Kuna vitu ni muhimu sana lakini havionekani katika hali ya ubora na kuna vitu ni bora lakini kuna wakati si muhimu kwa kiwango chake

Nov 6, 2016
77
271
KUWA MUHIMU NA SI BORA

Na Comrade Ally Maftah

Bahati ninayoipata kijenga marafiki imenikutanisha na Abdulkarim, katika harakati za kisanaa tukiwa katika moja ya kikao nilibahatika kuokota busara kadhaa kutoka kwa kiongozi huyu.

KUWA MUHIMU NA SI BORA

Kuna vitu ni muhimu sana lakini havionekani katika hali ya ubora na kuna vitu ni bora lakini kuna wakati si muhimu kwa kiwango chake.

Jukumu la kuchagua kuwa muhimu au bora ni la kwako,

UBORA
Kuwa bora unaweza kukutafuta kwa kujinaksi au kujiweka vitu vya kuvutia jamii na hadhira furani, ni kujiweka zaidi ya wengine katika muonekano, hapo ni nguo, mitindo ya unyoaji, nk

UMUHIMU
Kujiunda katika mfumo ambapo wewe unakuwa ni ufumbuzi wa changamoto au mwezeshaji wa jambo, umuhimu ni kufanya jamii au hadhira kutofanikisha jambo kiufasaha isipokuwa kwa mchango wako, ili kuwa muhimu lazima ujiendeleze kwenye namna ya kufikiri na kuchukua hatua kiufasaha.

MIFANO:
Chumvi ni muhimu lakini si bora, chumvi hainakshiwi sana na ni aghalabu kukuta inatangazwa sana,
Maji ni mujimu na ni mara chache kukuta yanatangazwa na kunakshiwa

ISIPOKUWA
Soda ni bora sana, hunakshiwa na kutangazwa kutwa kucha.

CHAGUA KUWA CHUMVI AU MAJI NA SI SODA.

NDIMI
Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
CCM LIA LIA


 
Back
Top Bottom