adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 11,721
- 25,516
Moja kwa moja..
Ukichunguza kwa makini vitu vikubwa vinavyongaliwa majumbani kwenye Tv ni tamthlia , movies na miziki na ndani ya hivyo vitu miongoni maudhui makubwa ni;
1. MAPENZI : humo utakuta kumejaa kutongoza , romantic scenes na mambo mengine ambayo hayafai watoto kuyaona wala kuyasikia. Mfano asilimia 90% ya movies za kizungu lazima utakuta kipande cha kufanya tendo kimewekwa (Mizagamuo Live)
2. UKATILI NA MAUAJI : mauaji ya kinyama , na utaumiaji hovyo wa silaha na mengineyo
3. UHUNI na UHALIFU : Mbinu mbalimbali za uhalifu , jinsi majambazi wanavyoishi maisha mazuri , uvutaji wa bangi , ulevi ,ufuksa nk.
4.USHIRIKINA : Watu kurogana ,kwenda kwa waganga , visasi .
5. KUCHEPUKA , UMBEA , USHOGA Nk.
ATHARI ZAKE.
Mtu akishazoe kuona na kusikia mambo ya hovyo katika Tv na Miziki tena wakati mwingine yakiwekwa katika taswira nzuri hapo moja kwa moja akili ya mtu inaathirika na kuona ni mambo ya kawaida sana hata likiwa jambo la hatari tena kubwa , na akili ya mwanadamu mara nyingi anapenda kujaribu katika vile amezoe kuona au kusikia mara kwa mara hatimaye mtu anajaribu na kujiingiza katika mambo yasiyofaa.
Na Mzazi asipochunga anakuta anazalisha sumu katika akili ya mtoto ambayo itakuwa inamtafuna taratibu kiasi ambacho kuathiri tabia zake tokea utotoni ,ukubwani hata mfumo wake mzima wa Maisha kwa ujumla.
MAONI NA USHAURI.
Hatukatai kwamba mtu huwezi kuchunga kila kitu sasa ni Dunia ya utandawazi lakini hata kama hauwezi kuchunga yote ni lazima mtu ujitahidi kufanya na kuzuia lile ambalo una uwezo nalo ili uweze kukomesha au kuounguza madhara ya kitu , mtoto anapoona jambo fulani kwao linapendwa kwao ,hakanywi linachukuliwa kawaida na mara nyingine Mzazi anasapoti basi yeye atachukulia kawaida katika maisha yake yote pengine ikawa ngumu kuacha.
Lakini ikiwa jambo Fulani kwao ni mwiko kwao na anaonywa mara kwa mara ni rahisi sana kuacha hata kwa baadae kwa sababu katika akili yake tokea awali anajua hili jambo baya Wazazi wangu hawalipendi na kulikuwa hakuna uhuru wa kulifanya nyumbani.
Kwa trend ya nyimbo za matusi, mavazi ya hovyo , uhuni pamoja na maudhui mengi yasiofaa katika TV ni kheri mtu kwako usiweke kabisa Tv wala kuruhusu nyumba yako iwe sehemu ya kusikiliza matusi na ujinga mwingine ili kuepuka wewe kuwa chanzo Cha kuharibikiwa kwa watoto na Familia yako kwa ujumla.