Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,640
- 26,965
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kiongozi akila rushwa katika shughuli za kiserikali, aliyepokea rushwa hana uthubutu wa kumchukulia hatua mtoa rushwa.
Wachina wanajulikana, na siyo siri, kutoa rushwa katika kupata miradi mingi ya ujenzi wa barabara.
Mfano mkubwa ni barabara za BRT mjini Dar es salaam.
Tetesi tunazisikia, lakini matokeo ya rushwa yanaonekana wazi.
Wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge Morocco miaka mitano iliyopita , tulikiwa tunaona mitambo mingi na wafanyakazi wengi barabarani, na maendeleo ya kasi ktoka kwa yule mkandarasi toka Japan.
Sasa hivi mchina amejijengea himaya barabara zote toka Airport hadi Boko, Mwenge Ubungo, Ubungo Kimara.
Na mchina anaenda kwa kusuasua, hakuna lolote tunalolishuhudia barabarani ,ila mateso ya foleni.
Waziri wa Ujenzi majuzi kaleta soo barabarani kwa mkandarasi, lakini hakuna lolote linalotokea.
Barabara hizi hazikamiliki kesho wala keshokutwa.
Hiyo ni dalili tosha kuwa mchina anaona, “mtanifanya nini?”
Kila nikipita hizi barabara nakerwa sana!
Lakini ndio namkumbuka Mwalimu na maono yake kwa mtu aliyekula rushwa.