Kuna umuhimu wa rais kufanya ziara za nje

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alifanya ziara nchini India hivi karibuni na ziara hiyo imezaa matunda makubwa kwani mbali na kusaini mikataba mbalimbali yakibiashara na serikali ya India imeipatia Kenya mkopo wa dola milioni 100 yenye riba nafuu.

Ni wakati muafaka wa Rais Magufuli atafakari upya sera zake za kutosafiri kwenda nje kwani Tanzania kama taifa tunaonekana tunajitenga na jumuia ya kimataifa wakati sisi ndio tunawahitaji wao kwa maendeleo ya kibiashara na uwekezaji.

Nakumbuka wakati wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete alifanya ziara nyingi na tuliona Tanzania ikifaidika na mambo mengi ikiwa pamoja na uwekezaji.
Tanzania haiwezi kujitenga na jumuia ya kimataifa kwani Tanzania ilikuwa ni nchi siku zote upo mstari wa mbele katika ushirikiano na jumuia ya kimataifa ndio maana serikali za awamu zote zilizopita zilikuwa zikipata misaada ya haraka pindi inapotokea shida.
 
kwa hili NAMUUNGA MKONO MAGUFULI hakuna ulazima wa yeye kuruka ruka hovyo kwenda ng,ambo ilhali hapa nyumbani kuna matatizo lukuki ya kushughulikia, mabalozi wapo wataifanya hiyo kazi hata Maiga ameshaonesha matunda ya nafasi maana Tanzania kufikia mwezi novemba mwaka jana ilipokea ugeni wa zaidi ya nchi 9 kutoka maeneo mbalimbali duniani... si kwa kuwa kenya wamefanya basi nasi lazima rais wetu aige... kila watu na taratibu zao... watakuja wenyewe au muda muafaka wa rais ukifika atafanya ziara za nje ila sio lazima kwa sasa... kwa hili YUKO SAHIHI 90%
 
Yule. Waziri. Wa mambo. Ya. Nje. Wa china. Alikuja. Tz. Kufanya. Ziara. Mweshimiwaa. Yule. Alikuwaa zake. Chato. Anagonga kengele. We.. Unamchezea. Yule.
 
Yule. Waziri. Wa mambo. Ya. Nje. Wa china. Alikuja. Tz. Kufanya. Ziara. Mweshimiwaa. Yule. Alikuwaa zake. Chato. Anagonga kengele. We.. Unamchezea. Yule.
Hicho kitu kilinishangaza sana how Waziri wa Mambo ya nje ya Marekani kufika Tanzania bila kuonana na Rais Magufuli
 
Akienda nje ataongea nini?

Mungu mjalie kiongozi wetu afya ya akili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…