Kuuliza si ujinga, nini hasa maana ya neno SIASA?

briophyta plantae

Senior Member
Feb 18, 2017
114
129
Kwenye kukua kwangu, hili neno Siasa ni neno la kawaida maana nalisikia mara kwa mara. Mfano:

Chama cha siasa. Mwana siasa...

Ila ukweli sijui maana yake. Maana hata wakati mwingine ni neno la heshima, na wakati mwingine ni neno la kuvunja heshima.

Ukiongea uongo, unaitwa mwanasiasa. Ukitoa hoja isiyokubalika na jamii, unaambiwa unaleta siasa.

Utasikia, "Hii nchi maendeleo yapo nyuma kwasababu serikali haifanyi kazi yake ipasavyo, wanaleta siasa tu kwenye mambo ya msingi."

Nisaidieni nijue SIASA ni nini hasa.

FB_IMG_1727638523954.jpg
 
Kwenye kukua kwangu, hili neno Siasa ni neno la kawaida maana nalisikia mara kwa mara. Mfano:

Chama cha siasa...
Mwana siasa...

Ila ukweli sijui maana yake. Maana hata wakati mwingine ni neno la heshima, na wakati mwingine ni neno la kuvunja heshima.

Ukiongea uongo, unaitwa mwanasiasa.
Ukitoa hoja isiyokubalika na jamii, unaambiwa unaleta siasa.

Utasikia, "Hii nchi maendeleo yapo nyuma kwasababu serikali haifanyi kazi yake ipasavyo, wanaleta siasa tu kwenye mambo ya msingi."

Nisaidieni nijue SIASA ni nini hasa.

siasa ni uongo uliokomaa,na mwanasiasa ni mwongo kuliko mwongo yoyote yule,,,yaani mwana siasa anaweza akapiga fix taifa zima na wa2 wakamshangilia!!!
 
Siasa ni mchakato wa kutafuta na kutekeleza maamuzi katika jamii, kupitia serikali au vyama vya kisiasa. Shughuli za kisiasa ni kama mijadala, upigaji kura, na utekelezaji wa sera za uma. Lengo la siasa ni kuunda mazingira ya utawala na maamuzi yanayolenga kuboresha hali ya jamii kwa ujumla. Ingawa siasa inaweza kuwa na athari chanya, pia inaweza kuleta mivutano na tofauti kati ya watu au makundi katika jamii.
 
Sasa watu wanafanya siasa kwa namna sahihi kulingana na maana yake,ni watu wachache kiasi gani wenye uelewa wa hili jambo siasa,kuna njia nyingine ya kufanya maamuzi kwenye taifa ukitoa siasa?
 
Sasa Ingia Angalia na Sema Angalia hai.
Kwa ufupi Siasa udumu kwa walio na kweli, otherwise ni majuto kwa wasio wakweli.
 
Inakuwaje sasa tunawapa dhamana watu tunaojua ni waongo na hawatatufikisha popote
swali zuri!!!!!,,,ni kama unavomtongoza mwanamke,unampiga fix na anjua kabisa unampiga fix,sometimes anajijua kabisa kwamba yeye ni mke wa m2,laki unampiga fix mpaka anakupa firigisi yake!! yah111 wanasiasa wengi ni SANGWIN!!!!!!!!samgwini ni jamii ya wa2 waliobarikiwa kuongea sana!!
 
Siasa ni porojo za kugeuza uongo uonekane kama ukweli na si vinginevyo
 
Sasa watu wanafanya siasa kwa namna sahihi kulingana na maana yake,ni watu wachache kiasi gani wenye uelewa wa hili jambo siasa,kuna njia nyingine ya kufanya maamuzi kwenye taifa ukitoa siasa?
Ili uweze kufanya maamuzi ya kitaifa lazima uwe kwenye nafasi yoyote kisiasa,kama sivyo kuna tetesi na sijui kama zina hakika, kuna wafanya biashara na watu maarufu wanaosemekana kuwa na maamuzi ya nani ashike nafasi ipi katika taifa kwa manufaa yao na kitaifa,sio nafasi zote ila ya uraisi ikiwemo
Siasa ni kila kitu na inaamua maisha yako ya sasa na baadae
 
Siasa ni mfumo au mchakato wa kufanya maamuzi ndani ya jamii, nchi, au shirika.

Kwa kawaida, inahusisha namna mamlaka, nguvu, na rasilimali zinavyogawanywa na kudhibitiwa.

Siasa pia inaweza kumaanisha shughuli za viongozi wa kisiasa, vyama vya siasa, na mikakati wanayotumia kushawishi au kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Siasa ni njia ambayo watu hutumia kuunda sera na sheria zinazolenga maslahi ya umma au ya kibinafsi.
 
Back
Top Bottom