Kuuzwa soko la Kurasini, viongozi warushiana mpira

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,642
8,699
Wakati viongozi wa soko la Kurasini, lililopo Mtaa wa Shimo la Udongo, barabara ya GSM jijini hapa, wakieleza wapo hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuuza soko hilo, uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umesema hautambui mauzo hayo.

Mbali ya halmashauri, uongozi wa mtaa na wafanyabiashara zaidi ya 160 waliopo sokoni hapo wamesema hawajashirikishwa hivyo hawajui ni kwa namna gani wataondolewa.

Soko_Kurasini.png

Mwenyekiti wa Mtaa wa Shimo la Udongo, Gerald Manjoli amesema alipata malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu mchakato wa kuuza soko hilo kwa mwekezaji, naye aliyafikisha kwa halmashauri.

Manjoli amesema: “Ni jambo la ajabu soko lipo mtaani kwangu linauzwa sina taarifa, hata viongozi wake hawataki ushirikiano na uongozi wa mtaa. Wanajiona wao ndio wamiliki wa soko hivyo wana uamuzi nalo, hii si sawa na inasikitisha.”

Akizungumza na Mwananchi, Katibu wa soko hilo, Bendickson Bazale amekiri kuwepo kwa mpango huo na kueleza kuwa wameshamaliza hatua zote, wanachosubiri hivi sasa ni kuingiziwa fedha kwenye akaunti ya soko ili wagawane.
 
Ila hao wafanyabiashara wa hapo wako local mno,serikali inapaswa kuliboresha hilo eneo
 
Back
Top Bottom