JEJUTz
Member
- Aug 22, 2024
- 68
- 171
Inasikitisha sana kuona vita vimegeuzwa kama ushabiki wa mpira.Huku watu wanakufa, watu wanapata ulemavu wa kudumu, wengine wanapoteza kila kitu!
Wengine wanatazama hii vita kwa itikadi za kidini kitu ambacho si kweli.Ukiingia mitandaoni watu wanabishana mpaka kutoleana maneno makali kisa vita vya Israel na Palestina like serious?
Tanzania tuliingia vitani na Uganda miaka mingi imepita lakini madhara ya vita hivyo yaliendelea kuonekana kwa miaka na miaka.
Sisi Watanzania hatuhusiki na wala hatufaidiki kwa chochote juu ya vita vinavyoendelea huko Mashariki ya kati.Ni ulimbukeni tu na fikra potofu.
Unakumbuka milipuko ya mabomu Mbagala na Gongo la Mboto? Basi sekeseke na pata shika hilo huko Mashariki ya kati ndio maisha yao.
Si vizuri na si vyema kushangilia pale mwenzako anapopatwa na matatizo.Kuna msemo unasema hivi 'mwehu anachekesha kama si ndugu yako'
Tuachaneni na siasa za dini badala yake tuombeeni amani na utulivu ili dunia iwe sehemu salama ya kuishi.
Ms.JEJUTz