Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 322
- 862
Ushindi mwingine ni kufahamu udhaifu wako ni upi na uimara wako uko wapi ukijua hilo kwa sehemu wewe ni mshindi na itakusaidia kujua nani anataka kutumia udhaifu wako kwa manufaa yake.
Kuna watu ni wajanja sana wanachokifanya ni kukusoma tu kujua eneo lako dhaifu na kufuatilia je unafahamu kuwa hapo ndio dhaifu kwako? Wakigundua hujui basi wanakuja kwa mgongo wa kukusaidia kumbe wanataka kujinufaisha kupitia udhaifu wako.
Wakijua udhaifu wako upo kwenye maamuzi basi watalitumia eneo hilo kujifanya kama wanakusaidia kuamua ila kwa jicho la tatu faida inakuwa kwao zaidi kuliko kwako.
Kwa juhudi zote watu hao watajitahidi usipone ili waendelee kukutumia kimanufaa yao hivyo watajifanya wema sana ili kukupumbaza usije kushituka.
Kuwa makini sana na marafiki ulio nao na mara nyingi fanya tathimini ya mara kwa mara kuangalia wamesimamaje kwako .
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako.