitu ambavyo inaonekana kabisa kanda ya Pwani haitakua na amani endapo atashinda.
Lakini pia inafahamika bayana kwamba anakusudia kugombea pia nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa, kitu ambacho kimeongeza joto la yeye hata kudhibitiwa kimkakati na wenye maslahi zaidi na nafasi ya mwenyekiti taifa.
Lakini pia, makamu mwenyekiti ni mkaksi sana linapokuja suala la rushwa, huyu nae tayari amejitenga nae baada ya kutonywa kuhusu mlungula aliojipanga nao boniyai kuusambaza kwenye uchaguzi huo.
Wajumbe wa kanda ya Pwani wameahidi kumfurahisha, wamekataa kanda yao kununuliwa kwa pesa, na wamekubaliana kumaliza kiburi ya huyu muungwana hususani wale wenye backup ya chairman kwenye sanduku la kura.
Nae jeuri ya pesa imempumbaza ameshindwa kabisaa kusoma mazingira na alama za nyakati, na atafurahishwa kweli.
Mwenyewe ameapa kushinda uchaguzi huo, eti anadai amekichangia sana chama hicho na mpaka kufikia hatua ya kujiapiza na kusema kwamba lazima ashinde uchaguzi huo muhimu, vinginevyo hatasita kuchukua hatua binafsi mbadala mbona kuna vyama vingine vya kisiasa vingi tu humu nchini.
Unadhani sababu nyingine zitakazomkwamisha huyu muungwana na kushindwa vibaya uchaguzi huo muhimu sana wa kanda ya Pwani ni zipi?🐒
Mungu Ibariki Tanzania
- Kuelekea 2025 - Wafuasi Chadema wamsindikiza Meya Mstaafu Boniface Jacob kurudisha fomu ya uenyekiti
- Kuelekea 2025 - Boniface Jacob: Hata Nikishindwa Uchaguzi sitoenda CCM na kubwatuka bwatuka kama Mbwa