Kwa akili ndogo na nyepesi, CCM haiponi! Nape na Mwigulu jibuni haya...

Status
Not open for further replies.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
CCM kwa kutumia akili zao ndogo,wamekuwa wakiibua mambo ambayo kimsingi hayana msaada wowote kwao zaidi ya kuwaangamiza na kuvipa umaarufu zaidi vyama vya upinzani husisani CHADEMA.
Hii ni kutokana na mambo haya.
1.ukabila
Hapa walitumia neno ukabila kama turufu ya kuua chadema,lakini badala yake imezidi kupata umaarufu Tanzania nzima. Walidai CHADEMA ni chama cha kichaga,lakini mbinu zao hii chafu imeshindwa.
2.Udini
Suala la udini lilishika kasi sana uchaguzi wa 2010,ambapo walidai CHADEMA ni chama cha kidini(kikristo),kauli hii ilikuwa na nia ya kuwagawa watz kwa misingi ya dini zao. Sasa najiuliza,kama CHADEMA ni chama cha kikristo,wakristo walioko ccm wanafanya nini? Na ccm ni ya dini gani? Na hao wasio na dini(wapagani) ni wanachama wa chama kipi?
Kauli hii ya kipuuzi ilikuwa na nia ya kuwagawa watz,lakin kwa kuwa watanzania wanajua kuargue na wako rational waliona hizi ni propaganda za CCM kuishiwa sera na uwezo wa kuongoza nchi.Na katika hili CCM hawajafanikiwa!!
3.Ugaidi
suala hili limeshika kasi sana baada ya la udini na ukabila kushindwa,katika hili tunashuhudia Mwigulu akitamba mtaani kuwa ana ushahidi ambao anaweza kutoa duniani na mbinguni. Hapa tunaona CHADEMA wanaibuka kidedea baada ya Lwakatare kufutia makosa ya ugaidi.CCM chali!! Ushahidi wa mbinguni na duniani chali!! Hii ni credit kwa CHADEMA,na wananchi wamejua nani ni mkweli na muongo.Naamini hili walidhani ni pigo kwa CHADEMA, CHADEMA iko makini kuliko TISS,cc na serikali yenyewe.
Pia katika mwendelezo wa propaganda za ugaidi,hapa tunashuhudia mlipuko wa bomu katika mkutano wa CHADEMA na kusababisha watu 3 kupoteza maisha na wengine zaid ya 60 kujeruhiwa vibaya.katikz hili, CCM wamekuja kichwa wakiishtumu chadema kuwa ndio waliohusika huku wakijua hawana ushahidi.Tunashuhudia kauli za serikali zinazokinzana juu ya suala hili,lakini hakuna mwenye ushahidi.
CCM mmeishiwa sera,bali mnafanya siasa za kitoto,chafu na za kishamba. Kama hamjui kauli zenu za kipuuzi za kila mtu anatoa kauli yake kadri upuuzi wake unavyomtuma hii ni credit kwa CHADEMA kukubalika.Siku zinasonga,ccm inashuka umaarufu, CHADEMA inapanda,mwisho wa siku 2014/2015 hii hapa.
Kuna watu sura zao sijui watazificha wapi siku CCM imeshindwa akiwemo Nape,Mwigulu,wassira,Ritz,Pinda,Lukuvi,Nkamia,Serukamba,Ndugayi,Makinda nk.
Maoni yqngu
 
maccm wanatafuta mbeleko ya kujibeba.
bado kitambo kidogo mwigulu na nape watalaumiwa hadharani kwa kuwaingoza mkenge wana-maccm wenzao.
 
Nasema CCM haitaponi.Haitavuka kamwe. Haiwezi kuvuka mitihani yote hii halafu ikabaki salama, haiwezekani. Hawataimaliza mitihani yote hii halafu wakabaki salama. Haiwezekani.

Mitihani yenyewe ni hii;

1.migogoro ya wakulima na wafugaji. Kila siku wanauana na serikali ya CM ipo.

2.Migomo ya madereva. Ni kovu ambalo haliwezi kufutika kirahisi kuelekea uchaguzi mkuu.

3.Ufisadi na rushwa, escrow,EPA,meremeta nk

4. Umaskini kwa watz. Hii inatokana na ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

5.UKAWA. Umoja huu ni mwiba kwa serikali ya kijani.

6.Uchakachuaji wa maoni ya wananchi kwenye rasmu ya Warioba. Hapa walionesha dharau kwa watz.

7.Ahadi hewa ya mahakama ya kadhi kwa waislamu. Mwaka huu ni ndoto kupata kura zao kwa uongo na ahadi za uongo.

8.Mgogoro wa Gwajima na Pengo.

Serikali ya ccm imeingia mkenge kwa kugeuza mgogoro huu kuwa wa kisiasa,kitu ambacho unajenga chuki kwa waumini wa Gwajima na wakristo wengine dhidi ya ccm.

9. Upendeleo wa polisi katika mikutano ya kisiasa.moja ya watu wanaochukiwa sana na jamii ya kitz ni polisi wanaoibeba ccm huku wakikandamiza upinzani.

10.Ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Hili ni chukizo kwa wanafunzi na wazazi wa wanafunzi hawa kwa sababu wazazi wao ni walipa kodi wa nchi hii.

11. Elimu ya uraia na mitandao ya kijamii. Elimu ya uraia imebadilisha mtazamo na fikra za watz juu ya ccm na upinzani. Walisema vyama vya upinzani vinaleta vita. Vita ipi? Mbona haijawahi kutokea vita?

12. Madai ya walimu. Katika watu wanaoiona ccm ni adui wao mkubwa ni walimu. Hawaitaki ccm na vibaraka wao.
Ccm kazi mnayo,hamtavuka salama.

Ni ngumu kwa hawa ndg zangu wa kijani kuvuka kwa sababu,ni ngumu wao kukabili mitihani yote hii bila kuzua tatizo lingine.
 
wajinga ni wengi mno na ww ni mojawapo ni serikali ipi unafikiri inaweza labda ya malaika na hiyo haiwezekani mwaka huu iwe iwavyo ccm hiyo madarakani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom