wakuu
Ni dhahiri kwa sasa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam anapitia wakati mgumu na wa kihistoria kwake kisiasa na kijamii
kijamii kwa sasa Makonda amepoteza marafiki wengi aliowazoea hapo awali kabla ya kufanya mambo yake bila ya yeye kujua nini matokeo yake
kwa sasa rafiki yake mkuu amebaki ni Magufuli tu, bila shaka hafurahii urafiki huu kwani magufuli sio rika lake
kisiasa na kiutawala, huku ndiko anapitia magumu zaidi kwani amepoteza uaminifu, umakini na kujiamini mbele ya watu anaowasimamia na kuwaongoza
licha ya Magufuli kumpa jeuri, lakini bado hali ni tete kwake kwani anapokuwa kazini kwake huwa yupo mwenyewe pekeyake bila ya kuwa na rais
Kisaikolojia ndio kaathirika zaidi kutokana na mambo aliyoyapitia ikiwemo ubashite, uvamizi wa clouds na kutengwa na wanahabari!
hili la kutengwa na wanahabari kinamuumiza mkuu huyu kwani hapo awali alizoea kuuza sura na kutafuta kiki kwenye vyombo vya habari hata kama hana jambo la msingi yeye alikuwa anahitaji kusikika na kuonekana tu
ukweli waliokushauri kung'ang'ania ofisi walikushauri vibaya, bora ungejiuzulu kwani unayoyapitia sasa yataendelea kukutafuna tu na hutafanya lolote kiutawala na kimaendeleo kwa ujumla