Kutuhumiana ubadhirifu wa fedha na minyukano wa viongozi CHAKUHAWATA Mpanda inatukatisha tamaa Waalimu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
515
1,238
Screenshot 2025-01-24 182317.png

Screenshot 2025-01-24 182332.png

Nasikitika kwa kile kinachotokea kwa Chama chetu cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA), Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi kwa baadhi ya viongozi kuona sasa chama hiki kugeuzwa kuwa mradi wa viongozi wa chama Manispaa ya Mpanda kujipatia fedha.

Tumechagua viongozi kwa ajili ya kulinda na kutetea haki za walimu Mpanda na wala si vinginevyo kwa kukigeuza chama kuwa ulingo wa mnyukano wa kila kiongozi kuona ni shamba la bibi la kujipatia fedha.

Imani kubwa ambayo walimu wa manispaa ya Mpanda ambayo tunayo kwa chama hiki ni wazi inakwenda kutoweka na kama hakuna jitihada za kukomesha ufisadi huu mchafu hapa Mpanda, Sisi Walimu wote tutajiondoa ndani ya chama hiki na kurudi tulikotoka.

Tunaomba na kutoa wito za haraka za viongozi wa CHAKUHAWATA kuchukua hatua za haraka kukomesha tabia hiyo ambayo inasababisha viongozi wao kwa wao kushitakiana mahakamani.
 
Back
Top Bottom