Kuzuia kutekwa na kuuawa wanaoonekana kuwa na mawazo mbadala au kupinga Serikali kwanini tusikubaliane kurudi kuwa nchi ya chama kimoja cha siasa!?

Mwangi T.

Member
May 30, 2014
93
46
Ni dhahiri kabisa kuwa nchi yetu na hasa viongozi wa serikali hawapo tayari na huu mfumo tunaoutumia sasa wa siasa za kidemokrasia!

Wakati mfumo unataka kuingizwa nchini miaka ya mwanzoni mwa tisini inasemekana yalikusanywa maoni kwa wananchi na wananchi waliukataa, inawezekana walikuwa sahihi au ni kwa vile tu hawakupewa elimu juu ya mfumo huu utakavyokuwa ili waamue kwa usahihi.

Mfumo ulipitiswa japo maoni ya wananchi wengi hawakuukubali.
Miaka imeenda mbele na tuko zaidi ya miaka 30 na huu mfumo lakini bado inaonekana haujakubalika nchini na hasa kwa upande wa viongozi wa serikali na chama kinachotawala yaani Ccm.

Chaguzi zote zilizofanyika kwa njia hii tunayoiita ya kidemokrasia zimeminya mno haki ya wananchi kuchagua kihalali.

Serikali inayotawala imeonekana kuchukizwa mara nyingi na watu wanaotoa maoni yao kinyume au kuikosoa japo hi haki ya kidemorasia.

Miaka hii tumeenda mbele zaidi kwa kuumiza, kuteka, kupoteza wale wanaoonekana kutoa maoni kinzani kwa serikali.

Imefikia sasa kijana au mtu kuwa chama cha upinzani ni kama uhaini wakati tuliamua wenyewe kuingia kwenye mfumo huu wa kidemokrasia.

Tunapoteza na kukatisha tamaa vijana wenye akili kubwa ambao wangeweza kusaidia Taifa letu kwa vile tu hawaamini katika CCCM!

Tukubaliane kwa pamoja kurudi kwenye mfumo tuliokuwa nao kwa kipindi kirefu wa chama kimoja!

Nawasilisha.

FB_IMG_1727781601058.jpg
 
Tatizo liko kwa ''mabeberu''. Tunataka fedha yao, tunataka matibabu yao, tunataka watoto wetu wasome shule zao. Tnataka watoto wetu wasafiri kwenda nchi zao. Tunataka watoto wetu waishi maisha ya ki-magharibi. Tukirudisha chama kimoja huoni haya yote tutayakosa? Huoni hata wachina na waarabu wanatamani maisha uhuru wa kuingia kwa mabeberu? NB: Haya siyo maneno yangu. Ni maneno ya mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom