Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,442
Tusijidanganye. CCM hawana nia ya kuona Tanzania inapata Katiba mpya inayotoa fursa bora katika utawala wa sheria nchini na ushindani sawa wa vyama vya siasa. Hilo halitakuja kutokea hata siku moja.
Kutegemea hilo litatokea ni sawa tu na mashabiki na timu zao za Simba, Azam, Kagera, Mtibwa nk, leo waambiwe Yanga wakiwa mabingwa wa ligi kuu, watasimamia kutungwa sheria mpya za Ligu Kuu Tanzania, na watakakikisha kanuni watakazosimamia kutungwa zitakuwa za usawa kwa timu zote! Dream on.
Ndio maana kwa mfano, wakati watu wanaongelea Katiba mpya yenye kuruhusu kushitakiwa kwa viongozi waliokuwa madarakani, CCM wanaongeza kinga ya kutoshitakiwa kwa viongozi wengi zaidi waliokuwa madarakani!
Tunachotakiwa kufanywa ni kuweka mkakati wa kuwa na uongozi wa mseto wa mpito wa kipindi fulani ambao ndio utasimamia serikali kufanya mabadiliko ya Katiba na Tume huru ya Uchaguzi, ili baada ya hapo ndio tuingie kwenye uchaguzi mkuu mpya.
Bila hilo hakuna Katiba mpya Tanzania ambayo itakidhi utashi wa vyama vyote vya siasa nchini, na hata katiba mpya ikitungwa na ikawa imesimamiwa na CCM iliyopo madarakani, tunajua itakuwa Katiba ya namna gani.