- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Madai:
Yapo madai kutoka katika jamii mbalimbali yakihusisha rangi nyekundu na radi. Baadhi ya jamii zinaamini kwamba kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua ni hatari kwa sababu yanaweza kusababisha ukapigwa na radi. Sambamba na hilo jamii nyingine zinaamini Mjusi kafiri na Kondoo wana uwezo wa kupambana na radi.
---
- Tunachokijua
- Radi ni mwangaza na miale ya mwanga mithili ya shoti za umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga katikati ya mawingu unaweza kuitwa "umeme".
Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hiyo ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani unaoonekana kama mwangaza mkali.
Mkondo unatoa pia joto kali na joto hilo husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huo unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali, lakini inaweza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu.
Ni kweli kwamba kumekuwa na imani mbalimbali kwa jamii nyingi za Kiafrika Tanzania na Rwanda ikiwamo zinaitazama radi kijadi zaidi. Wapo wanaamini ni hatari kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua kwa sababu mavazi hayo yanavutia radi kukufata. Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho kamili unaobainisha chanzo cha jamii hizo kuamini hivyo. Kamazima Lwiza, Profesa wa fizikia ya anga New York Marekani akieleza hadithi za uongo na kweli, saba kati ya hizo anataja nguo nyekundu kuwa kuvutia radi kuwa ni hadithi ya uongo.
Zipo Imani nyingine kadhaa za kijamii kuhusu radi ambapo pia baadhi ya jamii za Afrika ya sasa na Ugiriki zamani zinaamini radi zinatengenezwa na watu au miungu inatumika kama silaha ya kijadi kuwashambulia wengine au kutoa adhabu.
Hoja zote hizi ni sehemu ya hoja nyingine nyingi za kijamii kuhusu radi. Lakini hazithibitiki kisayansi
Je, sayansi inasema nini kuhusu uhusiano wa nguo nyekundu na radi?
Wataalamu wa hali ya hewa wanaeleza kuwa kwa tafiti zilizopo mpaka sasa ulimwenguni hakuna uhusiano wowote kati ya radi na rangi yoyote Ile. Mathalani, Wilbert Kikwasi wa TMA anaeleza kuwa radi inatokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi. Anaongeza kuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi unaobainisha namna rangi nyekundu inavyoweza kuchochea au kuvutia radi.
Zaidi ya hayo, Wataalamu wa masuala ya hali ya hewa wanafafanua kuwa Radi hutokana na kuachiliwa kwa umeme tuli, tukio ambalo hutokea kutokana na tofauti ya nguvu za umeme kati ya mawingu na ardhi. Radi ni Umeme ambao husafiri kutoka juu hadi chini na kwa kawaida hugonga vitu virefu zaidi.
Mazingira ya kupigwa na radi yanategemea zaidi kama umekaa kwenye vitu virefu kama miti, milima, kwenye minara shamba au kwenye mimea mifupi ambayo umeizidi Kimo. Mara unapoona dalili za radi Inashauriwa kutotumia mwamvuli kujikinga na mvua zinazoambatana na radi kwani mwavuli utakufanya kuwa kitu kirefu kupita vingine kufanya wewe pamoja na mwavuli wako kuwa njia rahisi ya radi kuingia ardhini.
Kukaa ndani ya nyumba zilizowekwa vifaa vya kuzuia Radi inaweza kuusaidia kujikinga na dhidi ya radi pia Kukaa ndani ya gari kunaweza kukuzuia kupigwa na radi, lakini unashauriwa kufunga vioo na kutokushika kitu chochote chenye asili ya chuma ukiwa ndani ya gari, hapo utakua salama.
Pia wakati wa mvua zinazoambatana na radi ni vema kuepuka kunawa mikono kwa maji, kufua nguo, wala kuogelea au kuoga. Ni muhimu kuzima vifaa vya umeme kama vile TV, Radio, computer huku ukichomoa nyaya zilizounganishwa kwenye chanzo cha umeme, epuka kuchomoa waya wakati radi inapiga. Usitumie Simu za mezani zilizounganishwa na waya kutoka kwenye nguzo wakati wa mvua za radi kwani kuna uwezekano mkubwa ukapigwa na radi.
Hakuna uhusiano wowote kati ya nguo za rangi nyekundu na kupigwa na radi, JamiiForums inasisitiza kuchukua hatua za kitaalamu za kujikinga na radi kama, kutokaa chini ya miti na majengo marefu wakati wa mvua.