Kuwa makini na vitu hivi katika malezi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665


WAZAZI ni nguzo kubwa katika malezi ya mtoto, matokeo ya tabia za mtoto yanatokana na malezi mazuri aliyopewa na mzazi.

Malezi anayoyapata mtoto kuanzia umri wa siku moja mpaka miaka 13 ndiyo yanayochangia kumtengeneza mtoto.

Kama mzazi kuna vitu vya msingi unapaswa kuwa mwangalifu lakini kati ya hivyo vipo vinne vya muhimu zaidi.

Kitu cha kwanza kuwa makini sana na adhabu unazompa mtoto, hatua za kinidhamu unazochukua dhidi ya mtoto wako zinaweza kumjenga ama kuathiri malezi yake.

Si lazima kila kosa umwadhibu unaweza kufanya malezi shirikishi pia, kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutoa lugha chafu kwa watu, utoro shuleni, ugomvi n.k toa sababu za kufanya hivyo.

Ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwanini haifai kufanya jambo fulani, ili kumpatia nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo.
Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali.

Hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kumsababishia hofu ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu hata wenzao pia.

Hata hivyo, pia haitakiwi kuwa mpole mno kwa sababu watoto wanaweza kuendelea kuwa wakosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wao katika jamii na shuleni.

Mazingira ambayo yanajumuisha hali ya hewa, watu wanaokuzunguka, vitu vilivyopo pia yanaweza kuchangia kuathiri malezi ya mtoto.

Mazingira humfanya mtoto kuwa tofauti, mfano anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. lazima watakuwa tofauti.

Wazazi tuna wajibu wa kuwawekea mazingira mazuri watoto ili waweze kukua katika maadili mema.

Jambo jingine ni mawasiliano, wazazi mnapaswa kuwashirikisha watoto katika mawasiliano na baadhi ya maamuzi ya kifamilia endapo atahitajika.

Hiyo itamfanya kuwa na uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake.

Pia katika maongezi, nina maana mtoto akisema jambo lolote ni muhimu kumsikiliza na si vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele.

Tabia hiyo itamsaidia kwa kumpatia uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.

Mfumo wa malezi pia unaweza kumjenga mtoto wako au kumharibu.

Weka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo kuwajengea hali ya kujisikia kuthaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo kuwaongezea furaha na amani.

Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya imani ya kupendwa imejengwa kwenye akili zao.


Chanzo: Mtanzania
 
Nilikwenda kumsalimia rafiki yangu mmoja.... Mwanae wa kiume ana miaka minne. Yule mtoto akamwambia mama yake.... " Mama nakupenda sana" .... Mtoto ana-smile anamfurahia mama yake... Nikasema wow wow.... Awesome.

I liked it... Admired it.... Loved it.
 
Maneno adhimu kabisa haya, asante sana.

Yupo mtoto wa kiume umri miaka minne, baada ya kumaliza kutizama sinema ya mfalme, akawaambia wazazi wake kuwa na yeye anataka aoe wanawake watatu.

Mama yake akamuuliza, ni yupi utakae lala nae ili ukitaka kudondoka kitandani akuzuie?
Mtoto akajibu, nitaendelea kulala na wewe mama, kwakuwa nakupenda sana.
Mama akabubujikwa na machozi ya furaha, huku akimkumbatia mwanae.

Mtoto akaendelea, hao wake wote watatu nitampa baba alale nao chumba kile cha nje.

Baba akabubujikwa na machozi ya furaha huku akitaka kumkumbatia mtoto wao bila mafanikio kwani mama bado alikuwa amemkumbatia huku akimtizama baba kwa jicho kali sana.

Tuwapende watoto jamani, hawana double standard.
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
 
Haya ndo mambo ya kuyaweka hapa tuweze kujifunza, sio kila post msambwanda... Hongera sana mleta Mada.... Agiza Jack Daniel nakuja kulipia.
 
Ahhahahahahahahhaha
Mkuu umenifanya nicheke aiseee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…