Kuuawa kwa Juma Mfaume kwa kushindwa kulipa deni la mkewe kwa kampuni ya OYA, kunatokana na urasimu na sera mbovu za BoT

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,843
31,046
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Pwani, siku ya Jumanne, tarehe 8 mwezi huu, kuwa wafanyakazi 4 wa kampuni ya OYA, walimuua Juma Said Mfaume, wakidai kuwa mkewe huyo Juma Mfaume, anayeitwa Khadija Ramadhan, alikopa pesa toka Kwenye kampuni hiyo ya OYA na akawa harejeshi marejesho Kwa kadri ya makubaliano yao.

Hiki kisa kinasikitisha sana.

Mosi: Huyo aliyeuawa Juma Mfaume, Wala hakuwa mdeni wao hao kampuni ya OYA, mdeni wao ni Khadija Ramadhan.

Pili: Huyo Marehemu Juma Mfaume, aliwaeleza hao wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, kuwa huyo mdeni wao, Khadija Ramadan hakuwepo hapo nyumbani muda huo.

Tatu: Huyo Marehemu Juma Mfaume, ambaye ni mume wa Khadija Ramadhan, aliwaeleza hao wafanyakazi wa OYA kuwa, huyo mkewe Khadija Ramadan, hakumjulisha kuwa amekopa hizo pesa katika kampuni ya OYA, Kwa hiyo hiyo taarifa ndiyo kwanza anaipata Kwa hao wafanyakazi wa OYA.

Swali kubwa ninalojiuliza, ni Kwa nini hao wafanyakazi hawakufanya subira ya kumsubiri huyo mdeni wao, Khadija Ramadan, badala yake wakataka kuingia Kwa nguvu, nyumbani Kwa Marehemu Juma Mfaume na kutaka kuchukua "assets" za huyo Marehemu??

Kutokana na kifo hicho Cha Juma Mfaume, ambaye alikuwa hadaiwi na Wala hakufahamu mkopo huo aliochukua mkewe Khadija Ramadan, ni dhahiri kuwa kampuni hiyo ya OYA wamefanya mauaji ya makusudi Kwa Marehemu Juma Mfaume.

Pamoja na hilo tukio lililotokea la kuuawa Kwa Juma Mfaume, lakini lawama zote nazitupia Kwa taasisi zeru za Fedha, kama vile BoT, Kwa mtindo wa wa urasimu mkubwa na sera mbovu za ukopeshaji za mabenki yetu.

Hivi kama taasisi zetu zingekuwa na sera nzuri za ukopeshaji, wananchi wasingependa kwenda kukopa Kwenye miyo mikopo umiza ya makampuni ya mikopo kama hiyo ya OYA.

Kwa hiyo ningependa kutoa rai Kwa taasisi zetu za Fedha, ikiwemo BoT zilegeze na zirekebishe masharti ya kukopa, Ili kuwaepusha wananchi wengi kukimbilia Kwenye hiyo mikopo inayoumiza sana wananchi Kwa kipindi hiki ambapo wananchi wengi wanaangamia

PIA SOMA
- Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo

- Mfahamu Juma Jangalu anayedaiwa kuuawa na wafanyakazi wa OYA
 
Back
Top Bottom