Kutishiwa kwa Zitto na Mageuzi ya lazima kwa TISS

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
17,005
20,421
Sababu kuu ya mimi kuamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni kuhimiza mageuzi ya idara ya Usalama Tanzania na mfumo mzima wa ulinzi na Usalama nchini. Nilifanya hivyo baada ya utafiti mkubwa nilioufanya na kujiridhisha kwamba mfumo uliopo hauwezi kulisaidia taifa katika ulimwengu huu mpya zaidi ya kulirudisha nyuma na kudumaza utu na fikra za kijamii huku dunia ikisonga mbele katika mageuzi ya kilimwengu.

Katika kitabu cha Ujasusi wa kidola na Kiuchumi, nimeeleza mageuzi makuu matatu ya muhimu na ya lazima kwa idara ya usalama wa Taifa ambayo ni kwanza, Sheria iliyounda chombo hiki, pili ni Muundo wa Chombo hiki, na tatu ni Sera ya chombo hiki adhimu kwa uhai wa taifa letu. Kwa mjibu wa katiba ya nchi, Chombo chochote cha usalama kinachoanzishwa kwa mjibu wa sheria ya Tanzania au katiba ya Tanzania, chombo hicho kitakuwa mali ya Tanzania na kitafanya kazi kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo.

Nimeainisha mapendekezo yangu kwa sheria ya Usalama wa Taifa ambayo nafikiri kwasasa sheria hiyo ni lazima ifanyiwe marekebisho ili kuendana na mageuzi ya dunia, tuko karne ya 21 sio enzi za zamadamu. Moja ya vifungu katika Sheria ya Usalama wa Taifa iliyosainiwa 20 January 1997 na Rais Mstaafu Mzee wetu Benjamiji W. Mkapa ambavyo ni muhimu sana kufanyiwa marekebisho ni. Mfano, kifungu 14 -(1), (2),(3), (4)-(a) na (b). Kifungu cha 15 -(1),(2), (3) -(a) na (b). Kifungu cha 16-(1) (a)na (b), (2) na (3).

Leo tunashuhudia uvunjifu wa sheria na maadili ya kiutumishi kwa afisa huyu wa Usalama wa Taifa aliyekuwa katika majukumu ya kikazi katika eneo la Bunge, huku afisa huyu akifahamu wazi kuwa Bungeni Dodoma pana rekodi mbaya ya kiusalama kwa idara hiyo na vyombo vingine kutotekeleza wajibu wao wakuzuia/kufumbia macho taarifa za shambulio la Mbunge Tundu Lissu ambapo hadi leo hakuna aliyekamatwa kwakuhusika.

Sasa leo afisa huyu anatumia upinde uleule unaoogofya watu unaohusu kumuua mbunge sawa kabisa na jaribio la kumuua Lissu, na eneo ni lilelile la Kibunge. Hapa afisa huyu ameichafua Idara na vyombo vingine vya ulinzi hali inayowezafanya umma utafsiri kama huyu Afisa ndie muhusika wa jaribio la kumuua Lissu ama anajua ama vyombo vinajua na ni sehemu yao ya utendaji kibunge.

Sheria ya Usalama wa Taifa inasema wazi kuwa si wajibu wa Idara hii wala Afisa Usalama wa Idara hiyo kufanya kazi za kukamata, kufokea, kutukana, kutishia, kufikisha mahakamani, kuadhibu, kung'ata na makeke yote nk, (law enforcer). Hizo ni kazi za kipolisi na sio TISS, Chombo hiki ni kitakatifu, kazi yake kuu ni kunusa taarifa/habari na kuzichakata ziwe nyeti ama krimu (classfied) nakisha kushauri mamlaka (sponsor) hatua za kuchukua. Kwa lugha rahisi nikuwa hata afisa usalama akakukuta unapanga kuiba, anaweza kushirikiana na wewe mkaiba wote mkala vizuri mtonyo wenu, lakini akipotea tu jumba bovu linakuangukia wewe, au mnaweza kukamatwa pamoja na mkaenda mahabusu/jela pamoja lakini yeye yuko kazini dhidi ya wizi wako na mtandao wako.

Katika kitabu cha Ujasusi nimehimiza muundo wa Idara ambao umepitwa na wakati ubadilike, muundo huu unahusu kuanzia uajiri (recruiting) na mengineyo, Mfumo wa chama kimoja wa 1962 ulikuwa ndio mfumo wa uajiri wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, na ndio ulikuwa mfumo wa ajira zingine, huwezi kuingia katika vyombo vya ulinzi na usalama bila kupita TANU YOUTH League/UVCCM. Hadi ilipofika 1992 ndipo mfumo huo ulianza kutoweka katika sekta zungine, lakini katika vyombo vya dola haukutoweka kabisa, Hivi leo watumishi wa vyombo vya dola wengi walioingia kazini kuanzia 1992 kurudi nyuma hadi 1962, hawa ni makada wa chama cha mapinduzi 100%. Wengi wao lei ni watu wazima ndio ma RPC, OCD na wakuu wa vitengo mbalimbali katika vyombo vya utumishi na vya dola, Hivyo ukimuona RPC anashangilia ccm ikishinda sio kosa lake bali itikadi kwake imekolea na aliingia jeshini kwa tiketi ya chama na sio professional yake.

Kizazi kilichoingia kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama miaka ya kaziribu angalau hiki msingi wa kuingia kwao ni elimu, undugulaizesheni na kuipenda kazi husika, japo ukada bado una nguvu ndani ya vyombo hivyo, kwamba leo unaweza kuona maajabu Kada wa ccm mfano Katibu mkuu au Mweneza maneno ananguvu kwenye vyombo vya dola kuliko RPC.

Sera ama Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi, hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe na Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI). Hapa ieleweke sana, sina maana biashara na makampuni ya uwekezaji yawe ya vyombo hivyo vya ulinzi, au yawe ya serikali, la hasha, nina maana pana zaidi kwamba ushughulikiaji wa taarifa kwa sasa kutoka taarifa za kisiasa zaidi, sasa iwe taarifa za uchumi na biashara zaidi na kuzipa ulinzi shughuli na biashara zote za uwekezaji wa ndani na wawekezaji wake.

Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.

Siku moja Luten Kanali Likvol Shekvov mkufunzi wa tabia na hisia za kibinadamu katika chuo cha majasusi cha Russian Federal Security Service (RFSS), alibainisha kuwa hulka za kibinadamu huathiriwa na unafiki, lakini unafiki usio na bughudha "unaolipa zaidi" ni ule ufanywao na wazee. Tafsiri yake kifalsafa alikuwa analaani wazee kujifanya hawajui njia na kuacha vijana wakienda mbio kwakupita porini. Chuo hiki ni maarufu ulimwenguni kwakufundisha majasusi, na hasa ufundishaji wa somo maarufu liitwalo ujasusi wa kisaikolojia (Forensic psychology). Ndani ya kozi hii ndimo huzaliwa ama hupatikana majasusi wabobevu wa saikolojia ya binadamu na mazingira ambao kwa lugha ya kijasusi huitwa Profiler.

Kwa undani zaidi, usiteseke, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi popote ulipo duniani.

Leo weekend tumeingiza katika promosheni nakala tano za kitabu cha Ujasusi , tunauza kila nakala kwa 50,000/=.

Lipia kwa 0715865544/0755865544 kisha tuma majina yako na mahali ulipo.…

Na Yericko Nyerere
IMG_20190119_083946_914.jpg
IMG_20190119_084159_155.jpg
 
Yericko bana?

Kwanza unatakiwa kuwalipa Jamiiforums kwa kutumia jukwaa lao kutangaza biashara yako. Kwa mtu muungwana lazima kwanza angelipia kabla ya kuanza kutangaza biashara.

Pili, Siku hizi kila mtu anadai ametishiwa na TISS wakati hao TISS wa kweli hawajulikani na hata ofisi zao huwezi kuingia bila ruhusa maalum.

Baada ya kesi yake mahakamani kukosa nguvu ya kisiasa kwa sasa ameenda bungeni kutafuta kiki nyingine ya kisiasa kupitia TISS.
 
Yericko mkuu hivi unamuamini Zito kweli kwenye hilo saga? Zito anaumwa kisaikolojia anaishi kwa mawazo sana MTU kama huyo hata ukimuangalia tu anahisi unataka kumfanyia kitu kibaya. Bahati mbaya zaidi mkiambiwa kitu na MTU wa upande wenu akili zenu mnaziweka kwenye freezer kabisa, think deep mkuu.
 
H

Na Yericko NyerereView attachment 998717View attachment 998718
Hivi barua zake za maspeaker na macg jumuia ya madola zishajibiwa kweli? Hilo hajamaliza ashaanzisha jingine? Ili mradi tu kuwachafua wenzake. Hizi kiki yetu macho. Instinct zinaniambia bwana zuberi ndo anaenda kumaliza utumishi wake wa siasa yungali kijana kabisa, alishindwa kuchanga karata zake vizuri alipokuwa na nafasi nzuri. The last kick of the dying horse.
 
Zito anatafuta kiki kwa nguvu zote kwa sababu anajua Mbowe yupo gerezani hivyo makeke ya chadema yamepungua. Anajua kabisa alifanya kosa kuingia vikao visivyo muhusu na kufanya fujo, pia anajua hayo aliyoanzisha hayana ushahidi wowote. Huyu apuuzwe tu maisha yaendelee.
 
Ndugu zangu,hakuna kipindi ndugu Zitto Mbunge wa Kigoma Ujiji alipata kuhaha kama sasa-kwa nini?
Wakati mwingine anahaha hadi inapelekea kwa yeye kuonekana analazimisha ili ionekane anapambania jambo fulani!

Lakini kwanini sasa!?

Matukio mengi hasa la jana lina walakini na hii ni kuonyesha huyo bwana Siasa anataka SIFA?

Ana amepima na kuona kwamba ni vigumu kwake kurejea Bungeni na sasa anaiishi ile dhana ya MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA?

Nisaidie tafadhari jawabu la....!
 
Kwanini Jiwe anahaha na hana amani kabisa licha ya:

1. Kuweka spika wake bungeni.

2. Kuzuia bunge LIVE isipokuwa yeye yuko LIVE muda wote.

3. Kupiga marufuku mikutano ya siasa kinyume na katiba isipokuwa kwa CCM.

4. Kuteka, kuua na kufunga kila mkosoaji.

5. Kudhibiti blogs, vyombo vya habari, mitandao na majukwaa huru.

6. Kuzindua mpaka miradi koko.

BADO WATU HAWAKUELEWI TU !!!!
 
Hivi mnamchukulia Ndugai kama mtu wa kawaida, huru na anayejua na kutimiza wajibu wake?
 
Ndugu zangu,hakuna kipindi ndugu Zitto Mbunge wa Kigoma Ujiji alipata kuhaha kama sasa-kwa nini?
Wakati mwingine anahaha hadi inapelekea kwa yeye kuonekana analazimisha ili ionekane anapambania jambo fulani!

Lakini kwanini sasa!?

Matukio mengi hasa la jana lina walakini na hii ni kuonyesha huyo bwana Siasa anataka SIFA?

Ana amepima na kuona kwamba ni vigumu kwake kurejea Bungeni na sasa anaiishi ile dhana ya MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA?

Nisaidie tafadhari jawabu la....!
Ana haha kwasababu kuna presidential vacuum.....nyota zake za kua raisi zimeanza kung'aa yeye ni presidential material time will say.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko mkuu hivi unamuamini Zito kweli kwenye hilo saga? Zito anaumwa kisaikolojia anaishi kwa mawazo sana MTU kama huyo hata ukimuangalia tu anahisi unataka kumfanyia kitu kibaya. Bahati mbaya zaidi mkiambiwa kitu na MTU wa upande wenu akili zenu mnaziweka kwenye freezer kabisa, think deep mkuu.
Iwe tukio la kweli au laa, bado logic ya andiko haibadikiki, uhitaji wa mageuzi ya TISS ni muhimu kuliko chochote
 
Back
Top Bottom