Uchaguzi 2025 Kusini Pemba: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580

Pemba Kusini.jpg

Misamiati:

Baraza: Wilaya
Wadi - Kata

Mkoa wa Kusini Pemba moja wapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania unaopatikana kusini mwa Kisiwa cha Pemba huko Zanzibar wenye Makao makuu yake huko Chake Chake. Mkoa una wilaya mbili tu, ambazo ni Mkoani na Chake Chake

Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 idadi ya watu katika Mkoa wa Kusini Pemba ni 271,350; wanaume 131,373 na wanawake 139,977 na Idadi ya Kaya ni 47,786

Mkoa huu una Halmashauri mbili (2) na majimbo ya uchaguzi tisa (9) ambapo Jimbo la Mtambile linaongoza kwa kuwa na watu wengi (37,945) likifuatiwa na Jimbo la Mkoani (watu 37,072). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Chake Chake ambalo lna watu 25,201.

Majimbo ya Kusini Pemba ni pamoja na;
  1. Chake Chake
  2. Wawi
  3. Ole
  4. Chonga
  5. Ziwani
  6. Chambani
  7. Kiwani
  8. Mtambile
  9. Mkoani
Hali ya Kisiasa

Hali ya Kisiasa kufuatia uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alitangazwa mshindi wa nafasi ya Urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27% huku mpinzani wake Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87%. CCM na ACT-Wazalendo ndizo zilizoshindana kwa karibu, huku kila moja ikipata ushindi katika baadhi ya majimbo.

CCM ilifanikiwa kupata ushindi mkubwa katika majimbo kama Chake Chake, Wawi, Chambani, Ziwani, Mkoani na Kiwani. Ushindi wa CCM katika mkoa huu unaashiria kuwa bado inaungwa mkono na sehemu ya wapiga kura.

Vyama vingine kama ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, ADA-TADEA, na UDP vilipata kura chache sana, na havikuweza kuleta ushindani mkubwa katika mkoa huu.

Japo CCM ilishinda uchaguzi huo kwa asilimia kubwa, matokeo yalizua malalamiko makubwa kutoka Vyama Vya Upinzani, ambapo ilidaiwa kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Maandamano na machafuko yalitokea baada ya uchaguzi, huku jumuiya za kimataifa zikikosoa mchakato wa uchaguzi na mwelekeo wa demokrasia visiwani Zanzibar. Serikali ya CCM ilikataa tuhuma hizo na kuendelea na utawala wake.

Soma, Pia:
+ Yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Mkoa wa Kusini Pemba
 
Back
Top Bottom