Kuvunjwa kwa Baraza Mawiri Kenya. Hii itasaidia kitu gani?

Kalamu

Platinum Member
Nov 26, 2006
11,570
14,515
Bwana Ruto katikiswa kwelikweli na hawa vijana waliotishia kumwangusha kijumla.

Licha ya kufuta bajeti na kuahidi kushughulikia mengine yaliyotajwa na hawa vijana, hali bado inaonyesha kuwa tete.

Hizi juhudi anazofanya sasa, ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi mawaziri wake wote, kasoro mmoja tu, zinaonekana kuwa mbinu za kuwaingiza wapinzani serikalini, akiwa na matumaini ya kupunguza hasira za kundi hili la Gen Z.

Wapinzani nao wamekwisha stuka, haieleweki kama bado watakuwa tayari kuungana na Ruto kuunda serikali mpya.

Tuwatakie mema majirani zetu, wakati tukipata funzo muhimu, kwamba viongozi wapo siyo kutuendesha sisi raia, bali kututumikia. Ruto angeamua kuwa 'Chura Kiziwi' wakati huu angekwisha kuwa historia.

PIA SOMA
- News Alert: - William Ruto avunja Baraza la Mawaziri Kenya
 
ni katika kuimarisha utendaji wa serikali na kuongeza ufanisi katika kazi za maendeleo ya wanainchi,

Rais na mkuu wa nchi,
wakati wowote kadiri atakavyoona inafaa, kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kama ambavyo mh.William Ruto mwenyewe alivinukuu, anaweza kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya au kubadilisha baadhi mawaziri na kusonga mbele 🐒

so,
hakuna suala la kujifunza kwenye mambo ambayo yako bayana kwenye sheria na katiba. Ruto ana mamlaka na amefanya aliyoyafanya kama ambavyo katiba inaelekeza afanye akiona inafaa 🐒

unasahauje usichokumbuka? 🐒
 
Sijui Kuria na Murkomen watafanya kazi gani.
baada ya muda lazima wataula tena kwenye mashirika ya umma, sio rahisi kuwaacha washirika muhimu kama hao mathalani Onesimus Kipchumba Murkomen, alijiuzulu useneta ili amsaidie Raisi serikalini 🐒

Lakini pia hata huyo Moses Kuria ni miongoni mwa watu muhimu sana kumdhibiti naibu wa Rais RigGy anaeleta matata hasa kule mount kenya, na kwahivyo hawezi kuachwa bila ajira kwa muda mrefu...

na by the way wanaweza kurejea tena barazani au kua washauri wa Rais kisiasa au kiuchumi 🐒
 
Bwana Ruto katikiswa kwelikweli na hawa vijana waliotishia kumwangusha kijumla.
Licha ya kufuta bajeti na kuahidi kushughulikia mengine yaliyotajwa na hawa vijana, hali bado inaonyesha kuwa tete.

Hizi juhudi anazofanya sasa, ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi mawaziri wake wote, kasoro mmoja tu, zinaonekana kuwa mbinu za kuwaingiza wapinzani serikalini, akiwa na matumaini ya kupunguza hasira za kundi hili la Gen Z.
Wapinzani nao wamekwisha stuka, haieleweki kama bado watakuwa tayari kuungana na Ruto kuunda serikali mpya.

Tuwatakie mema majirani zetu, wakati tukipata funzo muhimu, kwamba viongozi wapo siyo kutuendesha sisi raia, bali kututumikia. Ruto angeamua kuwa 'Chura Kiziwi' wakati huu angekwisha kuwa historia.
Ruto must go!
Anguka nayo!
 
ni katika kuimarisha utendaji wa serikali na kuongeza ufanisi katika kazi za maendeleo ya wanainchi,

Rais na mkuu wa nchi,
wakati wowote kadiri atakavyoona inafaa, kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kama ambavyo mh.William Ruto mwenyewe alivinukuu, anaweza kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya au kubadilisha baadhi mawaziri na kusonga mbele 🐒
Rais na mkuu wa nchi,
wakati wowote kadiri atakavyoona inafaa, kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kama ambavyo mh.William Ruto mwenyewe alivinukuu, anaweza kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya au kubadilisha baadhi mawaziri na kusonga mbele
🐒
Unajibu kama mlevi fulani hivi, tena aliyekuwa usingizini na ghafla anazinduka, huku akidhani alikuwa akiota ndoto mbaya.
Usilalamike kuwa nakuonea. Angalia wewe mwenyewe haya uliyo andika hapa chini.
Rais na mkuu wa nchi,
wakati wowote kadiri atakavyoona inafaa, kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kama ambavyo mh.William Ruto mwenyewe alivinukuu, anaweza kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya au kubadilisha baadhi mawaziri na kusonga mbele
 
Ruto must go!
Anguka nayo!
Wakikomalia hilo sijui atafanyaje. Itabidi tu aondoke.

Ilivyo sasa mbinu za kutumia mabavu na kuua, hiyo tayari imekwisha ondolewa mezani. Atauaje watu ambao Katiba inawaruhusu kufanya maandamano! Wajitahidi tu kuwabana mamluki wanaoingiza vurugu kwenye shughuli zao.

Ruto mwenyewe bado ile kumbukumbu ya ICC inamfanya asirudie tena hayo mambo yaliyo mfikisha huko.

Huyu anayo shida kubwa mikononi mwake.
 
Unajibu kama mlevi fulani hivi, tena aliyekuwa usingizini na ghafla anazinduka, huku akidhani alikuwa akiota ndoto mbaya.
ukweli una tabia mbaya sana dah 🤣

ni mchungu halafu haupendwi kabisa kuskika wala kuonekana wala kuelezwa...
pole nyingi sana kwa wanaoumizwa na ukweli, itabidi mzoee tu...

kuvunja baraza la mawaziri au kuteua mawaziri wapya ni jambo la kikatiba Rais anaweza kulifanya wakati wowote anaoona unafaa, na Sheria iliwekwa ikijua kwamba kuna nyakati Mkuu wa nchi anaweza kuwiwa kufanya hivyo 🐒
 
Kwani "Gen Z" shida yao ni serikali ya mseto!!??
Gen Z hawana affiliation na Azimio la Umoja wala nini, na wao hawana kiongozi.

Shida yao ni Ruto kuachia ngazi.
Wako kwenye mtego,Ruto sio mjinga,anajua namna ya kumlisha samaki chambo harafu akamtoa taratibu.Nadhani President Ruto kagundua au kapewa shindikizo na wababe wa dunia rafiki wa Kenya njia rahisi na salama namna ya ku handle young turks aka Gen Z.
Unageuka 180 degrees kila kitu,tena very fast, its so strange.
Lakini kama ni roho yake ndio ilimsukuma basi Raisi kaanza kutekeleza hustler,mama mboga serikali ya wanyonge aliyohaidi.
 
baada ya muda lazima wataula tena kwenye mashirika ya umma, sio rahisi kuwaacha washirika muhimu kama hao mathalani Onesimus Kipchumba Murkomen, alijiuzulu useneta ili amsaidie Raisi serikalini 🐒

Lakini pia hata huyo Moses Kuria ni miongoni mwa watu muhimu sana kumdhibiti naibu wa Rais RigGy anaeleta matata hasa kule mount kenya, na kwahivyo hawezi kuachwa bila ajira kwa muda mrefu...

na by the way wanaweza kurejea tena barazani au kua washauri wa Rais kisiasa au kiuchumi 🐒
Washauri wamepunguzwa wewe unawaongeza Kuria na Murkomen kupitia keyboard?
 
Washauri wamepunguzwa wewe unawaongeza Kuria na Murkomen?
suala ni kuimarisha utendaji wa serikali na kuvhochea ufanisi katika kuwaletea wananchi maendeleo, kupunguza ni jambo lingine....

nakuhakikishia ,
kuria, Murkomen, duale, Devis chirchir, kindiki, ababu namwamba, Alfred Mutua, Justin muturi n.k hawawezi kuachwa bila ajira 🐒

na kithuri Kindiki anaenda kua mwanasheria Mkuu wa serikali, Justin Muturi au Kipchumba Murkomen moja wao anaweza kua waziri wa masula ya katiba na Sheria 🐒
 
Wakikomalia hilo sijui atafanyaje. Itabidi tu aondoke.

Ilivyo sasa mbinu za kutumia mabavu na kuua, hiyo tayari imekwisha ondolewa mezani. Atauaje watu ambao Katiba inawaruhusu kufanya maandamano! Wajitahidi tu kuwabana mamluki wanaoingiza vurugu kwenye shughuli zao.

Ruto mwenyewe bado ile kumbukumbu ya ICC inamfanya asirudie tena hayo mambo yaliyo mfikisha huko.

Huyu anayo shida kubwa mikononi mwake.
Miili zaidi inazidi kuokotwa jijini Nairobi. Wakuu wa idara za serikali wanazidi kuanguka!
Kifupi ni kwamba Ruto Must Go!
 
ukweli una tabia mbaya sana dah 🤣

ni mchungu halafu haupendwi kabisa kuskika wala kuonekana wala kuelezwa...
pole nyingi sana kwa wanaoumizwa na ukweli, itabidi mzoee tu...

kuvunja baraza la mawaziri au kuteua mawaziri wapya ni jambo la kikatiba Rais anaweza kulifanya wakati wowote anaoona unafaa, na Sheria iliwekwa ikijua kwamba kuna nyakati Mkuu wa nchi anaweza kuwiwa kufanya hivyo 🐒
Unazungusha zungusha maneno, halafu unataka nipoteze muda wangu kusoma na kujibu takataka?
 
Miili zaidi inazidi kuokotwa jijini Nairobi. Wakuu wa idara za serikali wanazidi kuanguka!
Kifupi ni kwamba Ruto Must Go!
miili mingap gentleman imeokotwa?

akati 2007-2008 miili ilikua inakusanywa mtaani na buludaza kama takataka na Rais hakwenda popote 🐒

na by the way,
kwa uharibifu ule wa maandamano ya ghasia ya bandits wale, wezi, majambazi na waporaji ulitegemea pasiwepo vifo kweli?

kwamba wanyang'anyi wale ni malaika wasiumie na kupata majeraha mabaya yasiyoweza kusababisha vifo vyao, au kugongana vibaya wao kwa wao walipokua wanaiba na kupora vitu kwenye maduka ya watu, na kudondokewa na vitu mbalimbali kama vioo walivyokua wakiharibu wenyewe!🐒
 
Unao uhuru wa kujiandikia chochote... Lakini kumbuka 2008 siyo leo.
Na kesho itakuwa tofauti sana!
 
Back
Top Bottom