Kupotea kwa Titan mwaka 2023

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
519
915
Usichokijua kuhusu marowani ndogo iliyopotea kwenye bahari

Moja kati ya taarifa zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ni kupotea kwa manowari ndogo nchini marekani iliyowabeba watalii waliotaka kujaribu kwenda chini ya bahari kuangalia masalia au mabaki ya Meli kubwa ya titanic.

IMG_20230623_121116_359.jpg

Turudi nyuma kidogo mwaka 1912 kati ya tarehe 14 au15 Aprili dunia ilipatwa na mshtuko baada ya kutokea kwa ajali ya Meli kubwa ya Titanic ilyobeba abiria takribani watu zaidi ya 2,208.

Titan%20%E2%80%93%201.jpg

Iliweza kuua takribani watu 1500 huku wengine 708 waliweza kuokolewa wakiwa hai. Imepita zaidi ya miaka 111 Toka kutokea kwa ajali lakini mwaka 2023 kumetokea tukio jingine la kusikitisha ambalo limewaacha watu wengi na huzuni kubwa.

IMG_20230623_121116_388.jpg

Tarehe18 mwezi wa sita kikosi cha watu wa tano wakaamua kupanga safari ya kuelekea majini kufanya uchunguzi || udadisi kuhusu Meli ya titanic illyozoma miaka111 iliyopita. Safari ilianza siku ya jumapili saa 12pm mchana GMT na EAT ni 08am asubuhi.

IMG_20230623_121116_403.jpg

Kikosi cha watu watano ndani Kuna bilionea mmoja anaitwa Hamish Harding akiwa na jamaa anaitwa Shahzada Dawood na mwanae suleman pia Kuna mzamiaji mashughuli wa nchini France anaitwa Paul-Henri Nargeolet pamoja na Stockton Rush huyu ni CEO wa OceanGate.

Titan%20%E2%80%93%204.jpg

Safari ilikua ya siku 4 siku tatu 3 ndani ya maji na Kulikua na Gharama za kulipia ilikua ni dollar $250,000 sawa na milioni mia tano tisini na tisa na laki tano kwa Kila mmoja kulikua na watu watano ila abiria watatu walilipa.

3123.jpg

Baada ya safari kuanza na kupita zaidi 1hr na dakika 45 walipoteza mawasiliano kati ya waliokuwepo kwenye chombo na watu wa nchi kavu ilikua saa 1.45pm GMT na EAT 9:45am.

Kwa vile walikua wanaingia ndani ya maji na akuna hewa ya oksijeni wakaweka mfumo wa Oxygen ambao walitakiwa watumie masaa 96 Ili waweze kufika na kurudi salama ndani ya siku 4 tu.

Titan%20%E2%80%93%205.jpg

Walitakiwa mpaka kufikia alhamic wawe nchi kavu saa 10am kwa Gmt na Eat ni saa 6am. Kwaiyo adi kufika alhamic saa 7 mchana hewa ya oksijeni imekwisha chombo akijaonekana, akijapatikana Wala akuna abiria aliyeweza kuwasiliana nao.

Meli ya titanic imezama kwenye kina kirefu sana zaidi ya futi 12,500 wakati manowari inapoteza mawasiliano ilikua kwenye kina cha futi 4000 kwaiyo walibakisha futi 8500 Ili waweze kufika ila hawajafika wamekufa.

images%20-%202023-06-23T121526.238.jpg

Wako wapi ? Je ni wazima maana Kampuni ya OceanGate wamesema kuwa watakua wameshakufa kutokana hewa ya oxygen kuisha muda? Ila Mungu Anajua zaidi inawezekana kuwapata vipi unasemaje tabia ya kufanya fanya tafiti kwe Kila kitu ni salama?
 
Hili tukio ni ukumbusho mkubwa kuwa kuna wakati pesa si kila kitu.

Na utajiri wao wote mwisho wa siku kukosa oxygen kumewaondoa duniani.
 
Mkandamizo (mgandamizo?) unasababishwa na maji unaongezeka kadiri kina knapoongezeka.
Kuna taarifa inasema hapo juu mwaka jana 2022 kimefanya safari 10,hilo swala la mkandamizo halikuwepo...?
 
Kuna taarifa inasema hapo juu mwaka jana 2022 kimefanya safari 10,hilo swala la mkandamizo halikuwepo...?
Kina cha maji yalipo mabaki ya Titanic ni kama kilomita 4! Inawezekana hizo safari zilizopita hazikua za kina hicho. Pia inawekana kuna baadhi ya sehemu za chombo zilianza kuchoka hivyo kushindwa kuhimili mkandamizo.
 
Hawakufa kwa kuishiwa oksijeni, chombo kilizidiwa na mkandamizo wa maji kikapasuka (implosion).
Engineer wao wote ni kenge fizikia ya form nyoya kabisa hiyo.. pressure ya maji inazidi kadri kina kinavyoongezeka, sasa walicalculate vipi hao kenge, kina cha mita 4000 tu kimezidiwa na mgandamizo, futi 4000 ilikuwa ni ⅓ ya safari kamili ambayo ni futi zipatazo 12,000.
 
Kuna wafanyakazi wawili waliwahi kuhoji kuhusu uwezo wa chombo na vipimo muhimu ili kuthibitisha ubora na uwezo wa chombo ila waliondolewa kazini.
 
Au vip mwanangu hayo yote ya phsyc wewe ukiwa umeyajua kutoka kwa hao unaowaita kenge ila daah wabongo sisi tuna laana aisee yaani tuna laana ya milele unatumia simu na tech yao kuwaita kenge alafu cha kushangaza kabisa bado unatumia theory zao na princple zao ambazo umezisoma kwenye vitabu vyao baada ya wao kutumia muda mrefu kufanya research kwa gharama zao ndo wakakuandikia vitabu ili wewe pangu pa ukwa! upate maarifa na ufahamu alafu unavitumia ivyo ivyo vitabu vyao kuwatukana ama kweli hii laana imetuandaman vya kutosha!!
 
Kuna wafanyakazi wawili waliwahi kuhoji kuhusu uwezo wa chombo na vipimo muhimu ili kuthibitisha ubora na uwezo wa chombo ila waliondolewa kazini.
Duh!! Basi huenda kuna jambo nyuma ya hiki kiroja.
 
Au vip mwanangu hayo yote ya phsyc wewe ukiwa umeyajua kutoka kwa hao unaowaita kenge ila daah wabongo sisi tuna laana aisee yaani tuna laana ya milele unatumia simu na tech yao kuwaita kenge alafu cha kushangaza kabisa bado unatumia theory zao na princple zao ambazo umezisoma kwenye vitabu vyao baada ya wao kutumia muda mrefu kufanya research kwa gharama zao ndo wakakuandikia vitabu ili wewe pangu pa ukwa! upate maarifa na ufahamu alafu unavitumia ivyo ivyo vitabu vyao kuwatukana ama kweli hii laana imetuandaman vya kutosha!!
Numbers don't lie..

Wao si miungu, wao wanakosea, ni kwamba watakuwa wamekosea sehemu.

Natamani kuandika kirefu, naona tutaishia kupigizana kelele tu.
 
Back
Top Bottom