Kutoka Bungeni Sept 7, 2016: Chenge aionya Serikali kuhusu mazao, Nchemba amjibu Mbowe deni la Taifa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
95,470
167,286
Bunge limeanza na linaongozwa na Mtemi Chenge. Fuatilia

Mwenyekiti wa Bunge Mh. Chenge aionya serikali...

Wakuu,

Mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge ameitolea uvivu serikali juu ya tabia yake ya kuzuia wakulima/wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi na kupelekea baadhi ya mazao ya wakulima kuharibika kwa kukosa soko.

Akiwa anaongoza kikao, baada ya Naibu Waziri wa kilimo kujibu swali la nyongeza; Chenge alisema - "toka lini mfanyakazi/mwajiriwa analipwa mshahara wake halafu aje kupangiwa matumizi ya mshahara wake?"

Mwigulu:Taifa Linakopa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo

Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba amewaambia watanzania kuwa Tanzania inakopa ili kuwezesha ukamilishaji wa miradi ya maendeleo (development expenditures) na si matumizi ya kawaida(recurrent expenditures) wakati akiongezea majibu ya wizara ya fedha na uwekezaji.

Swali hilo lilikuwa la nyongeza liliulizwa na mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bunge Freeman Mbowe aliyeuliza kuwa 'deni la taifa linaongezeka kwa uwiano wa kila mtanzania anadaiwa zaidi ya milioni moja, je serikali ina mkakati gani wa kulipa deni hiloo?

Majibu ya Serikali kwa baadhi ya maswali yaliyoulizwa bungeni

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG]
imetoa wito kwa waajiri nchini kupeleka nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya jamii kabla ya miezi mitatu hadi sita ya muda wao wa kustaafu ili kukabiliana na changamoto zitakazoweza kujitokeza.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] itaendelea kuona haki inatendeka kwa mujibu wa Sheria ya Ajira ya Wageni Na. 1 ya 2015 ili watanzania waweze kuendelea kupata ajira katika NGOs na Taasisi binafsi.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] imesema hakuna mgogoro wowote kuhusu umiliki wa eneo lolote baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa tafsiri na suala zima la mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar limewekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya Zanzibar kabla na baada ya Muungano.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] imesema hakuna mgogoro wowote wa Mafuta na gesi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] imetoa wito kwa wanasiasa kutotumia masuala ya Muungano katika masuala yao ya kisiasa kwani watu wa pande mbili za Muungano ni ndugu ambao hata siku moja hawawezi kufarakana kwa sababu ya umiliki wa eneo.
[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] itaendelea kuvihimiza Vyama Vikuu vya Ushirika (Unions) kuangalia utaratibu wa kuvikopesha kwa utaratibu wa kuanzisha "Revolving Fund" badala ya kutegemea benki.

# Serikali haijakataza Soko la nje bali imesitisha kupeleka mazao nje ya nchi huku ikiandaa utaratibu halali wa kuuza mazao hayo nje kwa lengo la kukabiliana na janga la njaa nchini.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] inaendeleza maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda kwa ajili ya miundombinu ya msingi ili kuwezesha uwekezaji na ukuaji wa viwanda vidogo na vya kati katika Mkoa wa Kagera.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] inaendelea kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za ugani, upatikanaji wa pembejeo, utafiti na masoko ya mazao.

[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] kuendeleza viwanda vya nyama vilivyopo kanda ya ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera,
viwanda hivyo vitasaidia kuendeleza sekta ya ufugaji utakaoinua kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na kuendeleza uchumi wa mkoa husika.
Taifa linahiaji ustawi na uhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo, tunekeza.


Kipindi cha maswali na majibu kimeisha, Bunge mubashara limesitishwa. Kikao kinaendelea.
 
Wakuu,

Mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge ameitolea uvivu serikali juu ya tabia yake ya kuzuia wakulima/wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi na kupelekea baadhi ya mazao ya wakulima kuharibika kwa kukosa soko.

Akiwa anaongoza kikao, baada ya Naibu Waziri wa kilimo kujibu swali la nyongeza; Chenge alisema - "toka lini mfanyakazi/mwajiriwa analipwa mshahara wake halafu aje kupangiwa matumizi ya mshahara wake?"
 
Na yeye anaona ametoa bonge la pointi, hayo yamekuwa yakipigiwa kelele sana upinzani
 
Swala la chakula wala halihitaji siasa mipaka lazima ifungwe kwani mwaka huu hali ni mbaya sana kwenye mavuno.

Lazima kudhibiti Chakula chetu kuuzwa nje ya nchi kiholela,hali ya chakula si nzuri na serikali ikijichanganya kuwasikiliza wanasiasa basi wajiandae kuhangaika kulisha wananchi wake.

Kama mavuno ya mwaka huuu yangekua mazuri kusingekua na tatizo lolote lakini hali ya mwaka huu kwenye mavuno ni mbaya sana na hii ni bora Magufuli akaitwa dikteta kwakufunga mipaka kuliko kuitwa mwanademokrasia ambapo baadae itagharimu maisha ya watu.

Kwa mazao yasio ya chakula wafungue mipaka lakini kwa chakula hasa mahindi na mchele wakifungua mipaka wajiandae na huo mfumuko wa bei kwani chakula si kingi nchini.
 
Kuna watu nchi hii ni wanafiki sana eti Chenge mzalendo kama Lowassa kwa lipi waliloifanyia hii nchi tofauti na kuhujumu?
 
Back
Top Bottom