Kutumbua majipu ndio msamiati ambao Mh.Rais ameanza nao kujaribu kueleza maono yake kwa Tanzania
Kama sijakosea majipu ni matokeo ya mwili wa mnyama au binadamu kuwa na hitilafu fulani,inayosababisha damu kuchafuka...na kusababisha hali hii(tafsiri ya yangu
Kwa wale ambao tumewahi kuugua majipu angalau mara moja tunajua wazi kuwa kutumbua jipu ni hatua ya mwisho ambapo jipu linakuwa limeshakuiva ...na kukuumiza ! Na hii inawezekana tu kama jipu hilo halitakuwa la kujirudia!Kama litajirudia utabaini kuwa kutumbua jipu sio dawa bora!
Kwa kuangalia hali ya nchi ilivyo ni kama,mwili wa binadamu uliojaa majipu yanayoota na kuiva kila siku uchao! Na Mh.analijua hili ndio maana amekuja na dawa ....kuyatumbua!Hofu yangu atayatumbua mpaka lini! Inaeezekana akaendelea kuyatumbua mpaka mgonjwa akafariki .Hii njia haimsaidii mgonjwa,hapa ni lazima daktari aangalie kwa nini majipu,afu aabze kutibu chanzo na sio matokeo! La sivyo utaishiea kulowa damu na usaha mchafu na mgonjwa akufie mikononi!