Kutokwa na harufu mbaya ya mwili

Pelly

Senior Member
Mar 26, 2013
193
204
Habari zenu,

Kuna siku nilipost humu natoka harufu mbaya hadi mke wangu anasema ya kizee. Baada ya uchunguzi wa kina nimegundua ni sehemu za siri yaani kuanzia kwenye korodani na pembeni yake hizi kona za mapaja wa kike wangesema mstari wa chupi unapopita kutenganisha kinena na paja, nimetaja wanawake sababu sikuhizi sijawahi ona duka linauza chupi za kiume kama lipo naomba mnielekeze.

Sasa ndugu zangu naombeni msaada dawa gani itanisaidia?

Miaka mitano iliyopita nilifanikiwatibu fungus zilizonitesa zaidi ya miaka 4,hizi zilisababishwa na kuvaa nguo za ndani mitumba na pia kuvaa nguo bila kujikausha ukitoka kuoga.

Naombeni dawa itakayomalizia ili tatizo japo nilisha pona fungus na wala haziwashi sana nimehisi itakuwa bado harufu I natokea huko.

Asanteni
 
Hauko serious inamana umepata mda wa kuandika humu na unashindwa kwenda hosp wanapopatikana wataalam wa afya na kupata vipimo pamoja na dawa au unahitaji upate hali mbaya zaid ndio uanze kumsumbua chalamila akupe majibu mujarabu uanze kulalama tena hum
 
Ni hizohizo fungus mkuu,tafuta tube nzuri za fungus pharmacy yoyote uwe unapaka ushaoga
 
Mabaki mengi ya chakula mwilini yasiyovunjwa huchacha na kusababisha harufu kwenye uwazi wa asili na maeneo ya karibu na huko!!

Fanya mazoezi,hakikisha unakunywa chai au kahawa baada ya mlo Ili kuoongeza mmeng'enyo pia ACHA kuvaa maboxer yanayo bana labda pale unapolazimika kufanya hivyo Vaa kadeti au jeans nzito bila chochote ndani uziache zipumue!!!!

Kama upo maeneo ya joto kama Dar,tanga au popote pale boxer usivae kabisaa labda pale unapochomekea shati ndio uvae!
 
Niliona mahali wanasema Limao ni Dawa. Jaribu kupaka maji yake.
Yes limao ni dawa lakini inatakiwa iwe endelevu na inatakiwa kuwa msafi sana hizo area na ni kwa wanaume tu wanawake kwa asili ya maumbile yao halifai,unajua baadhi ya wanaume huona sifa kurudia nguo ya ndani zaidi ya siku moja hawajui wanalea tatizo.

Kwa hapa mwanzo mleta mada paka limao siku saba continuosly kisha utakuwa unajitengea siku kadhaa ndani ya mwezi uwe unarudia kupaka,mimi nimetenga siku moja kila wiki kwamba siku nne kwa mwezi na imenisaidia,kama utakuwa interested na tiba hii nakushauri uwe unajipaka usiku ukishaoga kupumzika kwa sababu ukijipaka mchana then ukavaa sarawali utatengeneza hali ya joto litakalosababisha kero na michubuko mikali.

NB;tiba ya kwanza ni usafi,oga vizuri,nguo ya ndani vaa siku moja tu na nyoa mav√zi mara kwa mara kadiri uwezavyo.
 
Habari zenu,

Kuna siku nilipost humu natoka harufu mbaya hadi mke wangu anasema ya kizee. Baada ya uchunguzi wa kina nimegundua ni sehemu za siri yaani kuanzia kwenye korodani na pembeni yake hizi kona za mapaja wa kike wangesema mstari wa chupi unapopita kutenganisha kinena na paja, nimetaja wanawake sababu sikuhizi sijawahi ona duka linauza chupi za kiume kama lipo naomba mnielekeze.

Sasa ndugu zangu naombeni msaada dawa gani itanisaidia?

Miaka mitano iliyopita nilifanikiwatibu fungus zilizonitesa zaidi ya miaka 4,hizi zilisababishwa na kuvaa nguo za ndani mitumba na pia kuvaa nguo bila kujikausha ukitoka kuoga.

Naombeni dawa itakayomalizia ili tatizo japo nilisha pona fungus na wala haziwashi sana nimehisi itakuwa bado harufu I natokea huko.

Asanteni

Pole sana.

Ni muhimu ukafika hospital uonane na daktari ili akufanyie uchunguzi na vipimo ili upatiwe matibabu sahihi.

Pia ni muhimu ukazingatia
-usafi wa mwili na mavazi
-chakula unachokula kila siku. Hakikisha unakula matunda na mbogamboga kwa wingi kwenye milo yako.
-mazoezi ya mwili

Kila la kheri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom