Jose Mourinho yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester United pale msimu wa majira ya joto utakapowadia, baada ya kukaa nje ya soka kwa muda kutokana na kutimuliwa kunako klabu ya Chelsea.
Ujio wa Mreno huyo unaonekana kuwa pigo kwa baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo ambao inaarifiwa tayari Mourinho ameshatoa taarifa kwa uongozi endapo atakamilisha taratibu zote za kujiunga na klabu hiyo.
Wachezaji ambao inasemekana wamekalia kuti kavu ni pamoja na Juan Mata ambaye alisajiliwa kutoka Chelsea kwa paundi mil 37 na Marouane Fellaini aliyesajiliwa kutoka klabu ya Everton kwa paundi mil 27.
Jose Mourinho (kushoto) alimuuza Mata kwenda Manchester United akitokea Chelsea January 2014 baada ya kudai kiungo huyo haendani na mfumo wake.
Mourinho pia atamuuza Marouane Fellaini (kushoto) akitua Old Trafford
Mata na Fellaini walisajiliwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes
Mourinho ndiyo alikuwa sababu kubwa ya Mata kuondoka Chelsea, baada ya kudai Mhispani huyo haendani na mfumo wake na kuamua kumuuza kwa Manchester United ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa chini ya David Moyes.
Japokuwa Mata alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2013, Mourinho aliidhinisha Mata kuondoka klabuni hapo Januari 2014 kwa kitita cha paundi mil 37.
Mata akitambulishwa baada ya kutua kunako klabu ya Manchester United.