Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,814
- 13,580
Habari wakuu,
Leo kuna Mkutano mkuu wa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini unafanyika Dar Es salaam. Mgeni rasmi ni rais Magufuli.
Ntawaletea updates ya kile kitakachojiri Moja Kwa Moja (LIVE) kutoka Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam.
UPDATES: 0945HRS
Rais kashaingia ukumbini.
UPDATES; 0950HRS
Anakaribishwa Askofu Kakobe kufungua kwa Maombi.
Anasema sio Vizuri kupinga kila kitu kana kwamba hakuna kilichofanyika.
Kuna watu wakisikia Rais Magufuli anasifiwa masikio yao yanawasha.
Usiposifia hata hoja yako haitasikilizwa. Sifia kwanza ndipo utoe hoja yako isikilizwe.
Kitabu cha wafilipi 4:8 8 Hatimaye ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa, yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo uzuri wo wote, pakiwepo na cho chote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.
Mungu ametupendelea sana Nchi hii.. Ukiangalia kule Kilimanjaro mpaka umepinda ili tu mlima uwe kwetu.
Tumezungukwa na bahari, maziwa na maliasili za ajabu sana.. Moja ya urithi tuliopewa ni madini.
Tumemuita rais kwamba ni shujaa kwa sababu miaka mingi watu wamekuwa wanaimba nchi masikini.. Lakini Magufuli kasema nchi yetu ni tajiri na inaweza kugawa misaada. Naomba rais uendelee kuimba hivyo ili kila mtu aimbe nchi yetu ni tajiri. Mwanzo 1:26-27 binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Unapokuwa unazungumza unaumba. Mauti na uzima vipi kwenye uwezo wa ulimi.
Kwa miaka mingi tumekuwa tukijitakia laana. torati 28:1-15 ni sura ya baraka na laana.. Zimetajwa mstali wa 33 na 43.
Katika maombi ninayokwenda kuomba namkabidhi rais katika mikono ya bwana na kufanya nchi hii iweze kuneemeka. (anaomba)
1005HRS:
Simon Msanjila katibu mkuu Wizara ya Madini anafanya utambulisho kwa Wagemi waalikwa na Viongozi mbalimbali
1015HRS
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda anaongea.
Napenda kuwakaribisha wote katika jiji la biashara, jiji salama. Anawatambulisha Viongozi wa dini akianza na Askofu Gwajima.
Wananchi wa Dar wameniomba nikufikishie. Kazi ya kujenga taifa na utaifa alishafanya baba wa taifa. Na hii ndo kazi umeachiwa kwamba Tanzania inakuwa moja. Sisi ni Watanzania lakini kwa utaifa hatujawa wamoja.
Kuna mpinzani mmoja alibwabwaja kule nje. Utafikiri yeye sio mtanzania na Mtangazaji ndio Mtanzania. Watu wamsamehe tu Tundu Lissu. Alipoulizwa akasema bado anaumwa.
Kuna nchi moja wamepitishwa muswada. Kuna nchi wanasema tanzania wasipitishe umeme.. Yaani nchi nyingine wanatupangia tufanye nini. Wananchi wa Dar wamenituma wamekuomba, ukikata tamaa, soma neno la Mungu. Mungu akitazama tanzania anakuangalia wewe. Tunaendelea kukuunga mkono. Kejeri zinazosemwa kwa baadhi ya watanzania. Mungu aliaandaa sehemu mbili. Usihangaike na watu wanaokwenda motoni
1025HRS
John Bina rais wa Wachimbaji wadogo Tanzania anaongea.
Wachimbaji wamenituma nikwambie kwamba umewapa heshima kubwa sana. Hata mimi mchimbaji mdogo nakaa high table. Wametuma nikuambie ukifika na ukatuangalia tu kwetu inatosha.. Wamesema namba yao sasa inafika Mil 6 wamesema wanakuunga mkono, chapa kazi
Tunakupongeza kwa kuleta Wizara ambayo inashughulikia madini peke yake. Na kuwateua viongozi wa hiyo Wizara wanaochapa kazi.
Kwa niaba ya wadau wa madini tunaomba upokee pongezi, tunashuhudia mageuzi makubwa. Umepunguza fukuzafukuza kwa wachimbaji wadogo. Umefanikisha kufutwa kwa kodi za kero kweye madini ya chumvi.
Umeimalisha uahirikiano katika Serikali na waxhimbaji wadogo.
Umetuletea Sheria nzuri ya madini ya mwaka 2007
Umejenga ukuta wa mererani.
Umetuletea ndege
Wanafunzi wetu wanasoma bure.
Wanaokubeza kwenye ndege washindwe na walegee. Nani haoni ujenzi wa reli, kikokotoo, stiegler's gorge nk.
Tulikuwa watetezi wakuu wa wachimbaji wadogo, lakini wewe ndo mtetezi wao sasa.
Tuna changamoto katika sekta ya madini.
1. Swala la mtaji. Mchimbaji hakopesheki kutumia madini yake wala leseni yake. Tunaomba tuweze kuwa tunakopesheka
2. Soko la uhakika. Hakuna masoko rasmi. Masoko yaliyopo nchini sio rasmi na bei elekezi hakuna hii inachangia ukwepaji wa kodi. Fedha inayonunua madini inayoingia na kutoka haijulikani
3. Utekelezaji wa sheria ya kusafirisha madini yaliyochakatwa hayajatolewa muongozo kwamba wachakatwe kwa kiwango gani yaweze kwenda nje. Angalia namna ya kuwasiaidia waliokwamba kwenye hii sheria
4. Uchimbaji wa kiholela. Kuna wachimbaji wanakuja kuchimba bila leseni.
Kuhusuani na maeno mazuri yaliyofanyiwa utafiti mengine wapewe wachimbaji wadogo.
5. Utozaji wa kodi usio rafiki kwa mchimbaji mdogo. Tunaomba mchimbaji mdogo akatwe kodi pale anapopata madini
MAPENDEKEZO
Tunapendekeza kuwepo na banki ya madini
BoT ianze kununua madini kwa sasa.
Kwasasa wanunuzi wa dhahabu hawaonekani.. Wanazira. Benki itakapokuwepo watacontrol soko. Gramm imetoka kuwa elfu 80 hadi elfu 30.
Tanzanite uiwekee hati ya Utambulisho. Kuna migogoro Mingi kwenye Tanzanite. Tunaomba uweze kuangalia.
Tunaomba Serikali iwasemee wachimbaji wadogo wasamehewe kodi ya viwanja ambayo hayajachimbwa.
Ushuru wa huduma ukatwe kwa mjibu wa sheria na sio kwa kudilia.
Serikali iongeze elimu katika uchimbaji wa madini. Tupo makini kwenye kuchimba lakini sio biashara.
Madini ya chumvi ni rahisi kuchimba hivyo tunaomba yachimbwe na watanzania au awepo mbia.
Tunaomba kuwe na siku ya madini iwe tarehe 5July kila mwaka. Tuna madini zaidi ya 560. Hii siku tunapendekeza iitwe Magufuli day.
Kundi hili ni kundi kubwa sana. Tunaomba tupate muakilishi ndani ya bunge.
1053HRS
Anaongea Abdulmajid Musa Nsekela, Mwenyekiti wa umoja wa mabenki nchini
Tunakupongeza rais kwa kuhakikisha Sekta hii ya madini inakuwa kwa kasi sana
Sekta ya fedha ni Sekta muhimu sana. Ni muhimu sana TBA kishiriki katika mjadal huu. Naomba nikihakikishie Sekta ya fedha ina uwezo. Idadi ya mabanki yamefia 52 yenye amana tril 29.9 za kitanzania.. Mwaka 2013 ilikuwa na tril 13.. Tuna matawi zaidi ya 800 nchi nzima.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali benki nyingi zimejiunga kwenye mfumo wa ulipaji kodi wa Serikali. Benki ambazo hazijajiunga naomba zifanye hivyo.
Milango ya mabenki ipo wazi kwa wawekezaji wa madini wadogo kwa wakubwa
Bil 357 imetolewa kama mikopo kwa watu wanaojihusisha na shughuli za madini tu.
Uchimbaji kwa wachimbaji wadowadogo umekuwa duni sababu hawajaingizwa kwenye mfumo rasmi. Tumeshindwa kutoa mchango unaohitajika kwao.
Baadhi ya changamoto
1. Wengi wanaukosefu wa leseni. Na wale wenye leseni wanazikodisha
2. Upembuzi yakinifu ya mapato na matumizi.
3. Wachimbaji wadogo wamekosa mshikamano na umoja
4. Wachimbaji wadogo wengi wamekuwa wakihama hama. Dhamana zao kidogo ni ngumu.
Changamoto hizi zimekuwa zikicheleweshwa maamuzi ya kusikilizwa na mabenki.
Nichukue nafasi hii kuwaomba wachimbaji wadogo waanze kujipanga kimkakati ili kuweza kutatua changomoto ya kukosa huda za kibenki.
Tunatumaini Serikali kupitia Wizara husika watakuja na mkakati unaoelewaka wa ununuzi wa madini ili kuleta tija.
1113HRS
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula ambaye amemuwakilisha Spika wa Bunge anaongea
Nasimama kuleta salamu za Spika. Ameomba radhi kwamba ikupendekeze kwa kikao hiki nimuwakilishe. Ana kazi nyingine kubwa inafsnyika kule bungeni
Tunakupongeza kwa kuweza kupkea Mawazo na mapendekezo yatakayowezesha Sekta ya madini yatakayoweza kuwanufaisha Watanzania.
Tunashudia Wizi na walanguzi wa madini yetu hawafanikiwi.
Umetoa agizo la kuhakikisha sasa kama nchi tunaanza kuwa na soko letu la madini
Kwa niaba ya spika tunapenda kukupongeza sana kwa maamuzi yaliyofanyanyika jana kwa kodi ya umeme kutozwa kwa asilimia 0. Hili ni jambo kubwa la kudumisha muungano. Ni kitu bunge limekuwa likitamani. Hasa hili la kifutwa kwa deni la zaidi ya bil 22.
Tunashukuru sana.
1120HRS:
Waziri wa Madini Dotto Biteko anazungumza
RAIS MAGUFULI(Rais Magufuli anaingilia kati)
Kabla ya Biteko Mimi nmekuja kusikiliza. Nmesikia changamoto za wachimbaji wadogo, nmesikia changamoto za Mabenki.
Leo nataka nisikie kwa wadau. Mumekuja hapa si sisi kuwapa hotuba bali mtupe hotuba sisi. Mimi nataka nisikie huko kwenu. Ninachoomba mzungumze kwa uwazi. Mawaziri wote, makatibu wakuu wapo hapa, Viongozi wa vyombo vya ulinzi wapo hapa.
Naomba mpige penyewe ili tujue ni nini kinaturudisha nyuma. Tujue kwanini madini yetu yanatoroshwa. Kwanini tra hawakusanyi kodi?
Kwanini makamishina wa madini wanalipwa mishahara na sheria. Kwanini madini yanatoroshwa na wao wapo na hawajawahinkusa kodi.
Tume ya dhahabu inafsnya nini?
Madini Kelwa kwanini yanauzwa lakini yanachimbwa.
Kwanini Tanzanite tumejenga ukuta lakini bado yanatoroshwa?
Kwanini hatuma masoko ya madini wakati makatibu wakuu wapo?
Hujawaeleza soko liko wapi lazima waeleze.
Tusipojibu haya maswali. Magumu tutakaa hapa na tutatoka bila jibu.
Kwanini bot hamtunzi dhahabu ili dola ikitelemka dhahabu ipo.
Kwanini wanunuzi wa humu ndani wanashawishika kutokulipa ushuru.
Mimi kwa maoni yangu na ushamba wangu nlifikiri haya ndo ya muhimu. Mimi nataka nijue kama kiongozi wenu.
Mimi nataka nijue kwanini Sekta ya madini inachangia asilimia 4 na sio asilimia hata 10.
Sasa naomba nichukue uchairman watu waanze kuzungumza.
Wanaokubali waseme ndio. Wasiokubali waseme sio. Waliosema ndio wameshinda. Sasa naanza kuwasikiliza. Nani anaanza.
Ananza wa tanzanite.
Anasema kuna matatizo kuhusu uchimbaji na utoroshaji madini.
1. Pale ukutani ukuta ulijengwa vizuri. Changamoto ni mshahara. Kila mfanyakazi anatakiwa kulipa mshahara. Migodi iliyoko ndani haifika 50. Mapato yanayopatika, ule utoroshwaji umepungua sana.
Hakuna mtu anayeruka ukuta kutoka ndani bali wanaruka ukuta kuingia ndani kutafuta mali. Mtu anayeingia ndani ya ukuta awe analipa mshahara
2. Sisi tunawajua wanaotorosha madini. Tunakuomba hata nusu saa tunaweza kuwataja. Tanzanite inatoroshwa na wageni. Vyombo vya ulinzi vifuatilie. Mtu anatorosha anakamatwa anapigwa fine na anarudi kuchimba madini.
Leopard Mtalwema anasema uchimbaji wa tin sasa ni miaka mitatu tumezuiliwa kuuza tin bila kuyeyusha. Miaka mitatu tumekuwa tukihangaika hatuna sehemu ya kuuza.
Mdau wa Almas:
Kero ya kwanza ni uwepo wa taarifa sahihi za deposit za dhahabu lakini si almas. Tunaomba tupate taarifa sahihi za uwepo wa Almas na bei elekezi.
2. Teknolojia duni ya uchimbaji.. Tunaomba Serikali iweze kutoa support
3. Kwenye Almas pia kuna utoroshaji wa madini. Wanunuzi wa dhahabu wanashindwa kununua leseni. Sababu leseni ya kununua almas si chini ya Mil 5.
Watu wa dhahabu;
Solomon anaongea
Kwanini dhahabu zinatoroshwa na tufanye nini?
Kwenye nchi yetu 95% ya dhahabu nchini inatoroshwa.
Tuna watu mil 6 wanaojishughulisha na mambo ya madini. Kwa siku tunaweza kuvuna tani 5 kwa siku watu mil 1 kwa wastani.
Dhahabu kwenye nchi yetu, kinachofanya dhahabu iibiwe ni kodi. Kodi inazidi mtaji.
Ukishaipata dhahabu unakodi ya
Kodi ya huduma ya 0.3%
Kodi ya royality 60%
Kodi inspection 1%(hii ilikuwa kwa wasifirishaji)
With holding tax 5%
VAT 18%
Sheria inasema kwa kila mil 100 unatoa mil 18 unaipa Serikali.
Hapa ndipo kunapotokea kizaa na mtu mmoja akasema ni sukumia ndani.
Kwa nchi nyingine. Dhahabu hilindwa na mwenye dhahabu.
Polisi tutawalaumu bure.. Kuna njia nyingi ya kutorosha dhahabu na polisi sio rahisi kujia. Mipaka yetu kuna mahusiano mazuri. Watu wanapita huku warudi huku. Vyombo vya usalama vipo vizuri. Dhabu inatoroshwa kwa side mirror, spare tyre, kabeji, tikitimaji nk.
Dhahabu yetu tuliyonayo dhahabu inaweza kuingizia hata 50% serikali. Kwanini dhahabu ni serikali inaibiwa si mfanyabiashara? Ukitaka kusema unaambiwa huwezi kufundisha Serikali.. Unaamua kuacha.
Tafuta watu wenye uzoefu. Wasomi wanasoma miaka minne. Lakini kuna watu wapo field mika 50. Waajiriwe wenyebuzoefu.
Watu wana mbinu nyingi za kutorosha madini. Ajiri wenye taaluma na wenye uzoefu.
Naomba uondoe hizi kodi mbili. VAT na withholding tax.
Fatuma Kikuyu anazungumzia Tanzanite: Vijana walio nje ya ukuta ni wengi kuliko walio ndani. Hatuna mshahara, waruhusu vijana waingie ndani wafanye kazi. Tunaomba uwaachie vijana wafanye kazi. Hatuwezi kulipa mishahara. Vijana hawataki mishahara, wanataka 10%.
Kishimba mbunge anasema
Swala la dhahabu ni kubwa. Na iponaina tatu. Kati ya hizo serikali inapata aina moja ambazo ni chache.. Hizi mbili ambazo ni nyingi si rahisi kuzipata.. Mtu anachimba bila msaada halafu akiuza unataka kwenye mil 100 serikali ipewe mil 28. Hauna wa kukubali.
Wachimbaji ni watu wenye uzoefu na akili nyingi. Hii ambayo haionekani iruhusiwe iletwe BOT. Wachimbaji wadogo wapo mil 6.
Kila 700 za dhahabu zinapotea kila siku. Ni vizuri BOT wanunue. Tatizo letu kubwa ni hilo.
Nchi ya afrika ipi yenye kiwanda cha chuma? Hakuna.
Nashauri tuuze nje chuma wakati tunajenga hicho kiwanda cha chuma
Matias Rwechungula mnunuzi wa dhahabu.
Tulitoa mapendekezo mwanzoni tuwe na marketing centre.
Mnunuzi wa Almas
H. Salvatory kutokea shinyanga.
Tunapungukiwa na wataalam mavalua. Kwa tanzania upande wa shinyanga yupo mmoja tu. Akiugua huwezi kusafirisha. Wapo watatu. Mmoja dodoma, dar na shinyanga.
Mhandisi Joseph kumbulu afisa madini kazi Mbulu.
Changamoto tunayoipata ni wachimbaji kulipa kodi.
Ofisi ya manyara ni mpya ina watendaji 5 na gari moja kwa manyara yote. Tuna upungufu wa wafanyakazi
Tatizo lingine ni kodi ya service levy. Inasababisha wachimbaji kutukimbia.
Dr. Omary Mzero wa Morogoro
Mtazamo umekuwa kwenye madini machache. Vito havithaminiwa. Morogoro tuna madini ya aina mabalimbali zaidi ya 200.
Maeneo mengi ya Morogoro yana leseni kubwa. Wachimbaji wadogo tunakosa sehemu ya kuchimba kwani penye vito pameshikiliwa na wenye leseni kubwa. Wachimbaji wadogo morogoro tunazidi 6,000. Wachimbaji wadogo tupewe vitambulisho kama Wamachinga ili tuweze kuchimba.
Mfanya biashara wa madini ya Vito anasema;
Sisi tuna hamu ya kulipa kodi lakini leseni ya ndani ya blocker tonatozwa dola zaidi ya Mil 150. Halafu ni hatua ndefu za kufuata. Unakaa hata miezi mitatu. Kuna urasimu wa dola. Tupo zaidi ya laki 5.
Leseni ya blocker punguza bei watu watakata kama mil 1.
Wachimbaji wa vito ni wengi kuliko wachimbaji wa dhahabu.
Zuio lako la kusafirisha madini ya vito limeleta madhara makubwa kwa wachimbaji. Hatuna wataalam.. Hatuna machine.
Tunaomba kipindi cha mpito kusafirisha madini.
Asha jummanne ngoma anasema
Nlishauri kupendekeza kutangaza madini nje ya nchi, nlipeleka maombi lakini sikujibiwabtangu 2007. Nakuja kujibiwa kwa kuchelewa 2014 kwamba imeshafanyika. Nikawa nmekosa hiyo fursa.
Hamisa Omary Kambi
Nmezuiwa kuchimba mchanga wakati Mkurugenzi kaniruhusu na nina leseni. Nanyanyasika.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Sisi kama mkoa tunapata changamoto katika migodi mikubwa.
Tunasimamia vizuri uzalishaji wa dhahabu na almas.
Changamoto ni mzigo unaosafirishwa tunajua uzito lakini hatujui thamani.
Kama mkoa tunasimia changamoto ni dhahabu na almas zinazozalishwa pembeni. Soko la almas halijulikani.
Solution tuanzishe soko kwaajili ya kuuza madini. Tulishawahi kulizungumza na mawaziri. Tupate eneo la kujenga soko la madini yetu
Polisi wanasema; Watanzania tuwe wazalendo. Na waaminifu.
Gavana: Benki kuu tupo tayari kununua dhahabu. Hapo awali tulikuwa tunanunua, lakini tulikuja kuuziwa dhahabu feki tukaamua kusitisha. Sasa tupo tayari kununua dhahabu inayotambulika kimataifa.
Tunashirikiana na wizara ya madini na benki kuu ipo tayari kuanzisha masoko.
Tupo tayari pia kuhifadhi dhahabu ambayo inasubiri wanunuzi.
Mwenyekiti wa stamico anasema;
Stamiko inahakikisha inashirikiana na wachimbaji wadogo kuwapatia vifaa vya kuchimba na kufanyia uchunguzi.
Kupitia wizara yetu ya madini baada ya muda mfupi tutaanza kutekeleza hilo. Kwakuwa bado tupo kwenye mchakato, tupewe muda wa kutekeleza majukumu.
Askofu Gwajima
Leo rais umekuwa kama nabii. Nliwaza nitoke bila kuongea
Watu ambao hawakuzaliwa kwenye ukanda wa madini sio rahisi kujua madini.
Si kweli hatuna soko la madini. Dhahabu yenyewe ni fedha. Nakushauri uwe na watu wenye siasa za biashara za madini. Unaweza kuunda watu wenye akili wa hii kitu. Sio elimu, elimu tu haitoshi..
Sitaki upunguze ushuru bali tuangalie ni namna gani tunatoza ushuru ambao haumuumizi mchimbaji.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuna marekebisho ya sheria kwa upande wa madini wanaenda kuyafanya haraka sana ili kupunguza kero upande wa wachimbaji wadogo
Waziri Biteko
Kikao hiki ni kikao cha mashauriano. Tunataka tufungue ukurasa upya kati yetu. Hizi siku mbili nitakuwa na ninyi. Naomba tushikamane. Sikusimama hapa kujibu hoja. Nawaomba sana, semeni kile mnachoamini tunaweza tukakibadilisha.
Hivi ninavyoongea kuna timu ya wataalam wapo dodoma wanatuandalia kanuni na sheria za Masoko hayo. Tunaomba tupewe muda mdogo tunalikamilisha.
Wale wote waliokija ofisini kwangu kulmba vibali, nawahakikishia tutawajengea mfumo wa kuondoa urasimu.
Ukikwaza sio kwa niamba mbaya, tunataka tuunganishe nguvu zetu.
Nawaomba wachimbaj wote, mimi tutakutama tutazungumza zaidi.
1425HRS
Rais Magufuli anasema.
Nashauri kwa kunikaribisha katika mkutano huu wa Mashauriano. Kila mkoa Tanzania una madini.
Mungu ametujalia utajiri mkubwa wa madini ya kila aina.
Wale wa chuma cha liganga walitaka kutulalia ndo maana hatujawapa. Kulikuwa na madini mengine hawajazungumza. Nchi hii imependelewa kwa kila hali
Nchi yetu haijanufaika vya kutosha na madini haya, haijainua vipato vya watanzania isipokuwa kwa watu wachache. Mchango katika pato la taifa ni 4%. Hii yote ni sababu ya ukosefu wa Masoko, mitaji, mikataba mibovu, kutokuwa na mikakati, mikakati ya kuwatambua wachimbaji wadogo, tulirenga wawekezaji wakubwa.
Nikili Serikali tulijisahau na kuangalia Sekta nyingine. Ndio maana nawashukuru ninyi wadau mlioamua tukae pamoja tushauriane kwa uwazi.
CCM katika ilani yake iliahidi kusimamia sekta ya madini. Tumerudisha umiliki wa raslimali za madini kwa watanzania, tumeunda wizara mahususi, tumepitia mikataba ya madini, tumeongeza usimamizi, tumejenga ukuta mgoni wa Tanzanite, tumetoa leseni 15, 206 kwa wachimbaji wadogo
Bil 7 tumezitoa kama luzuku kwa wachimbaji wadogo
Mgodi wa mwadui umezalishwa 341 elfu
Tulipanga kukusanya Bil 164 tumekusanya bil 301.
Uzalishaji na mapato kutoka kwa wazalishaji wadogo umeongezeka.
Tumedhibiti utoroshaji wa madini. 332 za madini tumezikamata mwanza.
Mchango wa madini Kwenye pato la taifa umeeongezeka kutoka asilimia 4 mwaka 2015 hadi 4.8% mwaka 2018
Bado hatujafikia kule tunapokutaka. Bado tuna safari ndefu.
Zile asilimia zilizokuwa zinatozwa kwa kitu kimoja haziwezi zikakubalika. Kwahiyo kikao hiki nmejifunza sana.
Waziri na katibu wakuu wa wizara ya fedha na madini, katika kikao hiki mumejifunza
Mawazo yenu ni mazuri, ntashangaa kama mawaziri wangu hawataguswa.
Tani laki 6 zinauzwa wapi?
Nlipochaguliwa kwenda wizara ya ujenzi nlifukuza mainjinia 261. Nlipopeleka kwa Sumaye akakataa, Mkapa akasema fukuza..
Mainjinia walikuwa wanatembea kwa manoti kwenye Socks. Baada ya hapo barabara zimejengwa maelfu kwa maelfu.
Ndo maana mwaka jana nlisema watengue.
Mimi kufukuza mawaziri wa madini sisiti. Ndo maana nikasema siku ike nakuapisha Hata wewe nikiona mambonhayaendi unaondoka
Tumeshindwa kitu gani kutafuta mtu tumwambie jenga gold smelter hapa.
Wizara ya madini kuletewa zawadi ya kupelekea mke wako ni kitu cha kawaida.
Hizi fedha zinazopatikana ndo zinatengeneza barabara, zitaleta maji nk.
Sisi wote tutakwenda kujibu tumewatendea nini watanzania. Tulikuja uchi na tutaondoka uchi na sanduku moja tu.. Nothing.
Yale mtakayoyaamua hapa, kama mnauhakika haya mabadiliko yataleta manufaa nipo radhi niwaambie wabunge wafanye mabadiliko.
Tanzania tuna dola Bil 5.3 hifadhi ya fedha za kigeni. Nchi inaweza kujiendesha kwa miezi mitano bila kufanya kitu chochote.
Kwanini hii hela tusinunue dhahabu? Kila mtu anahitaji dhahabu hata dola ikishuka.
Tunadanganyana wee sababu ya interest zao.
Centre za kuuzia madini ni kitu muhimu. Pamba, kahawa wana centre zao. Tanzanite pamoja na kujenga ukuta hadi leo hawajajenga centre. Kukosa uaminifu ndio unatuponza sisi watanzania.
Uangaliwe utaratibu mzuri zaidi ya watu wanaoingia kuchimba Tanzanite, hamna haja ya kuwazuia. Watu wanatafuta ajira na ajira zao ni nguvu zao. Kuwazuia hatuwatendei haki. Mbona ikulu watu wanakaguliwa na ikulu hawaji kuchukua kitu.
Nliagiza zifungwe Camera pale Tanzanite lakini hadi leo hazijafungwa. Unaangiza hawatekelezwi.
Sasa nakuagiza wewe, ndani ya mwezi mmoja Camera ziwe zimefungwa tofsuti na hapo nakufukuza wewe na watendaji wako. Tafuta mtu yoyote akafunge pale ukimkosa waambie watu wangu watakupa..
Kila mmoja anapotaka kufsnya kitu anataka akapate percentage ngapi.
Siku namaliza muda wangu na ninyi mtakuwa mumemalizika. Siwezi. Nakwambia waziri Biteko uwe mkali. Aliyekuwa waziri pale hakuwa mkali ndo maana nikaona akapumzike ofisi ya waziri mkuu pale. Naongea ukweli that's me.
Nchi hii tumeibiwa mno. Halafu kila siku tunaimba sisi ni masikini. Kuna mfadhiri wa kukufadhiri wewe? Wanajifadhiri wenyewe. there is no free lunch.
Mambo mengine ningependa tuyashughulikie ni
Usimamizi kwenye sekta ya madini hasa mikataba na vipengele vyake. Ikiwemonkufanya ukaguzi mara kwa mara kwenye migodi.
Kule ilipokuwa inauzwa tanzanite, imepoteza kazi za watu 15 elfu. Kwanini wasingefanya kazi hapa Tanzania
Watu 17 walijitokeza kuja kujenga smelters hapa. Mpaka leo hatuna Smelter. Na wanaotaka kuja kujenga hawapewi.
Tuwe na tabia ya kuamua. Kama umepewa wilaya, wizara, mkoa taasisi amua. Msiwe wavivu wa kuamua.
Kule Kelwa tuna tin nyingi. Tangu shule ya msingi nlikuwa nasomaga kwenye historia.
Watu wanakatazwa kusafirisha eti rais kazuia makinikia. Nmekuzuia kupita kwenye mlango hata kuchungulia dirishani umeshindwa?
Kwanini msiseme leteni hapa lipa ushuru wetu pelekeni mnakotaka. Kazi hizi za uwaziri ni risk.. Chukua risk ili mambo mengine yaende.
Mimi ninachohitaji ni mapato, wananchi wanadai hawajatengenezewa utararatibu wa kulipa mapato. Mablocker mnawatoza dola halafu mnampa risiti feki.
TRA hawajachangamka.. Mimi ni refa. Nakupiga njano au nyekundu. Njano nakuhamisha wizara na nyekundu unatoka nje huku unauangalia mpira.
Nakuagiza waziri, sijui utaunde tume utaiijmtaje. Kafuteni maeneo yote ambayo yameshindwa kuendelezwa. Mara 10 muwape wananchi wetu walipe kodi. Maeneo ya madini ambayo hayajaendelezwa yafuteni
Waziri naona unalalamikiwa. Unapolalamikiwa jua upo katika best direction.
Uwekezaji wa wachimbaji wadogo wadogo na wakati. Kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wakubwa sio ubaya, ubaya unakuja unapowasahau hawa wadogo.
Watu 11,500 wapo kwenye migodi mikubwa na migodi midogo wapo Milioni 6. Nguvu zetu ziende kwa hawa wengi.
Tuachane na maneno ya michakato. Tumechakata mno.
Niwaombe watu wa madini, vumilieni kwa siku mbili, tulikuwa tumechelewa mno. Mimi sina tatizo lolote kwa yale mtakayokubaliana kwa manufaa ya tanzania
Almasi ni dola 500 hadi 1000. Kwenye bei wanayopewa Serikali ni 280. Ni aibu. Nafuu upeleke darasa la nne atakuwa mzalendo.
Huyu alitakiwa ashitakiwe kwa uhujumu uchumi. Hatufai
Kikubwa ninafuraha kubwa kwamba mahudhurio ni mazuri. Na ninampongeza rais kwa kufanya hivi. Makongamano ya kitaiffa yaanzie hapa. Lazima tuamue mambo yetu wenyewe
Ni vizuri upunguze kidogo ukisanye kingi.
Hata mimi sehemu yenye kodi nyingi siendi. Hata mimi ningekwepa.
Huku nauza sikatwi, huku nikienda napigwa ningekwepa tu. Tatizo mnadhani michangoya wasiosoma haifai. Biashara haihitaji degree tena ukiendelea kusoma ndo inakushinda kabisa. Huyu kishimba anasema ni darasa la saba lakini tajiri ana maduka nk. Musukuma anasema ni la saba lakini ana mabasi, ana helcopter na kila kiitu
Kesho namtuma makamu wa rais mumkabidhi hayo mliyokubaliana
Natumaini Mawaziri na makatibu wakuu, mtashiriki, vyombo vya ulinzi na usalama mtashiriki, Wakina Kakobe mtashiriki kwemye mazungumzo haya.
Rais Magufuli amemaliza kuongea 1536HRS