Kushuka kwa thamani ya shilingi, zigo lililomshinda Mwigulu kulielezea kiuchumi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,211
26,213
Kulingana na data zilizopo hata mtandaoni, shillingi yetu imeshuka kwa kiwango cha kutisha.

REKODI ZIPO HIVI:
Mwaka 2020. 1 Dollar -Tshs 2,314.8
Mwaka 2021. 1Dollar -Tshs 2,314.3
Mwaka 2022. 1Dollar- Tshs 2,326.1
Mwaka 2023 1Dollar- Tshs 2,419.6
Mwaka 2024 1Dollar- Tshs 2,463.5(Jan -June)
Sasa hivi June 2024 1Dollar -Tshs 2,627.5

Hizi ni data unaweza kuzipata hata Bank of Tanzania(Benki Kuu)

Lakini blck Market rate kwa sasa hivi mitaanai 1Dollar-Tshs 2,850, na dollar haipatikani hata benki zetu.

KWA NINI?

Dollar ZOTE ZINANUNULIWA NA MAKAMPUNI YA KI CHINA, kwa bei ya Tshs 2,850 tena bila kupepesa macho.

Nashangaa wabunge hawambani Waziri wa Fedha kuwa hili ni janga la kitaifa. Na janga hili limeanza baada ya mwaka 2022.

Dr wa uchumi, Dr Mwigulu Nchemba hapa inabidi awajibike na madhara ya kuwapa wachina kazi zote za ujenzi na wao wachina wanakausha Dollar katika uchumi wetu.
 
Kwa mujibu wa Dokta mwenyewe, uchumi wetu unakua vizuri, na nchi yetu deni la taifa linahimilika, na bado tunakopesheka.😂😂😂
Na tunatarajia kuwa na deni la trillion 120 bye Oct 2025.. yaani Samia kwa miaka minne atakuwa amekopa trillion63.Lakini ni huyuhuyu mwiguru chemba na January na kinana na ndugu nape nauye walisimama bungeni nakusema serikali ya maguru ilikopa pesa nyingi sana abazo zilikuwa trillon 7 kwa miaka 5.Nashangaa wao ndani ya muaka 5 watakiwa wamekopa trillion 63..Hivi Hawa kwanini tuwaamini
 
Inawezekana kweli, lakini mimi tatizo langu na Mwigulu ni jinsi asivyoelezea kwa nini Dollar haipatikani kwa kawaida yake kwenye uchumi.
All imports require this covertible currency.
Dollar rate inakua determined na balance of trade i.e imports vs exports tanzania has imbalance terms of trade kila kitu tuna import na sie tuna export kdgo mama aongeze nguvu kwenye tourism inaweza kutuokoa.
 
Dollar rate inakua determined na balance of trade i.e imports vs exports tanzania has imbalance terms of trade kila kitu tuna import na sie tuna export kdgo mama aongeze nguvu kwenye tourism inaweza kutuokoa.
Tuna import mno. Inatakiwe tuzalishe wenyewe na vingine tuanze kuexport nje ndio tutabalance trade. Utalii impact yake ni ndogo kwenye uchumi kwa kuwa mahoteli mengi na sekta nzima ya utalii imeshikwa na makampuni toka nje. Kwa hiyo hela ya utalii inarudi hukohuko nje.



Kwa hali ilivyo dola itafika 3000. Na wakiendelea kusifiasifa dola itakuja kuwa 10,000.
2025-$1=Tsh 3,000/= +

2028-$1=Tsh 10,000/=+



Anaupiga mwingi mno 🤣
 
Back
Top Bottom