Kushushwa kwa PAYE kupandishe morali

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
RAIS John Magufuli ameonesha dhamira yake ya dhati ya kuboresha hali ya Mtanzania, baada ya kuwakumbuka wafanyakazi kwa kushusha Kodi ya Mshahara (PAYE) hadi kufikia asilimia tisa kutoka 11 ya sasa kuanzia mwaka wa fedha ujao wa 2016/17.

Dhamira hiyo ya dhati iko katika hotuba aliyoitoa juzi mjini Dodoma wakati akihutubia Taifa katika Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa kwenye Uwanja wa Jamhuri na kusema amefanya hivyo ili kuwapunguzia mzigo wa kodi watumishi.

Akihutubia umati wa wafanyakazi uliohudhuria sherehe hizo, Rais Magufuli alisema Serikali yake kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake, imeamua kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia tisa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hii ni habari njema si kwa wafanyakazi tu hata familia zilizo nyuma yao. Imani yetu ni kwamba hatua hiyo sasa, itaongeza morali kwa wafanyakazi. Hata hivyo, Rais Magufuli amewakumbusha watunga sheria nchini yaani wabunge kwamba nao wana wajibu katika hili kwani wao ndio wanapitisha Bajeti ya Serikali itakayosomwa bungeni siku chache zijazo.

Na hili tunaamini limesikika kwa wahusika. Pia Magufuli pamoja na kutoongeza mishahara kwa watumishi, lakini akasema kwa kadri hali ya kiuchumi itakavyokuwa inaimarika, ndivyo itamwezesha kufanya maamuzi aongeze kwa kiasi gani. Wafanyakazi wana imani kubwa na Rais Magufuli. Hilo halina ubishi.

Tunasema hakuna ubishi kwa kuwa ni kiongozi anayetimiza ahadi zake. Wakati anafanya kampeni zake, alisema watumishi wanapata shida kutokana na makato ya mishahara, hivyo hana budi kulishughulikia hilo akiingia madarakani, sasa ametimiza ahadi hiyo.

Katika hotuba hiyo, akasema Serikali inaendelea kuangalia vyanzo vyake vya fedha ikiwemo hatua aliyokwishachukua ya kuwabana wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa fedha nyingi za Serikali. Rais Magufuli akasema ni nafuu ya shetani kuliko watumishi hewa na kubainisha kuwa mpaka juzi, watumishi hewa walikuwa wamefikia idadi ya 10,295 serikalini.

Imani yetu na ya Watanzania ni kwamba uchumi ukiimarika, Rais atatimiza kabisa ndoto za wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara. Tunasema hivyo kwa kuwa hakuna maana kuongeza mishahara ambayo haiwezi kulipika kama ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma ambapo upandishaji huo usioakisi hali halisi ya kiuchumi.

Suala hili limekuwa likisababisha kuwepo kwa madeni makubwa yaliyokuwa yakizalishwa katika maadhimisho ya Mei Mosi na yameendelea kuwa mzigo mkubwa kwa viongozi wa Serikali za awamu zote.

Pia tunampongeza Rais Magufuli kwa kuliona pengo kubwa lililokuwepo huko nyuma kati ya mfanyakazi wa mshahara wa chini na ule wa juu na kuamua kushusha mshahara huo hadi Sh milioni 15 ili hizo zingine zipelekwe kwa hao watumishi wa mishahara ya chini.

Rais Magufuli akasisitiza kwamba wasiotaka kufanya kazi kwa kuwa walikuwa wakipata mishahara mikubwa, waache kazi mara moja kwani haiwezekani katika nchi moja mtu mwingine anapata mshahara wa Sh milioni 30 hadi 40, huku mwingine anapata mshahara wa Sh 300,000.

Kilichobaki sasa, ni wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla. Katika hili, akawatia moyo kwani anasema ambao ni wachapa kazi wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na uaminifu, waendelee kufanya kazi kwa kujiamini, kujituma bila kuwa na wasiwasi wowote kwa kuwa yeye yuko pamoja nao.
 
hili la kuahusha P.A.Y.E kwa 2% ambayo ni wastani wa shs.1,100 ni kama lile la kuwaambia walimu wapande bure daladala
 
Usanifu ni mbaya sana, what kind of kidding is this?
 
...unapuguza 2% ya kodi ambayo ni sawa na 1,100, unapandisha sukari 1,200 halfu unataka watu wakupigie makofi na vigeregere!!!!???...huu ni upuuzi wa kiwango cha lami...
 


Nikiangalia Sana Ni kama unalipwa kwa ajili ya kumsifia maghufuli
 
Ni mtu pekee aliyekosa ufahamu ndiye atakayeshangilia kushuka kwa koda kwa kiwango cha sh. 3,800. Huku ni kucheza na akili za wajinga.
 
Nchi hii hadi pale wananchi ujinga utakapowatoka ndipo maendeleo yatakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…