Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Ludewa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
366
434
OFISI YA MBUNGE JIMBO LA LUDEWA

Januari 21, 2023 Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga akiambatana na Mweneykiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Wise Mgina na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Ndg. Gervas Ndaki wameupokea ugeni kutoka mamlaka ya bandari Tanzania ( TPA ) walio fanya ziara ya kikazi ya siku moja.

Katika ziara hiyo uongozi kutoka Mamlaka ya bandari Tanzania ( TPA ) walitembelea bandari ya Lupingu na Bandari ya Manda ili kujionea hali halisi ya maeneo hayo na ugumu wanao kutana nao wananchi pindi wanapotaka kusafiri kwa njia ya maji.

Akitoa maelezo ya mipango ya uboreshwaji wa bandari za Ziwa Nyasa Meneja wa Mamlaka ya Bandari zipatikanazo Ziwa Nyasa amesema mwaka huu utafanyika ujenzi wa bandari ya Manda kwa kuifanyia maboresho ya haraka kwanza ili iendelee kutoa huduma kwa ufanisi.

Alisema serikali imedhamiria kuboresha bandari zote za Lumbila, Ifungu iliyopo kata ya Kilondo, Makonde na Nsisi iliyopo kata ya Lifuma walau kwa kujenga vyoo vya kisasa na sehemu za kupumzikia abiria.

Ameongeza kuwa wapo kwenye mpango wa kuongeza ratiba ya meli iwe ina safiri mara mbili kwa wiki na siku za mbeleni kuongeza meli za abiria ziwe mbili.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Joseph Kamonga amewashukuru viongozi hao kwa kufika maeno ya bandari na kujionea adha wanazo kutana nazo wananchi wa Ludewa pindi wanapo safiri kwa njia ya maji.

Amewaomba viongozi hao kuzifanyia uboreshaji mkubwa bandari zote mbili kwani ni hitaji kubwa kwa wananchi wa kata nane ziishizo pembezoni mwa ziwa Nyasa lakini pia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Ludewa kwenda wilaya nyingine.

Baada ya kumaliza ziara ya kukagua bandari Mhe. Mbunge akiambatana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Ludewa, walikwenda kuangalia eneo lililo tengwa kwaajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari kata ya Ruhuhu ambalo wananchi wamelitoa.

Wananchi wameonesha uhitaji mkubwa wa sekondari kwenye kata yao kwani kila mwaka vijiji hivyo vitatu vya Kipingu, Ngelenge na Ilela vilivyopo kata ya Ruhuhu hupeleka watoto 115 Shule ya Sekondari Manda ili hali wangeweza kusoma kwenye shule yao iwapo ingejengwa.

Katika jitihada za awali wananchi wa kata ya Ruhuhu wamesha andaa tofali Laki mbili na elfu kumi, fedha taslimu Milioni mbili na eneo lenye ukubwa wa ekari 15.

Mhe. Mbunge amewapongeza wananchi wa kata ya Ruhuhu na kuwa ahidi kushirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha shule ina jengwa na watoto kutotembea umbali mrefu kwenda kufuata elimu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri aliwaahidi wananchi kuwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 , Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani itatenga fedha za kukamilisha madarasa mawili na iwapo watafanya vizuri wataongezewa madarasa mengine hadi shule itakapo kamilika na hayo ndiyo makubaliano yake na Mhe. Mbunge yaliyo shuhudiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa.

#Umoja na Kazi kwa Maendeleo ya Ludewa.

Imetolewa na m;

Ofisi ya Mbunge,

Jimbo la Ludewa.

Januari 22, 2023.
 

Attachments

  • IMG-20230122-WA0008.jpg
    IMG-20230122-WA0008.jpg
    103.6 KB · Views: 1
  • IMG-20230122-WA0009.jpg
    IMG-20230122-WA0009.jpg
    97.3 KB · Views: 2
  • IMG-20230122-WA0010.jpg
    IMG-20230122-WA0010.jpg
    104.1 KB · Views: 2
  • IMG-20230122-WA0011.jpg
    IMG-20230122-WA0011.jpg
    133.6 KB · Views: 3
Pia,umshauri Mheshimiwa Mbunge,afuatilie kwa umakini upatikanaji wa Mbolea!!,mpaka mwishoni mwa December vijiji vyote vilivyoko katika Kata ya Luana,mbolea ilikuwa haijafikishwa katika Kata hiyo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom