Kuna wanawake wamejiingiza kwenye vikoba, michezo, upatu ambao umewafanya wawe ni watumwa wa maisha

Magical power

JF-Expert Member
Sep 27, 2022
1,510
4,146
Kuna wanawake wamejiingiza kwenye vikoba, michezo, upatu ambao umewafanya wawe ni watumwa wa

Maisha
1732465714208.jpg
.

Imefikia hatua mpaka wanaume anapotaka kumsaidia mtu anambiwa unamapaje mtu hela hiyo mimi nadaiwa kikoba

Mtu anayecheza michezo sawa na mtu anabet kila pesa huiwazia kamari tu akaizalishe😀🙌🏿

Wapo kwenye vikoba, michezo kwa pesa ya kuungaunga yaani wamefanya hata watu kula vyakula visiyo sahihi kwasababu wanabajeti pesa ya matumizi ya familia wapate pesa yao

Wapo wengine wameingia kwenye mikopo na madeni makubwa kwasababu woa hawataki kupitwa jambo, wanataka kila jambo wawepo

Wamejikuta waliingia kwenye migogoro, shida kwenye mahusiano yao na wapo waliachwa kwasababu ya madeni, kuwa busy na vikoba

Dada angu ni KWELI unatafuta kipato kwa ajili yako na familia yako basi cheza unavyoviweza acha tabia ambayo itakupa fedheha na aibu tu

Haya mambo ndio yamewafanya baadhi ya wanawake kuanza KUDANGA na kutumikishwa kimwili ili wapate pesa ya kucheza michezo na kulipa madeni wanayodaiwa kwenye chama😎.
 
Back
Top Bottom