Kutoka chama kimoja na kuhamia chama kingine ni uamuzi wa kijasiri na wa kipekee sana kisiasa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
21,410
23,066
Ni ukomavu, ujasiri na utashi wa kipekee sana kisiasa. Ni uamuzi mgumu na mzito sana kwa mwanasiasa. Kuachana na mazingira ambayo uliishi na watu ulo wazoea vizuri sana, na kuungana na watu wapya na wenye, itikadi, malengo na nia tofauti kabisa na chama ulichotoka. ni uthubutu wa kipekee sana.

Pamoja na kwamba inaweza kuimarisha haki, uhuru wa mtu kuamu atakavyo kujiunga chama cha siasa na demokrasia lakini pia inaweza kudidimiza, kudumaza au kukomaza ukuaji na uhai wa vyama vya kisiasa, mathalani chama kimoja kinaweza kunufaika na kingine kikaathirika.

Kwa mfano Taasisi zilizojengwa kwenye misingi legelege huduwazwa, huzubaa, hubabaika na kutaharuki kwa hali hiyo ya kuhamwa na mwanachama wao, huku wakimsindikiza kwa maneno mbofu mbofu na shutuma mbalimbali nzuri na mbaya mwanachama huyo muhamaji.

Lakini Taasisi zenye misingi imara na madhubuti hutumia hali hiyo ya kuhamwa kama fursa ya kujitatmini, kujisahihisha palipo na changamoto na kujiimarisha vizuri zaidi kusonga mbele.

Ukiachwa achika maneno mbofu mbofu ya nini tena, ndio ntolee hiyo 🐒
 
Kama wangekuwa wanahama kama mashabiki wa mpira bila kutegemea faida ya moja kwa moja kimaslahi, hapo sawa.

Vinginevyo, huo ujasiri umehafilishwa sana (underrated).
 
Back
Top Bottom