sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,230
Chanzo ni sio bbc wala Aljazeera, ni makao makuu ya kanisa katoliki nchini Vatican kwenye kwenye maktaba ya Idara ya Mafundisho ya Imani >> Dicastery for the Doctrine of the Faith << title imeandikwa 3 November 2023.
Tamko liliandaliwa na Idara ya mafundisho ya imani kisha Papa Francis akaidhinisha, kwa lugha nyepesi ni kwamba tamko hili linawahusu wakatoliki wote duniani wakiwemo wa hapa Tanzania.
Hii ni tafsiri ya kilichoandikwa…
Tarehe 14 Julai 2023, Idara ya mafundisho ya imani ilipokea barua kutoka kwa Jose Negri, Askofu wa Santo Amaro nchini Brazil, Kauliza maswali kadhaa kuhusu ushiriki katika sakramenti ya ubatizo na ndoa kwa watu waliobadili jinsia na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Baada ya kufanya utafiti kuhusu suala hili, Halmashauri hii inajibu kama ifuatavyo.
Majibu yafuatayo kimsingi yanarudia yaliyomo muhimu ambayo tayari yalishaelezwa na Halmashauri hii kuhusu suala hili hapo awali.
1. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kubatizwa ?
Mtu aliebadili jinsia ambaye amepitia matibabu ya homoni na upasuaji wa kubadilisha jinsia anaweza kupokea ubatizo kama ilivyo kwa waumini wengine wa kanisa katoliki ikiwa hakuna hali ambayo italeta taharuki kwa kwenda kinyume na utaratibu wa zoezi la ubatizo. Kwa watoto au vijana wadogo wenye mashaka katika ubadilishaji wa jinsia, wakiwa tayari na wanapotaka wanaweza kupokea ubatizo.
Kwa wakati huo huo, Vifuatavyo ni muhimu kuvizingatia, hasa wakati panapokuwa na shaka kuhusu hali ya maadili, lengo au kuhusu nia yake kuelekea neema.
Katika Ubatizo, Kanisa linafundisha kwamba, wakati sakramenti inapopokelewa bila toba kwa dhambi kubwa, anaebatizwa hawezi kupokea utakatifu wa kiroho, ingawa atatambulika kapata ubatizo. Katekisimu inasema: misingi ya Kristo na Kanisa iliyofikiwa na Roho, haifutwi bali inabaki milele ndani ya Mkristo kama hali chanya kuelekea neema kama ahadi na uhakikisho wa ulinzi takatifu na kama wito wa ibada ya kimungu na utumishi wa Kanisa.
Mtakatifu Thomas wa Aquinas alifundisha kwamba wakati kitu kilichokuwa kikizuia neema ya Mungu kabla ya ubatizo kinaondolewa kwa mtu ambaye aliebatizwa bila kuwa na nia sahihi, alama maalum ya kiroho wanayoipata wakati wa ubatizo inawasaidia kuwa wazi zaidi kupokea neema ya Mungu. Mtakatifu Augustine wa Hippo alikumbusha hali hii akisema kwamba, hata kama mwanadamu anajikuta katika dhambi, Kristo haangamizi alama aliyopokea kwake katika Ubatizo, alama hii imemweka wazi kama mali yake.
Hivyo, Inatupasa tuelewe kwamba Papa Francis alitaka kusisitiza kwamba ubatizo ni mlango unaomruhusu Kristo kujiweka ndani yetu na sisi tuweze kuzama katika imani yake. Hii inamaanisha kwa vitendo kwamba hata milango ya Sakramenti haipaswi kufungwa kwa sababu yoyote ile hata kama mtu kabadili jinsia ama anafanya mapenzi ya jinsia moja. Hii ni kweli hasa linapokuja suala la sakramenti ya mlango wa ubatizo...., Kanisa katoliki si ofisi ya forodha, ni nyumba ya baba ambapo kuna nafasi kwa kila mtu na maisha yao yenye taabu.
Hivyo, hata wakati shaka zinabaki kuhusu hali ya maadili ya mtu au nia yake kama ni nzuri ama mbaya kuelekea neema ya Bwana, hatupaswi kamwe kusahau upendo wa dhati usio na masharti wa Bwana, Hata pale mtu anapokosea mara kwa mara, Mapenzi ya Mungu yapo wazi na anaweza kumrudia kutengeneza uhusiano imara. Mapenzi haya yapo wazi ila hubadilika kwa maana hatuwezi kutabiri matendo yetu ynavyoweza kuathiri uhusiano. Hata ale ambapo mtu anaefanya juhudi kumrudia Bwana ana uwezekano wa kuendelea kufanya makosa, hatuwezi kubeza jitihada zake za kutaka kubadilika. Hivyo yatupasa tuthamini jitihada zao kila moja wetu anaetaka kubatizwa na kuungana nao kwenye safari ya kikristo
2. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa mzazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki ?
Mtu mzima aliebadili jinsia anaweza kuruhusiwa kuchukua jukumu la kuwa mzazi wa ubatizo. Hata hivyo, busara ya kichungaji inahitaji isiwezeshe zoezi hili ikiwa kuna ukiukaji wa utaratibu wa ubatizo unaoweza kuleta taharuki ama kuidhinisha kwa njia isiyofaa.
3. Je, mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa?
mtu aliebadili jinsia anaweza kuwa shahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayotoa ubatizo kwa waumini wengine.
4. Je, watu wawili wa jinsia moja wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtoto ambaye anapaswa kubatizwa, ikiwa mtoto huyo wamemuasili ?
Ndio inawezekan, Ili mtoto apate ubatizo, lazima kuwe na matumaini yenye msingi kwamba ataelimishwa katika dini ya Katoliki (angalia kanuni ya 868 1, 2 au CIC; kanuni ya 681, 1, 1st CCEO).
5. Je, watu wenye jinsia sawa wanaoishi pamoja wanaweza kuwa kuwa wazazi wa ubatizo kwa mtu ambae tayari kabatizwa ?
Kulingana na kanuni ya 874 1, 1o na 3o CIC, yeyote mwenye uwezo na "anaishi maisha yanayolingana na imani na jukumu analochukua" anaweza kuwa mzazi wa ubatizo. Hali ni tofauti ambapo kuishi pamoja kwa watu wawili wa jinsia moja siyo tu kuhusiana na kuishi pamoja, bali ni wawe na uhusiano thabiti unaofahamika na jamii.
Kwa hali yoyote, busara ya kichungaji inahitaji kuzingatia kwa busara kila hali, ili kuhifadhi sakramenti ya ubatizo na hasa upokeaji wake, ambao ni mali yenye thamani inayopaswa kulindwa, kwani ni muhimu kwa wokovu.
Kwa wakati huo huo, ni muhimu kuzingatia thamani halisi inayotolewa na jumuiya ya Kikristo kwa majukumu ya wazazi wa kibatizo, jukumu walilonalo katika jumuiya, na heshima wanayoiweka kuendana na mafundisho ya Kanisa. Mwishowe, inapaswa pia kuzingatiwa kwamba kuna uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwingine kutoka familia ambaye anaweza kuhakikisha uhamisho sahihi wa imani ya Katoliki kwa mtu anayebatizwa, huku wakijua kwamba wanaweza bado kumsaidia mtu anayebatizwa, wakati wa ibada, si tu kama wazazi wa kibatizo bali pia kama mashahidi wa tendo la ubatizo.
6. Je, wapenzi wawili wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa ?
watu wenye jinsia zinazofanana wanaopendana na kuishi Pamoja wanaweza kuwa mashahidi wa ndoa za kikatoliki chini ya misingi sawa na ile inayoruhusu waumini wengine kuwa mashahidi wa ndoa.