Kuondoka kwa Sefue Ikulu na kupungua kwa Matamko ya Serikali

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Wakuu.
Toka Katibu kiongozi Balozi Sefue kuondoka Ikulu, tumeshuhudia kupungua sana kwa matamko ya serikali kwenye vyombo vya habari.
Mwanzoni kila baada ya siku tatu ilikua ni lazima litoke tamko la Ikulu, hata Rais akinunua kandambili mpya utasikia jamaa au Msigwa keshatoa tamko, tofauti kabisa na siku hizi ambapo matamko ni nadra sana.

Kumetokea ishu kubwa kubwa sana hapa katikakati lakini hakuna Press Release kama za Sefue na Gerson Msigwa wake, ishu kama ya bomba la mafuta ya Uganda, Sefue engekuewepo tungekuwa tumeshasikia tamko la Ikulu, Ishu ya Wamarekani na MCC yao, Uchaguzi wa Zanzibar, ishu ya mishahara ya watumishi hewa, Uhakiki wa Silaha na mambo mengi ya hivi karibuni.

Hivi sasa katibu kiongozi Eng Kijazi anapiga kazi kimya kimya kama hayupo vile, na kwa rekodi yake ya ukatibu mkuu wizara ya ujenzi enzi yuko na Magufuli na pia rekodi yake pale Ubalozini India nampongeza Magufuli kumuweka Engineer kwenye kitengo nyeti kama hicho.

Sefue alikua mtu wa media na alikua anaendana sana na JK, lakini huyu wa sasa nadhani hata wengi wakikutana naye pale Posta jioni anagombania daladala la kwenda Mwenge wachache sana watamtambua.

Hongera sana Kijazi, piga kazi.
 
No, nadhani ni kwa vile wakati wa Semfue ndiyo JPM alikuwa ameingia madarakani, moto ulikuwa mwingi, pangua pangua ndiyo ilikuwa inafanyika kila kukicha na hivyo matamko mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…