Kuna uwezekano Royal Tour haikuleta faida

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
20,188
29,648
Akiongea Leo wakati akipokea Ripoti kuhusu utendaji wa Wizara ya mambo ya nje kwenye Ikulu ya Dar, Rais Samiah amedai kwamba suala la branding sio suluhisho, kwani tumefanya branding nyingi na kutumia makampuni ya ulaya lakini hakuna faida iliyopatikana na zaidi imeleta hasara kwa serikali.

Kwa kauli hiyo ya Rais, inaonekana Royal Tour haikuleta matokeo mazuri ndio maana Rais kalalamika. Rais ametaka serikali ijikite kwenye kufanya kazi kwa bidii, na ndipo nchi itafahamika kwa kazi zake na sio kutupa pesa kwenye mambo ya branding.
 
Amejisahau tuu akajikuta anasema ukweli wake kutoka moyoni..! Na huo ndio ukweli

Hivi sasa hivi Msigwa na kundi lake wanajisikiaje? Siku kumi baada ya royotua walikuja na makala na mapicha ya magari ya watalii wakisema mama anaupiga mwingiiiii…..royotua imelipaaaaaaaaa

Sasa wameanza kunena kwa lugha wenyewe bila kulazimishwa…Rais kasema mwenyewe kuwa royotua ni hasara tupuuuuuuuu
Hahahahahahaha
 
Akiongea Leo wakati akipokea Ripoti kuhusu utendaji wa Wizara ya mambo ya nje kwenye Ikulu ya Dar, Rais Samiah amedai kwamba suala la branding sio suluhisho, kwani tumefanya branding nyingi na kutumia makampuni ya ulaya lakini hakuna faida iliyopatikana na zaidi imeleta hasara kwa serikali.

Kwa kauli hiyo ya Rais, inaonekana Royal Tour haikuleta matokeo mazuri ndio maana Rais kalalamika. Rais ametaka serikali ijikite kwenye kufanya kazi kwa bidii, na ndipo nchi itafahamika kwa kazi zake na sio kutupa pesa kwenye mambo ya branding.
duh kwa ushahidi upi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amejisahau tuu akajikuta anasema ukweli wake kutoka moyoni..! Na huo ndio ukweli

Kaongea kutoka moyoni mwake. Amedai kwamba tumewahi kupeleka tangazo CNN lakini hakuna tulichoambilia.
 
Hebu tupe Takwimu za Watalii kabla na baada ya Royal Tour.

Sio Mimi mkuu, nimemnukuu Rais Leo alipokuwa anaongea ikulu. Maana Tume ilishauri serikali iweke pesa kwenye branding kimataifa. Ndipo Rais alipopata wasaa wakuongea akaponda mambo ya branding na kwamba hayana tija. Tena akadai makampuni ya ulaya yanafaidika kwenye branding lakini nchi haipati kitu. Ndio maana nikasema inawezekana royal tour haikutudisha fedha zake.
 
Back
Top Bottom