Kuwekeza mabilioni ya umma kwenye bandari kisha kuwapa wageni kuendesha ni ile Nyerere alisema kupewa vipande vya chupa tukidhani dhahabu

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,838
7,722
Habari kutoka serikali kufuatana na taarifa za leo serikali kwa sasa inawekeza mabillioni ya shilingi kuimarisha bandari ya Mtwara. Shughuli zinazofanyika ni pamoja na kuongeza kina cha maji kuongeza idadi ya gati maeneo na majengo ya kuhifadhi mizigo pamoja na vifaa vya kushusha na kupakia mizigo. Mambo kama hayo yamefanyika kwa kiwango kikubwa bandari za Dar es Salaam na Tanga.

Jambo nalotaka kuzungumzia ni huu ujinga na ufisadi unaoendelea kufanyika. Wajanja kampuni za kigeni hasa za uarabuni na India kazi yao imekua kusubiri wekezaji za umma za nchi zetu kisha kuja kujidai watawekeza na vigogo wapenda rushwa wanawapa kandarasi kuendesha bandari zetu eti ni wawekezaji. Eti watawekeza kuleta vifaa na utaalam kuendesha bandari. Yaani kama nchi tutumie mabilioni kutengeneza bandari kisha tushindwe kuweka vifaa.

Hizo kampuni wala wakipewa hizo kandarasi hawawekizi kitu ila kuanza kuvuna wao mapato huku wakigawa rushwa kwa vigogo na serikali wala haipati chochote cha maana. Mfano ni kampuni ya TICTS ambayo wala haikua ya wageni ila watanzania wajanja walitumia uongo kujidai ni kampuni ya Hong Kong na wakaikamua nchi kwa karibu miaka 30 kujipatia utajiri mkubwa juu ya uwekezaji wa umma bila wao kujenga hata jengo moja bandarini.

Watanzania wanasoma mambo ya fedha na utawala zaidi kuliko ufundi na uhandisi. Ni ajabu kwa nini shirika letu la bandari lisiweze kuendesha bandari zetu kwa ufanisi. Vigogo wa serikali wakisha idhinisha uwekezaji mkubwa wnakula njama na wajanja waje kuenddesha uwekezaji hizo kama bandari ambapo ukweli wanahongwa.

Iweje chini ya kiongozi aina ya magufuli aliweza kuwabana vigogo bandari ya Dar muda wa kungoja meli bandarini ukapungua kutoka zaidi ya mwezi mmoja hadi kufikia wiki moja? Au tujiulize kwa nini meli Mombasa zinatumia siku chache tu kwenye bandari wakati bandari inaendeshwa na shirika la bandari la Kenya Kenya Port Authority?

Sasa serikali wametuambia wao wenyewe wanaboresha bandari kwa mabilioni ya hela za umma. Subirini mtasikia wanapewa wageni kuendesha eti watawekeza. Binafsi sijasikia au kuona DPW wanawekeza nini bandari ya Dar badala yake ni kazi ya kuvuna ambapo hawakupanda kitu.

Tuamke watanzania haya mambo Nyerere alituelimisha zamani yanaendelea. Wageni na kwa siku hizi Wahindi na Warabu wanachukua mali zetu za thamani kwa vipande vya chupa tukidhani ni dhahabu.
 
Back
Top Bottom