Kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Rombo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM Samora Kanje dhidi ya mh Joseph Selasini mwanasheria mkuu wa serikali na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rombo imechukua sura mpya baada ya maamuzi ya jaji anayesikiliza kesi hiyo kuamua kumruhusu kwa huruma bwana Samora Kanje ili atoe ushahidi mahakamani na kurekebisha hati zake za kiapo pamoja na Mashahidi wake baada ya Yeye mwenyewe kutokuwepo kwenye orodha ya Mashahidi wa kesi hiyo pamoja na kuwasilisha hati za viapo zenye makosa kisheria pia zilizopo katika LUGHA ya kiswahili kinyume na sheria.
Baada ya maamuzi ya jaji huyo ameiahirisha mpaka jumatatu wiki ijayo.
Kwa upande wa mawakili wa upande wa walalamikiwa wakiongozwa na wakili msomi Masumbuko Roman na wakili wa serikali Wanga wamefikia uamuzi kuandika hati ya kumkataa jaji anayesikiliza kesi hiyo na kuomba mahakama KUU iwapangie jaji mwingine kutokana kusuasua kwa mwenendo wa kesi hiyo pamoja na jaji kukosa weledi wa kimaamuzi katika kusimamia sheria kanuni na taratibu za kimahakama kwa kitendo chake cha kuamua kumruhusu Samora Kanje kutoa ushahidi ilihali Yeye sio shahidi katika kesi hiyo kwa mujibu wakili wake bwana Samba.
Kesi hiyo ataendelea tena jumatatu wiki ijayo SAA tatu asubuhi ndani ya mahakama ya hakimu mkaazi Rombo Mkuu.