Bra-joe
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,615
- 1,111
Habari Ndugu zanguni,
Nadhani wote tumemsikia Tundu Lisu akitoa hoja zake kuhusu chaguzi zetu. Tukiacha ushabiki pembeni na kuwa Wazalendo, tutaona kwamba hoja zake ni za Kitaifa, haziegemei upande wowote wa kisiasa au kidini. Lengo lake ni kutoa mwongozo wa nini tunapaswa kufanya kama Taifa ili tuendelee kuwa na amani na kupata maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote.
Mambo matatu ambayo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapaswa kufanya ni:

- Wakuu wote wa ulinzi na usalama wa Kitaifa wakutane na Rais na kumshauri akubali kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayorekebisha mapungufu ya chaguzi zetu.
- Wakae pembeni na kuwaacha wanasiasa wabishane kwa hoja majukwaani bila upendeleo kwa upande wowote. Endapo upande mmoja utaamua kufanya maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kurekebisha vifungu vya Katiba ili chaguzi zetu ziwe huru na haki, basi vyombo vya ulinzi na usalama visiingilie maandamano hayo, bali vitoe ulinzi tu.
- Vyombo vya ulinzi na usalama viungane na Tundu Lisu kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoruhusu chaguzi zetu kuwa huru na haki ili kuepusha machafuko.